#TwitReport
Watu walikuwa smart na wababe, mtu anayeogopwa na Rais na vyombo vyote vya dola huyo sio wa mchezomchezo. Umewahi kuwaza ni namna gani vitengo vya usalama vinamtambua mtu kwa kutumia alama za vidole?, basi haya yote yasingekuwepo bila ya mtu aliyeitwa Edgar Hoover
👇
Imeandikwa na kuhaririwa na HumphreyMoris #TwitReporter

Edgar Hoover
Me napenda kumuita Mzee wa michongo, mkuu idara ya FBI toka mwaka 1924 hadi alipofariki mwaka 1972 wakati wa vuguvugu wa kesi ya mjombaangu Richard Nixon (Nimeandika mengi kuhusu huyu bwana
hadi nimechoka-mnipe tuzo😀)
Hoover Alihudumu bila kustaafu kwa muda mrefu na hakuna hata kiongoz mmoja aliwahi kumchokonoa. Ukijaribu kumgusa jiandae kupata aibu
Aliamini sana kwenye mafaili (kutambua udhaifu wako kwa mambo madogo madogo ambayo atakulazimisha ufwate anachokisema
kwakuhofia atakuanika hadharani)
Aliwajua mahawara wa marais na viongizi wote (John Kennedy alipata shida sana)
Ubaya ni alitumia hata vitisho ili ufuate anachosema😊 alifanya haya yote kwa maslahi mapana ya FBI ambayo aliijenga upya na kuifanya iwe taasisi imara inayoogopwa.
Wakati wake FBI ndo ulikuwa wakati mbaya kwa serikali ya Marekani
1. Communists
2. Majambazi wakubwa na maarufu kama Pretty Boy Floyd, Baby face Nelson, John Delinger, Bonny and Clyde, Machine Gun Kelly, Alcapron AKA SCARFACE

HIZO NAMBA NIMEZITAJA HAPO NI NAMBA CHAFU VIBAYA SANA
fikiria mtu kama Edgar atapambana nao vipi kama sio usmart na ukatili wa hali ya juu?
Hoover inasemekana alizaliwa mwaka 1895 huko mjini Washington.
Alisoma sheria level ya degree na masters huko George Washington University
na kuingia kwenye kitengo cha sheria kama mtunza ma file mwaka 1917. Umakini wake kwenye mafile na kuwajua watu
ulimsogeza na kuwa msaidizi wa karibu sana kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu chini ya mzee wake Mitchell Palmer. @mlevi1276
Tambua, huu ndo ulikuwa msimu mgumu kwasababu Urusi walikuwa wanajitahidi kupenyeza falsafa yao ya communism, na kwa Marekani huyu ndo alikuwa adui number moja. Sera hii ilipigwa vita mno.
Baadae Hoover alikabidhiwa kitengo cha Bureau of Investigation (kabla haijawa FBI) kama kiongozi kivuli lakini kwa uchapakazi wake baada ya miezi 7 alipewa kitengo kamili.
Kabla hajawa director, aliitwa ofisini na kuambiwa rasmi kuwa anapewa nafasi hiyo.
https://twitter.com/humphreymoris/status/1386657119919816709?s=20
Alisema kabla sijakubali nina masharti yangu ma 3
kwanza

http://1.Ni  lazima kupandisha vyeo pale mfanyakazi anapofanya jambo zuri.

2.Kuitenga FBI na masuala ya kisiasa.

3.FBI kureport kwa mwanasheria mkuu pekeake.
WALIKUBALI.
Kichaa akaanza kazi, woooooy wooooooy

Kesi iliyompatia umaarufu hapo mwanzo ni pamoja na ile ya kutekwa kwa mtoto wa rubani Charls Lindbergh
Mtu wa kwanza kurusha ndege pekeake katika bahari ya Atlantic bila kulala kwa masaa 55. Siku moja nitawapa kisa chake.
Hoover alidharauliwa kwenye hii kesi lakini baada ya kujulikana kuwa mtoto wa Lindbergh amefariki-alianza kuaminiwa kwasababu alishiriki kikamilifu kumkamata mtekaji na muuwaji wa mtoto huyo.
Kabla ya kukamatwa, Hoover alichunguza kwa undani siku moja na kudhihirisha mashaka ya kichanga hiko kuwa hai, kwasababu alipata ushahidi unaoonyesha kuwa mtoto huyo aliangushwa kwa bahati mbaya na kufariki siku ile ile ya tukio.
Kesi hii ndo ilikuwa njia kwa Hoover kuanzisha idara ndani ya FBI ambayo walichunguza masuala ya alama za vidole. Wengi walikamatwa wakati huu na kupelekwa jela kukutana na wahuni wenzao (si unaukumbuka msemo wa DC wa Iringa😁
Rais wa Marekani miaka ya 1930 bwana Franklin Roosevelt ndo alizidi kumpa kichwa Hoover,
Hoover aliitumia nafasi hii ya wahalifu kuipatia sifa FBI, na kupewa madaraka ya kuchunguza watu wote walioonekana kuwa tishio kwa serikali ya Marekani.
Binafsi alifuatilia kwa umakini wanaharakati wa Khu Klux Klan.
Black Panthers, Weather underground na wengine wote ambao waliitikisa serikali ya marekani wakati huo.
Hoover hakuwahi kurudi nyuma kwenye mikakati na utendaji hadi pale alipofariki dunia mwaka 1972 kwa mshtuko wa moyo.

Natamani kukujuza haya mambo 10 machache kuhusu Hoover
Naomba tushuke na Thread
1. Kuna wakati alifanya mambo kwa faida yake mwenyewe, kama hakupendi au hawapendi watu wa aina fulani, atafanya juu chini akudondoshe. Kuna wakati alitumia hadi njia zisizofaa kisheria kama kuweka vinasa sauti na kufake kesi.
Hata Martin Luther king alipata tabu sana na Hoover, inasemekana aliwahi tengenezewa figisu na kumpiga picture akiwa na hawara, picture ambazo zilipelekwa moja kwa moja kwa mke wa Martin Luther King.
Sema Luther alikuwa Imara sana,
kuna barua toka FBI iliyomtaka Luther King kujiua. Hakujiua mpaka alipouawa kwa risasi miaka ya 1960.
Nimewahi kuandika hapa kuhusu hiyo barua https://twitter.com/humphreymoris/status/1364629802406264835?s=20
2. Skendo,
Jamas hakuoa wala hakuwa na mahusiano.
Mavazi yake yaliwapa watu wasiwasi na kudhani ndo wale waleee, eeeh hao hao sio lazma niandike hapa.
Alikuwa na ukaribu mkubwa na mfanyakazi wake wa kiume Clyde Tolson, muda wote walikuwa pamoja.
Hata mavazi, walikuwa wanavaa sare maranyingi. Baada ya Hoover kufariki, vitu vingi alirithi Tolson ambaye naye alikuwa mgonjwa kipindi hiko.
Pia bwana Hoover aliwahi kuwa na scandal ya kutembea na baadhi ya wanawake maarufu, wengine walikiri kuwa na mahusiano naye alipofariki.
Licha ya kutiliwa shaka na mahusiano yake, Hoover aliwahi kumshawishi Rais Dwight Eisenhower kufukuza kazi watumishi wote wenye tuhuma ya naniliu eeh hivyo hivyo, jinsia moja.
3. Hakuamini katika kuajiri mwanamke ndani ya FBI
Na kama akikupatia ajira, alikuwa hawaruhusu kuvaa suruali na aliwapiga marufuku kuvuta sigara, alitoa ruhusa kwa wanaume tu.
4. Hoover alifanya kazi FBI chini ya Marais 6 lakini alipatana na marais wawili tu
Roosevelt na Johnson.
Wengine wanne walijaribu kumuangusha lakini walishindwa.
Wanne hao ni Eisenhiwer, John Kennedy, Harry Truman na Richard Nixon
Richard Nixon, ambaye ni wa mwisho kwa Hoover. Kabla Hoover hajafariki, alimwomba sekretari wake Mwanamama Hellen Gandy kuchoma ma file yote ya siri endapo kuna baya litamkuta, kwasababu alikuwa Hazielewi akili za Richard Nixon.
Kumbuka Hoover maishani mwake aliwahi kuwaamini wanawake watatu tu
1. Mama Yake
2. Sekretari wake (Hellen)
3. Mtoto wa kike wa mtaani ambaye alikuwa rafiki yake mkubwa, alikuwa anamchukua ofisini mara kadhaa na hata kwenye mafunzo ya kuendesha farasi.
Hao pekee.
Hivyo Nixon hakupata bahati ya kuyatia mikononi mafile ya Hoover. Miaka kadhaa baadae, msimamizi wa Hoover aliyeitwa Mark Felt, alifanikiwa kumng'oa madarakani Rais Richard Nixon kwa sakata la watergate scandal.
Mzimu wa Hoover ulimtafuna Nixon
5.Mwaka 1950 kama ilivyo kwa Sir Alex Ferguson na ma Sir wote, Mfalme George VI alimvika cheo cha Sir (Knight). Lakini Hoover alikataa kuitwa Sir Maishani mwake.
6. Wengi walimwita mwoga kwa kukataa kwenda vitani, lakini ukweli ni kwamba Hoover alichagua kuitunza familia yake maisha yake yote.
Baba wa Hoover alipata ugonjwa wa akili na kuachishwa kazi bila pensheni, hivyo Hoover aliamua kuilea familia yake
huku akisifiwa kwa kumpenda mama yake ambaye aliishi nae pamoja, kumpeleka sehemu za starehe kama kutazama movie hadi pale Mama Alipofariki.
7.Alikuwa mbabe/mroho wa madaraka.
Kwa sasa Mkurugenzi wa FBI anafanya kazi kwa miaka 10 tu. Hoover aliitumikia FBI kwa miaka 48 toka 1924 hadi alipofariki. Hakuna mkuu wa FBI aliyefanya kazi muda mrefu kama yeye.
8. Alikuwa na taarifa za wamarekani 430,000. Yeyote aliyemtilia shaka alimfuatilia, kwa mfano hapa twitter usishangae ukaambiwa file lako lipo sehemu fulani: wakulu wanakuchora tu😀.
Baadhi ya watu maarufu aliowafuatilia zaidi ni kama Marlyn Monroe..mwigizaji na mwanamitindo aliyesadikiwa kuwa na mahusiano na Rais John Kennedy.
Rais Eleanor Roosevelt
Mwanasansi Albert Einstein😀
Na wengine weeeengi. https://twitter.com/humphreymoris/status/1280501065046253571?s=20
9.Hoover alipenda sana kucheza kamari ya mbio za farasi. (Alikua mtu wa mikeka sana)
10. Aliitumia Tv kupitisha Agenda ya kusifia kazi za FBI (Spinning Dr). Tv ilirusha series ya THE FBI mwaka 1960 na 1970, huku ikionyesha case zenye uhalisia wa kweli ambazo zilisimamiwa na FBI huku Edgar Hoover akiwa chief editor wa Script-
na haikuruhusiwa kurushwa kitu chochote bila ruhusa yake ili kuijengea FBI mwonekano mzuri.

This is Humphrey Moris #TwitReporter na leo nimekupa baadhi yanayomuhusu Edgar Hoover.
KWAHERI
You can follow @humphreymoris.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: