#TwitReport
Kama ni mpenzi wa muziki wa malijendi wa kama John Lenon, whitney, SamCock, Tina Tana, Diana Rose, James/Bobby Brown na Sting
Ni nadra mno kutomfahamu mwanamama Aretha Franklin (25/03/1942 – 16/082018)
(Nikitaja jina lake naomba wote tupige goti na tusema shikamu)
Je? umewahi kutambua haya kutoka kwa mwanamama huyu Aretha Franklin.
1. Mtoto wa mchungaji aliyeanza kuimba kwaya kanisani na kufungua dirisha la muziki mzuri ulimwenguni- aliwashika watu kisawasawa hadi serikali mjini Michigan ilipitisha kuwa sauti yake chanzo cha asili
(natural resource)
kama yalivyo madini na mlima kilimanjaro nchini Tz.
2. Alikuwa mwoga wa kusafiri kwa ndege baada ya ndege aliyopanda mwaka 1980 kutoka Atlanta kuelekea nyumbani kwao Detroit kupata shida hewani kwasababu ya hali ya hewa.
Aliwahi kujiunga na mafunzo ya kutoa uoga lakini alishinwa kuhudhuria mafunzo kwa wiki mbili na kumfanya ashindwe kuhitimu- alifariki akiwa bado mwoga,
Alikiri kukosa mambo muhimu kutoka katika miji kadhaa kwasababu ya hofu yake ya kukwea pipa...alikuwa radhi kupanda gari.
3. Unamkumbuka waziri wa mambo ya nje wakati wa utawala wa Rais Bush? Bi Condoleezza Rice. Alikuwa rafiki mkubwa wa Aretha. Mwaka 2010 Wakiwa pamoja ofisini kwa waziri huyo, alimshawishi kuimba naye jukwaani kuhamasisha michango ya elimu huko Philadephia...
Bi Condoleezza alikubali na baada ya mwezi mmoja walikinukisha vibaya mno, kwa vibao vya "I Say A Little Prayer" na "America (My Country 'Tis Of Thee)."
4. Aretha aliwahi kupambana kumtolea dhamana Angela Davis-mnazi wa kikomunist na mwanadada machachari wa kikundi cha Black Panther ambaye alikamatwa wiki ya 8 baada ya kutangazwa kwenye list ya watu 10 wanaotafutwa na FBI mwaka 1970.
Aretha alipambana kumtoa lakini ilishindikana, kesi ilikuwa ngumu - lakini hadi leo hii Angela Davis ananukuliwa akimsifu Aretha kwa kuwa na moyo wa kuwasaidia wapambanaji. Kumbuka Aretha alikuwa mnazi wa kikomunist pia.
5. Aliwahi itwa mama wa imani wa mwanamuziki Whitney Houston (Godmother) japo si kweli, mtangazaji ambaye alikuwa binamu wa Whitney alizidisha chumvi.
Ni Mwaka 2012 ambapo alishindwa kuhudhuria mazishi ya kipenzi chake, mwanadada Whitney kwasababu ya maumivu makali ya mguu.
Siku kadhaa baada ya mazishi, mama mzazi wa Whitney alikanusha kuwa Aretha hakuwa Godmother wa mwanae-bali walipendana kama ndugu, japo hadi leo hii kuna wanaoamini kuwa ni kweli-Licha ya Aretha mwenyewe kukanusha pia mwaka 2017.
Mama wa imani au baba wa imani (Godmother/Godfather) kwa wakristo ni yule anayemsimamia mtoto toka ubatizo- na kazi yake kubwa ni kumchunga mtoto aishi kwenye njia takatifu ya ukristo maishani mwake.
Labda ndiomaana Aretha alikanusha, kwasababu wote tunafahamu Whitney alifariki kwasababu gani (Sina hakika kama ndio sababu kuu ya kukanusha)
You can follow @humphreymoris.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: