ILI UFANIKIWE NI LAZIMA UKUBALI KUPOTEZA KWANZA.

Mzee Mengi alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Gazeti la Dar Leo vile vile. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika....
#UZI ENDELEA👇👇
Internet zikaingia nk.
Akaachana nayo. Afu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli.
Hivi unadhani Novida imeenda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je? Lakini CocaCola wamefilisika? Mengi amefilisika?...
No.

Okay, tufanye hivi, ule ukumbi wa Sinema pale Mwenge ITV ulikufa kifo cha fasta. Competition. Century Cinemax ilileta upinzani. Wenye mradi wakajifunza.
Kuna matajiri wengi tu walipoteza sana pesa. Mabasi ya Scandinavia yapo tena? Kuna maduka mengi tu Kariakoo yamefungwa...
kipindi hiki.
Ni kawaida kwenye ulimwengu wa biashara. Si uliona Landmark Hotel Ubungo ilibadilishwa ikawa hostel. Umeona jinsi ambavyo tayari amerejea na kuwa hoteli ya kisasa zaidi. Alishajifunza. Sijui unaelewa?
Dar Village hapo Rose Garden Kijitonyama haijajengwa hadi leo..
Mradi wa mabilioni uliingia mdudu miaka zaidi ya 9 sasa. Wewe unataka utakachoanza nacho kisife. Hela zako hutaki zipotee. Aisee you're not an entrepreneur. Kaa tu na hela zako. Bora ukazinywee Pepsi baridi tu au kula nyama choma kama unataka. Umekuwa mtu wa kutaka.....
mafanikio yasiyo na changamoto yoyote. Ndo maana unasubiri ukiambiwa aisee biashara ya Matikiti inalipa hatari huyo umo. Ukiambiwa mayai ya kware yanalipa huyo. Hutaki kutulia kwanza ujifunze.
Hakuna biashara isiyolipa.....
Unapoanza biashara kwa mara ya kwanza kabisa usiifanye ili kupata pesa - ifanye ili kujifunza tu vitu muhimu. Hela zije zisije usijali kwanza jifunze kwanza.
Ukishakuwa na PRACTICAL KNOWLEDGE (ufahamu uliopatikana kutokana na uzoefu) hapo unaweza.....
kuifanya hiyo biashara kama kitu cha kukutengenezea pesa au unaweza kwenda kufanya biashara nyingine ukiwa hauko "mbumbumbu" kama mwanzo.
Tatizo wengi tunataka biashara yako ya kwanza iwe kama ya Dangote keshokutwa. Aisee biashara ya kwanza inaweza kukupiga mpaka ukachakaa....
JIFUNZE KUPITIA STORY HII
Mmarekani mmoja aliingia kwenye restaurant huko London, ile kuingia tu aligundua kulikuwa na kijana mmjo wa ki-Africa mwenye umri wa kama miaka 28 akiwa amekaa kwenye kona

Yule mmarekani alikwenda mpaka kaunta akatoa kitita cha pesa na kumrushia.....
muhudumu kisha kwa sauti kubwa akasema "muhudumu! namnunulia chakura kila mmoja aliemo humu ndani isipokuwa yule mwafrica pale konani", Muhudumu alikusanya pesa na kuanza kugawa chakula cha bure kwa kila mtu aliyekuwemo ndani ya restaurant hiyo isipokuwa yule kijana wa kiafrica,.
Yule kijana hakukasilika badala yake alimtazama yule mmarekani kisha kwa sauti kubwa akasema "ASANTE SANA"
Yule mmarekani bila kujali kwa mara nyingine tena alivuta kitita cha pesa na kumtupia muhudumu kisha akapayuka "sasahivi nitamnunulia chupa ya wine na nyongeza ya...
chakula kila mtu aliyemo humu ndani isipokuwa yule mpuuzi aliyekaa pale kwenye kona.

Muhudumu kwa mara nyingine alikusanya ile pesa na kuanza kugawa chakula cha bure na wine kwa kila mtu aliyekuwemo mle ndani isipokuwa yule mwafrica,

Baada ya muhudumu kukamilisha kuwahudumia..
kwa chakula na vinywaji yule kijana wa kiafrica alimtazama mmarekani kisha akatabasam na kusema kwa mara nyingine "ASANTE SANA"

Hii ilimshangaza yule mmarekani na kuamua kumuuliza muhudumu "hivi yule kijana ana matatizo gani mbona nimenunua chakula na vinywaji kwa kila mtu...
aliyemo humu ndani isipokuwa yeye lakin hajachukia badala yake amekaa pale anatabasamu na kunishukuru eti "Asante sana!! Au ni chizi?

Muhudumu alitabasamu kisha akasema "hapana siyo chizi, bali yeye ndiye mmiliki wa hii restaurant hivyo anakushukuru kwa kuwa ww ni mteja mzuri".
Kwa uweza wa Mungu maadui zako bila wao wenyewe kujua wakaone kama wanakuangamiza na wakakufanyie mambo mengi ya kukunufaisha na kukuinua ktk maisha yako.
Kama unaamini sema AMEN..
Unasema umekata tamaa? Usifanye hivyo! Mwaka 1976, Oprah Winfrey alishushwa cheo kama mtangazaji nanga ya habari ktk runinga WJZ-TV Mjini Baltimore, Marekani. Aliambiwa “akiwa hewani hakuwa na mvuto na uchangamfu. alielezwa kuwa ana sauti mbaya isiyovutia lakini leo ndiye ni..
miongoni mwa wanawake wanaoheshimika na matajiri zaidi duniani”
Big no hupaswi kukata tamaa mwaka wako mmoja au mwezi au siku moja yako mbele imebeba historia kubwa sana ya maisha yako
Jisemee moyoni.. Mimi mkubwa mimi nitajiri mimi nina vitu...
Nikwambie kitu
:-
Unakata tamaa kwakua unatumia muda mwingi kuwaza namna ya kushindwa kuliko namna ya kuweza, kabla ya kuanza biashara basi unaanza kuwaza ni kwa namna gani TRA ni wasumbufu, namna ambavyo watu siku hizi hawanunui nguo, namna ambavyo huwezi kufanikiwa...
kwakua hiyo sehemu kuna mambo ya kishirikina. Kuwaza namna ya kushindwa kabla ya kuanza kunahalalisha kushindwa kwako, kuna leta neno “Nilijua” unashindwa kuilazimisha akili yako kufanya kitu kipya katika kutatua tatizo.

Nisawa na unatengeneza mlima ili ukishindwa kuupanda basi.
uusingizie mlima, lakini kiuhalisia kuna kua hakuna mlima mbele yako, ni vitu ambavyo umejiambia wewe mwenyewe na ndiyo ambavyo hukufanya kurudi nyuma. Nikweli biashara ni ngumu, lakini kwanini usiwaze namna ya kufanikiwa, usijipe moyo wewe mwenyewe na kuwekeza akili yako katika.
kuwaza namna ya kushindwa, kuna watu wengi wanahangaika na wamefanikiwa tena katika mazingira hayohayo unayoyaogopa.

Uki-google neno SUCCESSFUL PEOPLE (watu waliofanikiwa) utaletewa picha za watu waliovaa suti na wenye magari au Private Jets nk. Google haitakuletea picha zao..
wakati wakiwa wanapambana. Wakati wakitoka jasho na wakiwa kitaa kuyatafuta mafanikio... Hizo picha ni mpaka uzitafute mwenyewe. Na hizo ndo muhimu kuziona.
Laiti ungeona picha za Bill Gates wakati akiwa hajawa Bill Gates...
Michael Jordan kabla hajawa jina kubwa....
Jeff Bezos wakati anahangaika na Amazon bila kupata hata senti ya faida...
Mbwana Samata wakati anatoka Temeke hadi Taifa kwa mguu..
Diamond wakati anabembeleza kuimba kwenye show za watu nk

Naamini ungepata picha tofauti mno kuhusu neno MAFANIKIO...
Nimekuwekea PichaNadhani ni picha zinazosaidia kufikisha ujumbe niliokusudia kupitia Hu #UZI

Mafanikio siyo picha za suti na magari mapya.

Ni HUSTLE...
@_missharry
You can follow @DrBadiBoy.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: