Mamilioni kujenga nyumba za wakuu wa wilaya na mikoa.

Milioni 838 kumalizia nyumba ya mkuu wa mkoa Kagera, Milioni 170 kujenga uzio na nyumba ya mlinzi kwa mkuu wa wilaya Temeke. Milioni 555 kukarabati nyumba ya mkuu wa mkoa Ruvuma..
Wakati makusanyo ya mapato katika wilaya ya Kakonko kwa mwaka 2020/21 yalikua ni Milioni 539, ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya umetengewa milioni 700. Fedha hizi ni mara tatu ya fedha zinazogharamia elimu kwa shule za msingi Kakonko
Fedha zilizotengwa kumalizia nyumba ya mkuu wa mkoa Kagera Tshs.838,349,169.44, ni mara mbili ya fedha zilizotengwa kununua vifaa tiba katika mkoa wa Kagera, milioni 397 zimetengwa kwaajili ya vifaa tiba.
Ukarabati wa nyumba Katibu Tawala Kisarawe umetengewa milioni 130.

Fedha zinakaribia kulingana na bajeti ya sekta ya afya Kisarawe Kwa mwaka 2020/2021, milioni 150.
Ukarabati wa nyumba ya Katibu Tawala Mkuranga milioni 140 na

Ukarabati wa nyumba ya Katibu Tawala Bagamoyo milioni 120.

Fedha hizi ni zinakaribia bajeti ya sekta ya afya katika wilaya hiyo kwa mwaka 2020/2021 ambapo milioni 300 zilipelekwa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati.
Bajeti iliyotengwa kukarabati nyumba ya mkuu wa mkoa Ruvuma ni milioni 555, fedha ni zaidi ya fedha zilizotengwa kujenga vituo 18 vya afya Ruvuma, ambapo ni milioni 500 tu iliyotengwa.
Ujenzi wa nyumba za Katibu Tawala Wilaya za Kondoa na Mpwapwa umetengewa jumla ya milioni 600.

Mwaka jana Wilaya ya Mpwapwa iliweza kujenga nyumba mbili za walimu wa shule ya msingi Lukole zenye jumla ya vyumba sita kwa Milioni 35.5 tu.
Kujenga uzio na kufanya 'landscaping'(kutengeneza garden n.k) nyumba na ofisi ya mkuu wa wilaya Wanging'ombe ya mkoani Njombe imetengewa milioni 360.

Fedha hizi zinakaribia jumla ya fedha zote zilizopelewa kwa ajili ya kugharamia elimu ya msingi katika wilaya hiyo, milioni 384.
You can follow @TheChanzo.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: