#UZI 👇

Wasanii Wetu Pendwa Wa Bongo Flava Mnaotoa Hizi Nyimbo Za #Kampeni Za Kunadi Na Kusifu Sera/Maendeleo Na Juhudi Za Vyama MbaliMbali, Mnafanya Kazi Nzuri Sana Kama Wasanii. NAWAPONGEZA👏🏻Lakini Niwashauri Kitu Kimoja Kama Itawapendeza 🤔
#UZI 👇

Kwenye Nyimbo Hizo Mnazotoa EPUKENI TUNGO ZINAZO #DISS WAPINZANI WA VYAMA HIVYO MNAVYOVINADI!!

Msidhani Mnapowa-DISS Wapinzani Ni Mnawa-DISS #Viongozi Wa Vyama Hivyo Tu, HAPANA!! Ni Mnawa-Diss Hadi Wananchi Ambao Ni Wafuasi Na Wanachama Wa Vyama Hivyo Pinzani.
#UZI 👇

Kwa Mfano Chama Unachokinadi Kilipata Kura Milioni 8, Na Wapinzani Walipata Kura Milioni 6, Hapa Inamaana Unapotoa Kauli Mbaya Kwa Wapinzani Katika Wimbo Wako Ni Unaenda Kuwakwaza Watu Milioni 6!!
#UZI 👇

POINT YANGU HAPA NI KWAMBA UBAYA MKUBWA NI UNAKUTA WAFUASI HAO WA UPINZANI NI MASHABIKI ZAKO WA KAZI ZAKO ZINGINE ZA SIKU ZOTE ZA SANAA YAKO!! HALAFU LEO UNAONGELEA SIASA KITU AMBACHO NI MUSTAKABALI WA MAISHA YAO!! TENA KWA KUWA-DISS
#UZI 👇

Maneno Kama

-Wapinzani Wana Hanya Hanya!!
-Wapinzani Tumbo Joto
-Wapinzani Wapo Taabani
-Wapinzani Wamekaa
-Wapinzani Wanatetereka Sana

Na Mengineyo Ya Kebehi/Dharau/Kejeli Yanaweza Yakawapa Tafsiri Ambayo Siyo Nzuri KatiKa Mustakabali Wa Maisha Yao
#UZI 👇

Mwisho Wa Siku Ukatofautiana Nao Na Ukawapoteza Kama Mashabiki!!

Tukumbuke Kutengeneza Na Kuongeza Mashabiki Na Sio Kupunguza Mashabiki!!

Na Pia Tukumbuke Kuna Maisha Baada Ya Kampeni Na Uchaguzi!!
You can follow @Roma_Mkatoliki.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: