#Uzi

✍️ 2014 Nilikua Mitaa Ya Jamhuri- Posta Jijini Dar es salaam , Nikisubiri Kupokea Zawadi Yangu Ya Simu Aina Ya Htc Kutoka Kwa Kaka Yangu Aliekua Akiishi Zanzibar , Nilisimama Kama Dk 25 Kaka Akawa Amefika Ile Sehemu Aliyoniambia Anikute .. FUATILIA
Tukawa Tunasalimiana Pale Na Akinipa Maelekezo Kuhusu Ile Simu Alikua Kaleta Na zawadi Zingine Za Nguo Na Laptop vyote Vikiwa Ndani Ya Begi La Mgongoni .. Alinipatia Na Pesa Tsh 50000/= Kwajili ya Matumizi Yangu Madogo Madogo Na Nauli Ya Kunirudisha Nilipokua nikiishi Kimara....
Tulisimama Pale Kama Dakika 15 au 20 Hivi Baadae Kaka Akasema Anawahi Usafiri Mana Tiketi Alikua Tayari Kashakata Na Muda wa Kuondoka Ulikua Unakaribia Kufika Hivyo Tukaagana Pale Vizuri Tukaachana Akaondoka Na Mimi Nikaondoka Kwenda Kutafuta Gari Nipande Nirudi Home...
Nilivyokuwa Nikitembea , Nilitembea Kama Hatua kadhaa Hivi , Nikasikia Mtu Kanigusa Begani Kugeuka Nyuma Hivi Ni Mzee Mwenye Umri Kama Miaka 52 Alikua Kavaa Suti Nyeusi Yani Kavaa Vizuri na Begi Dogo Jeusi Mgongoni ...
Nikamsalimia Vizuri Akaniambia Samahani Mwanangu Mimi Naitwa Mzee Mashauri Mwenyeji Wa Mkoa wa Briadi Simiyu Hapa Mjini Nimefika Asubuhi Ya Leo , Nilipanda Fuso Ya Mizigo kutoka Bariadi Tulipofika Morogoro Kuna Gari Ndogo Aina Ya Verosa Tulikua Tumetangulizana Nayo...
Bahati Mbaya Ile Gari Iligongana na Gari Jingine Lililokua Mbele , Kweny Hio Gari Ndogo Walikuemo Wazungu Waliumia Sana Hawakuweza Kujitambua Tulishuka Pale Tulichukua Baadhi Ya vitu Walivyokua Navyo Lakini Askari Polisi walifika pale baadhi ya vitu walibeba wao ....
Mimi Nilibahatika Kuchukua Hizi Hapa Dhahabu Alikua Na Bahasha Huku Akiifungua , Haraka haraka Akaifunga akisema kuna wezi hapa wataiona..Sasa Mwanangu Nipeleke Hospital Ya Mhimbili Nimesikia Tangazo Wamelazwa Hapo Wazungu Na Atakayepeleka Hizi Dhahabu Kuna Zawadi Nono Wanatoa...
Kabla Hatujaondoka Pale na yule mzee Akaja Mbaba Mwigine Akauliza Vip... Vip.. Nikamuelezea Kama Mzee Alivyonelezea Yule Mbaba Akasema Haya Madiri Nayafanya sana hapa mjini Hizi ni pesa. Huku Akitoa simu yake mfukoni Akampigia Mtu Eeee! Boss vip ukowap Nina mzigo Mwingine Hapa...
Ukowapi Nipo Hapa Mbele Round About Hapa Busi tusubiri Hapo Tunakuja ... Wakasema Tuondoke Mimi Nikawaambia Siondoki wewe Msaidie Babu mimi Naenda Mbali Babu akaanza kulia Mjukuu wangu Naomba nisaidie Nitaibiwa kwa huruma zangu Nikaondoka na wale watu kwenda ...
Tulitembea kama dk 6 Tukakuta Gari ndogo Imepaki Anasema Pandeni Twende Offsini .. Nikapanda Mimi seat ya Mbele yule mzee akapanda nyuma na yule Mbaba Mwingine Akawa Anaendesha Gari....
Alivyoendesha Gari Kama umbali kdgo Akaniomba mimi nishuke tuzngumze Nkashuka na bahasha Akaniomba Alikua ana vidawa kweny chupa akatia kweny ile dhahabu ikawa inatoa povu akasema hapa tunapiga Mil30 Baadae akasema Rudi kweny Gari Tukapanda Gari tena...
Babu Akasema Mimi Saivi Siondoki Hapa Bila Advance Naombeni Mnipe chochote Yule Dreva Akatoa waleti yake akaiweka kwenye begi la Babu Na yule Mwenzie Akatoa Simu Na hela. Akaweka Ikabaki Zamu Yangu Mimi Nikagoma Lkn wenzie Wakasema lazima Niweke Mbona wao wameweka ...
Wakidai Hawamwamini Babu bhuc Namimi Nikatoa simu yangu kweny Begi na ile hela elf 50 na kisimu kdgo nikampa Babu akaweka kwenye Begi Nikabaki Na begi Langu Halina Kitu na bahasha ya dhahabu tu Dreva kaendesha Gari ...Alikua Anakatisha Bara Bara ovyo Hadi nikawa sitambui ....
Tena Maeneo yale tuliyopo Aliendesha Lile Gari Ikafika sehemu Akaniambia sasa hizi Hela zitakua Nyingi Sana Samahan Binti Unaitwa Nani ... Naitwa Harriet Haya Vzuri Naomba Chukua Hii Elf 2 000/= Kanunue Hapo Mfuko Mkubwa wa plastiki Kwenye Lile dula pale Mimi napaki Gari Hapo ..
Shuka Ununue Haraka Tukachukue Hela Uwahi Nyumbani .. Tunauzia Dhahabu Pale Kwenye Lile Geti Kubwa Mimi Hata Sikulitazama Lile Geti Nikashuka Nikaenda hadi Dukani ... Lkn nikajiuliza Kwann nisiwasubiri wakija Ninunue ndio tuingie .... subiri pale dk 5 ...20...30.. sioni mtu
Ikabidi Niende kwenye Lile Geti Nilivofika Mlinzi Akaniuliza Unashida Gani Nikamwambia Kuna Mtu Namsubiri Anaitwa Rashid ... Mlinzi Kasema Oooouh! Rashidi Anayependa Kuvaaa Pensi Nikamwambia Ndio Mana kweli Alikua amevaa pensi hafu kanyoa upara oke msubiri hap...
Nilisubiri kama saa 1 Nikashtuka Itakua Nimeibiwa Ikabidi Niikague Dhahabu Kuangalia Dhahabu vzuri Hivi ni Mchanga Mtupu.... Mwili Ukaishiwa Nguvu .. Mlinzi nikamweleza AKASEMA UMEIBIWA MDOGO WANGU😔😔
Mlinzi Nikamuuliza Mbona Ulisema Unamjua Akasema ninayemuongelea Mimi Huyo Ni daktari Wa Hapa Aghakan Hospital Kumbe pale Ilikua Hospital Na sio sehemu ya kuuzia Dhahabu😞😞 ILE ELF MBILI IKAWA NDIO NAULI YANGU YAKURUDIA KIMARA
Plz Guys Utapeli Umekua Mwingi sana ... wapo wanao tumia madawa ili akuibe kitu ambacho kinaweza kuhatarisha maisha yako TUWENI MAKINI🙁🙁...
@threadreaderapp please unroll🙏
Reweety Post Hii Iwafikie Wengine Wasije Kuibiwa Kama Mimi.....🙏🙏😒😔😔😔
You can follow @DrBadiBoy.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: