Happy International workers day!

Siku ya leo naomba kushare na nyinyi kumbukumbu yangu.

Baba yangu alikua ni Mjasiri amali (Miti ya Ujenzi, Kokoto na matofali) na niwaambie nikiwa na miaka 7 nilikua naenda kumpa baba leave aende nyumbani akanywe chai na muda wa chakula cha
Cha Mchana na kuanzia hapo nilijizoesha kwenda mara kwa mara.
Nilipofika miaka 12 nikawa sipendi kabisa kufanya kazi za nyumbani nikawa naamka mapema kuliko yyt naenda kazini kwa baba nafagia huku nasoma dua ili ata akija baba akute nishauza, niligombwa kwakua nilikua mdg
Na sehem ilikua asubuh haijachangamka ila sikuchoka, akili zilipochanganya nikawa nikiambiwa uza mti mmoja 1000-700 nilikua najitahid nisishuke chini ya 850 halafu 50 najiwekea mimi na niliendea na utaratibu huo na hapo ndipo nilipojifunza kupenda pesa😂
Kiasi ambacho pakipungua kitu utamskia mama kaangalieni bank (mkobani kwangu) na kweli hawakua wakikosa na mpk leo hakuna anaeamini nyumbani nikisema sina pesa kutokana na mazoea hayo đŸ„Č

Kuna siku baba aliniacha dukani hio siku nikauza sana kama laki 7 ilikua 2001 na duka
Linaonyesha wazi ile gap, nipo na pesa nimeshika sehem nacheza na watoto wenzangu akapita huyo Mzee ambae alikua anapenda kuniita MCHUMBA kitu ambacho nilikua nachukia sana basi nikakimbia baadae alipoondoka nikarudi kucheza huku nasubiri kuiona furaha ya baba yng
Ghafla namuona baba yng uyooo anakuja najiangalia pesa sina tafuta tafuta na wewe pesa siioni nilijiskia unyonge na vibaya sana baba akaniita mama nikaenda namwambia baba nimeuza sana halafu nikamueleza baba alinijibu “HONGERA ILA USIHUZUNIKE HIO PESA HAIKUA RIZKI YETU” tukashkur
Nilipofika 16 nikawa namwambia baba yy akafanye pirika zake kama mimi naenda skuli mchana na kama naenda asubuh jioni nakaa mimi basi kwenye upande wa matofali kulikua na mashine zile za mkono nikawa naenda nawaambia wanifunze kuchanganya mchanga pmj na kupiga matofali mpk nkajua
Ikawa kila siku naenda kupiga tofali 5, baba anauliza wewe mwanamke kazi hizi za nn wewe pumzika nikamjibu baba wakija kudai kuongezwa mshahara utajuaje bila kujua ugumu/urahic wa kazi? Wacha niendelee kwa kweli baba alinipenda sana mpk watu walikua wananiita jicho la Boss flan
Lengo sio kujisifia ila ni kuonyesha ni jinsi gani tunatakiwa kuwazoesha watoto wetu tunayoyafanya ili wawe wasimamizi wazuri, kweli nlikua msimamizi mzuri na nisiseme uwongo hio ndio kupenda kwangu pesa, kazi na biashara ilipoanzia na kupenda kujifunza

@Chahali @MarekaMalili
You can follow @20qnana.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: