Kutoka Library
Kama ulikuwa hujui naomba nikwambie kitu;
Uber hawana gari hata moja, ila ndio wanaongoza kwa kukodisha magari

Alibaba hawatengenezi bidhaa hata moja ila ndio wanaongoza kwa kuuza vitu

Netflix hawana tv chanel yoyote ila ndio inaongoza kuuza movie——✍️
Bitcoin hawana hela yeyote ila wanaongoza kuwa na biashara ya hela nyingi mtandaoni

Facebook hawapost chochote ila ndio mtandao unaoongoza kwa kutoa habari duniani

Kuna muda wazo lako tu ukiliweka vizuri litakuingizia mtonyo wa kutosha hata bila kuwekeza hela nyingi,
cha muhimu kuwa mbunifu na kuja na kitu cha tofauti ambacho kitarahisisha maisha yetu ya kila siku. Acha uoga wa kujaribu, usikute wazo lako halihitaji hata kuwa na hela nyingi ila linakutaka uwaze nje ya box na kuwa mbunifu zaidi ili uweze kufikia malengo yako.
Changamsha ubongo wako, waza na wazua jinsi ya kulitendea haki wazo lako, usifanye kwa mazoea kama watu wengine wanavyofanya ila fanya kama kijana wa kisasa na kimawazo ya kisasa halafu utakuja kunipa majibu. Kumbuka ni marufuku kukata tamaa
Kuna dada mmoja kutoka mikoa ya Kaskazini alikuja hapa Dar akasema anataka kuanzisha mgahawa wa vyakula mbali mbali vya asili. Wazo zuri kabisa. Anahitaji ushauri. Unamshauri nini. Kwanza swali swali la kwanza kumuuliza lilikuwa UNAJUA KUPIKA?
Akasema ndiyo lakini sitaweza kupika peke yangu vyakula vyote hivyo wakati nafungua biashara.

Ushauri kwake ukawa: nafikiri usianze na kufungua mgahawa huko naona ni mbali sana. Kwa nini usianze kupika kidogo tu nyumbani kwako ambapo hutakuwa na gharama ya kodi ya huo
mgahawa mpya kwanza. Wala hutakuwa na mishahara ya kulipa. Wala hutakuwa na gharama za kununua viti vya kisasa nk. Anzia nyumbani ulipopanga. Pika ambia vijana mtaani waje kula. Wasipopenda hao chakula chako rekebisha. Utajuaje hawajapenda? Watakuwa hawarudi. Fanya hivyo.
Baada ya muda utapata wateja permanent kisha hao wateja watahitaji uwe na eneo kubwa zaidi lenye hadhi ya mgahawa na hapo sasa utakuwa ushaweza kusajili biashara yako kisheria na kulipa kodi ya pango la mgahawa maana hata wateja wa kudumu tayari utakuwa nao.
Dada akaona huyu hanitakii mema. Anataka na mimi nitumie muda mrefu kama yeye. Akatafuta washauri wengine. Wakampa yale mahesabu niliyosema juzi kuwa yanayokufanya uone biashara ni kama ujauzito tu. Miezi 9 ushatoka. Dada akawaamini. Akawekeza pesa.
Na nyingine akakopa nyingi kuongezea. Akaenda Sinza akapata Fremu kwa sh 500,000 kwa mwezi. Kodi ya mwaka milioni 6. Nunua majiko, vyombo, meza, viti, feni, vyakula vyenyewe mpaka anaanza kawekeza kama milioni 8. Na zaidi ya milioni 6 kakopeshwa na wajanja. Tena zingine kwa riba
Kaajiri na wadada wa kumsaidia kupika na kuhudumia wateja. Kaanza kazi baada siku chache chakula kinabaki, anaita mateja wanakuja kula na kuosha vyombo. Baada ya mwezi anafukuza wale wadada anasema kumbe nimejua kwa nini wapishi hoteli kubwa ni wanaume😀.
Haya.
Mwezi wa pili wateja hawaji. Anapata frustrations.

Mwezi wa tatu hali ni hiyo hiyo akaanza kusema kumbe amegundua pale kuna WACHAWI🤣🤣 eti usiku huwa wanacheza ngoma mle kwenye mgahawa usiku kucha lea hiyo wateja hawaji.
Miezi minne ukimuuliza UNAENDELEAJE jibu ni moja: WE ACHA TU😂😂. Wala miezi saba haikufika. Akauza masufuria na meza na viti akaanza kuwaza maisha kwa nini yamemwendea hivyo. Amesahau ushauri aliopewa mwanzo wa kuanza kupika nyumbani anakoishi.
Sasa anadaiwa kwa nguvu na waliojifanya wanamsaidia mikopo. Yuko frustrated. Na biashara ishakufa.

Nataka kusema nini?
Kumbuka uwezo wa kufanikiwa pakubwa unajengwa kwa kuanzia chini na kukua kidogo kidogo. Ndiyo maana kwa wastani inachukua miaka 10 hadi 30 kwa mtu kuwa
TAJIRI toka anapoanza biashara. Ijapokuwa kuna wanaofanikiwa kwa muda mfupi kama wenye UBER na TAXIFY. Lakini hizo tunaita EXCEPTIONS. Ili uwe kama wao buni kitu ambacho kitapata subscription nchi nzima au dunia nzima. Lakini kama unataka kupika chakula watu waje wale
mpaka uwe tajiri basi kubali kuanza kidogo tu na ujipe miaka 10 huko kama hujawahi.. but sana sana miaka 20.utakuwa umefanikiwa kiuchumi.

Biashara siyo ujauzito. Jipe muda. Anza kidogo. Biblia inasema USIUDHARAU MWANZO MDOGO.... DO NOT DESPISE A HUMBLE (SMALL) BEGINNINGS✍️
You can follow @DrBadiBoy.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: