MAMBO NANE (8) YA RAIS SAMIA KUZUNGUMZA NA BUNGE

1.SHERIA KANDAMIZI NA ZA HOVYO
👉 Ndani ya miaka 5 ya utawala wa Meko ni kipindi ambacho Tanzania imeshuhudia utungwaji wa sheria nyingi kandamizi na za hovyo zenye kulenga kukandamiza wananchi na uhuru wao wa kikatiba.
👉Moja ya matukio ya ajabu ni pale sheria nane zilipopelekwa bungeni na kujadiliwa kwa masaa matatu kisha kupitishwa, wabunge wachache sana walipaya fursa ya kuchangia maoni yao
-Ndani ya utawala wa Meko tumeshuhudia sheria zinatungwa ili hukalalisha uporaji wa mali za watu na
wafanyabiashara kwa kisingizio cha uhujumu uchumi, kuna watu wamepoteza Maisha kutokana na msongo wa mawazi na wengine wamewekwa ndani
•Natarajia Samia kwenye hotuba yake atazungumzia sheria mbovu kwa ujumla wake maana bungeni ni mahali sahihi zaidi , ndiko sheria hizi mbovu
hutungwa kwa hati za dharura na natagemea ataanza mchakato wa kibunge wa kufuta sheira zote kandamizi na za hovyo zilizoumiwa watu kwa miaka 6 ya utawala wa Meko
•Samia atatumia nafasi hii kuomba MSAMAHA kwa taifa na wahanga wote walioteswa na kuumizwa ambapo yeye likuwa VP
•Samia atatumia nafasi hii kuwahakikishia wafanya biashara na wawekezaji walioumizwa na Meko kuwa sasa mambo yako tofauti na awape confidence ya kufanya biashara Tanzania bila kusumbuliwa na kuporwa mali zao na serikali
•Samia atatumia nafasi hii kuomba ushirikiano kwa
wananchi na asasi za kiraia kushiriki bila uoga katika utawala wa nchi yao kupitia maoni yao na kwamba kila mtu ataheshimika katika mitazamo yake
•Sheria za huduma za Habari, sheria ya mitandao, takwimu na sheria ya NGOs na sheria ya makampuni zirekebishwe kwa haraka zaidi
2.KUBORESHA MAHUSIANO YA KISIASA BAINA YA VYAMA VYA SIASA
👉 Meko aliwachukia wapinzani na kuwana wanasiasa wa upinzani kuwa maaduni wakubwa na wasiofaa kuishi ndani ya nchi hii.Ndiyo maana ndani ya miaka yake 5 na miezi 5 ya uongozi wake ameuwa sana wanasiasa na kuwafunga na
kuwafilisi kwa kuwa ni wapinzani
👉Meko alijenga hisia ndani ya wana CCM na wafuasi wake kuwa CCM tu ndiyo wenye haki ya kufanya siasa ndani ya Tanzania na wapinzani ni wahalifu na wahaini
👉 Ndani ya utawala wa Meko aliweza kuzuia CSOs, NGOs kufanya kazi zake kwa uhuru akafika
hatua mpaka kutunga sheria ya kudhibiti kila kinachofanywa na CSOs na waliobisha waliishia kufungiwa na kufutwa kabisa.Waliobaki ni wale waliokubali kuwa mouthpiece ya Meko na wanaofuata masharti yake hata kama hayako sawa
•Samia kwenye hotuba yake anapaswa kulizungumzia hili
na kuonyesha utayari wa serikaliyake kuondoa mazuio na sheria za ajabu zinazokwamisha CSOs kufanya kazi kwa kuwa zina nfasi muhinu sana katika maisha na ustawi wa taifa , faida ya kazi za CSOs ni kubwa sana kwenye maeneo ya utawala bora na haki za binadamu,
CSOs zinakazi kubwa ya kufanya utetezi wa haki za binadamu na utawala bora, inawezekana hiyo kufanyika wakati sheria imewapa nguvu watumishi wa wizara ya afya kupitia msajili wa NGOs kudhibiti NGOs?
•Samia akemee wazi wazi makundi hatari ya propaganda yaliyoundwa na Meko naf
wafuasi wake ili kuchochea mtazamo wa kuwa uzalendo ni kushabikia CCM au Rais aliyeko madarakani na kuacha kutumia resources za nchi kufadhili na kulipa makundi haya kwa kuwa ni hatari

3.TUNATAKA MAENDELEO YA WATU NA SIYO VITU
👉Ndani ya utawala wa Meko tumeshuhudia serikali
ikijikita kwenye miradi mikubwa mikubwa isiyo na tija kwenye maisha ya watanzania huku ikitumia mabilioni ya fedha. Unanunia madege watoto hawana madarasa!
👉Tunataka maendeleo ya wat una siyo vitu .. WAtu hawana fedha mifukoni kwa kuwa hali ni ngumu na mzunguko wa fedha umekuwa
mbaya san ana haupo na maisha yamekuwa magumu sana
👉Watu wanahofu ya kufanya biashara kwa kuwa wanahofia TRA watakuja kuwakamata na kuwafilisi kwa kuwa TRA wao kazi yao ni kukamua watu kodi tu na hili limeharibu sana bishara za wat una maisha yao
•Samia anatakiwa kuzungumza
jinsi atakavyoirudisha nchi kwenye mstari sahihi ili kuanza kuvutia wawekezaji na watu wafanye biashara kama zamani na waone maendeleo kwenye maisha yao siyo kwenye midege na madaraja
•Samia anatakiwa kubadili utendaji kazi wa TRA kama siyo kui disband kabisa maana utendaji
kazi wa TRA umekuwa siyo friendly kabisa na kuogopesha watu kufanya biashara kwa kuogopa TRA
•TRA ni lazima ifanyiwe maboresho makubwa, watanzania hasa bara wanashindwa kuingiza vitu nchini kutokana na kodi kubwa, kodi zingekuwa za kawaida, watu wengi zaidi wangeingiza mizigo
4. SERIKALI IFANYIE KAZI WATU NA SIYO WATU WAIFANYIE KAZI SERIKALI
👉Serikali ikubali kuwajibishwa na wanainchi waiajibishe serikali na viongozi wa umma kwa kuwa wako madarakani kwa ridhaa ya wananchi na siyo kwa ridhaa yao.
👉Wananchi wahusishwe kwenye maamuzi na hili liondoe
dhana ya kuwa viongozi ni miungu watu na kiburi kilichopelekea ma DCs na RCs wanaweka ndani watu hovyo,wanashiriki kuiba kura,wanachapa viboko wananchi.

•Samia azungumzia ambavyo serikali inawajibika kwa wananchi na siyo wananchi wanawajibika kwa serikali na pia wananchi
washirikishwe kwenye maamuzi yanayohusu maisha yao
•Viongozi wanaokiuka maadili ya uongozi na kunyanyasa wananchi wawajibishwe bila kuchelewa
•Taasisi za umma zinazogusa watu kila siku zifanyiwe maboresho makubwa, zifanyekazi kwa uwazi, leo tunaambiwa polisi inakamata watu
na kuwaweka ndani bila kuwaingiza kwenye vitabu vya kumbukumbu, hii inawezekana vipi?
•Biashara za watu lindwe, hukumu sahihi na inayokubalika itokane na mahakama tu, TRA na mamlaka nyingine zisiwe na nguvu ya kufikia kuuwa biashara za watu
•Tume ya haki za binadamu na tume
ya maadili ya viongozi wa umma ziimarishwe na kupewa uhuru zaidi wa kufanyakazi kwa niaba ya wananchi

5. CHAGUZI HURU NA MARUFUKU KWA DOLA KUINGILIA CHAGUZI ZA KIRAIA
👉Ndani ya miaka 5 na miezi 5 ya utawala wa Meko tumeona jinsi alivyotumia dola kuharibu chaguzi za hii nchi
na ambayo Meko aliweza shinda uchaguzi ni kwa kutumia dola au kununua wapinzani ambao nao bado alitumia dola kuwapa nafasi za kuchaguliwa, hakuna uchaguzi uliofanyika
👉Vyombo vya dola vimeacha majukumuyake ya msingi na kujiingiza kwenye mambo ya chaguzi za kiraia mpaka imefika
mahala TISS wanachapisha karatasi za kura na kuzisambaza nchi nzima.
👉Tumeona jinsi Jaffo na Meko walivyofanya uhuni kwenye uchaguzi wa LG 2019 bila aibu kabisa, hii tabia ni ya kihuni na dhuruma kwa wananchi
👉Tumeona jinsi ambavyo wabunge 19 wanaojiita wa Chadema walivyoingi
zwa bungeni kinyume na utaratibu kwa msaada wa dola..
•Samia anatakiwa akemee na kueleza wazi jinsi wabunge hawa 19 wanavyolinajisi bunge ambalo tayari liko hapo kwa wizi wa kura, wabunge 19 wamelipwa mishahara kinyume na maadili, fedha irudishwe
•Samia aweke wazi kutojihu
sisha tena kwa vyombo vya dola kwenye chaguzi za kiraia
•Samia aongee wazi jinsi ambavyo amejipanga kurudisha imani kwa wananchi na jumuiya ya kimataifa juu ya mwenendo wa chaguzi zijazo nchini
•Samia aeleze wazi msimamo wake juu ya mchakato wa katiba mpya ya Warioba
6.HATMA YA WALIOPOTEA ,KUUWAWA, KUWEKWA MAJELA NA KUTESWA
👉 Ndani ya utawala wa Meko tumeshuhudia watu wameuwawa,wamepotea ,wametekwa,wameteshwa,wamepigwa risasi. Jambo hili limeichafua sana nchi mpaka imefika mahali akina Bashite wamewekewa vikwazo kusafiri nje ya Tanzania
Samia azungumzia jinsi ambavyo serikali yake na utawala wake utakavyo endesha uchunguzi huru juu ya wahusika wa haya mauaji,utekaji na uteswaji
•Na aweke wazi ni hatua gani anafikiria kuzichukua kwa wale wote watakaokutwa na hatia za makosa haya dhidi ya binadamu wenzao
Mahabusu wote wanaotumikia kifungo kwa muda mrefu bila upelelezi kukamilika waachiwe huru mara moja
•Watu wote waliowekwa huru kupitia utaratibu wa kukubali kosa na kulipa deni wahojiwe kama walitendewa haki
•Mwanasheria mkuu na DPP wamepungua sana kuongoza ofisi za umma,
kwa kuwa wamechafuka sana Samia atangaze kujitenga nao rasmi
•Vikosi ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama zilivyotumika kuumiza watu vivunjwe mara moja , viongozi wa vikosi hivyo wachukuliwe hatua, wanasiasa waliosimamia hivyo vikosi na watumishi wa umma wawajibishwe
na familia zote zilizoathirika na matendo maovu yatokanayo na vyombo vya ulinzi na usalama waombe msamaha na walipwe fidia
•Wanasiasa, wananchi na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyoumizwa waombwe radhi na kuhakikishiwa usalama wao

HAYA MAMA DEMKA SASA au AMUA KUYAACHA..
7. AJIRA KWA VIJANA
👉Suala la ajira kwa vijana ni bomu la muda mrefu na linahitaji kuwa na mkakati wa kuondoa hili lazima Samia atoe muelekeo wa jinsi ya kutatua hili tatizo
👉Vijana wanamaliza vyuo na hakuna ajira inafika mahala vijana wanaona kusoma hakuna maana kabisa
You can follow @kigogo2014.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: