THREAD: Jinsi ya kuboresha mahusiano yako na professional stakeholders wanaosupport jitihada zako iwe wafadhili, wabia, mawakala au wadau wa biashara
Awali ya yote kama wewe ni Mkurugenzi, Executive Director, Managing Director, CEO au Mwenyekiti Mtendaji uelewe kwamba hili jukumu linakuhusu moja kwa moja. Asilimia ya kutosha ya muda wako utatumia kuboresha au ku’maintain’ current partners
1. Mindset. Ni muhimu kumthamini mdau uliye naye kwa nguvu ile ile unayotumia kumpata mpya. Kwakuwa tu umeshampata haimaaniishi usimzingatie tena au usipalilie uhusiano wenu. Ili uweke hizo jitihada ni lazima ubadili mtazamo ili umthamini kwa kumaanisha. Water your garden
2. Mawasiliano. Kumthamini kimoyo moyo haitoshi. Mpe taarifa kinachoendelea katika kazi zako iwe katika mfumo wa reports, newsletters, update emails, social media tags au hata kuschedule calls. Kwa upande wako, akikutumia taarifa zake ni muhimu kutambua kwa kutoa feedback
3. Ushiriki. Hii ni tofauti na mawasiliano. Unaweza kualikwa au usialikwe. Mfano umeona your funder/investor ana host a webinar, ni vizuri ukashiriki, tafuta fursa ya kuchangia mada inayoongelewa ukitumia kazi yako na yake kama mfano. Usishiriki for the sake of it, please engage
4. Mazuri na Mabaya. Share wins and losses. Tunatumia nguvu kubwa sana kuficha madhaifu yetu au pale tulipokosea. Ukiwa unafanya kazi lazima kuna mahali utakwama tu. Kitakachoboresha uhusiano wenu sio kufunika kombe, it’s okay to fail, utashangaa ukiwa mkweli watakavyokusaidia
5. Give and take. Kuna stakeholders wataokupa pesa inawezekana ni benki, donor au investor. Kuna stakeholders utakaofanya nao kazi lakini sio pesa. Hawa wa pili hawapewi thamani kama wa kwanza, it’s wrong. Huyu anapunguza workload, anakupa credibility, network na insights. Value!
6. Muendelezo wa Give and Take. Huyo wa pili likely anakuhitaji kama unavyomuhitaji. Kwahiyo lazima umsaidie katika kazi zake. Hii ni next level baada ya mawasiliano na ushiriki. Unamsaidia katika kazi zake, unampa moyo, mawazo na ‘connection’...
7. Mwisho, lazima uwe na stakeholder map. Kila stakeholder utambue thamani yake kwako na thamani yako kwake. Hata mkopaji ana thamani kwa anayekopesha ingawa yeye ndio ana shida. Hakuna uhusiano usio na exchange of value/thamani. Usiende blindly. Tambua ni nini. Zingatia thamani
You can follow @FarajaNyalandu.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: