KILIMO THREAD: Watu wengi wamekua wakiuliza ni namna gani wanaweza kupata watu watakao wauzia mazao yao nje ya nchi: 🍇🍉🍊🥑🥬🌶️

Twende tukaone Kampuni unazoweza kufanya nazo biashara 👇👇👇
Je unalima na Unatamani kuuza mazao yako nje ya nchi lakini ujui uanzie wapi. Kupitia Uzi huu utaweza kujua kampuni zinazouza mazao mbalimbali Ulimwenguni kutokea hapa kwetu Tanzania na utaweza kuangalia namna utakayoweza kufanya biashara nao.
Uzi huu nitakuletea Kampuni zinazouza mazao mbalimbali Ulimwenguni kutokea hapa hapa Tanzania. Mawasiliano yao Kama utahitaji nitakupatia DM tafadhali. Bila gharama.
1. Rungwe avocado campany (Mbeya)

Zao: Hawa wanasafirisha Sana parachichi Ulimwenguni na wanalima Sana parachichi huko wilayani Rungwe.

Ujazo: Wanasafirisha mpaka Tani 1500 kwa mwaka.

Soko: EU, UK, France
2. Africado (Kilimanjaro)
Zao: Wanasafirisha Avocado Hass
Ujazo: Mpaka Tani 3000 kwa mwaka
Masoko: Wanauzia Sana EU, UK France

3. Mara farming Co LTD (subsidiary of Kenya based Co)
Zao: French beans, Passion na Peas
Ujazo: Mpaka Tani 500 kwa mwaka
Masoko: EU, UK Netherlands
4. Serengeti Fresh( subs of Sunripe in Kenya)
Zao: French beans, Peas, Soy beans
Ujazo: Mpaka Tani 1500 kwa mwaka.
Masoko: UK, Belgium France Netherlands

5. Darsh Industries Ltd
Zao: Nyanya (Processed)
Ujazo: Mpaka Tani 10000 kwa mwaka
Masoko: EU UK Mozambique Burundi
6. ECOVEG
Zao: Mbogamboga, Tango
Ujazo: Mpaka Tani 1.5 kwa week
Masoko: Hawa wamejikita zaidi soko la EAC (East Africa community)

7. Kilimanjaro Nature Ripe
Zao: Maembe
Ujazo: Mpaka Tani 10 kwa mwaka
Masoko: Dubai na Oman
8. TAHA fresh horticulture logistics
Zao: Mazao yote ya Mbogamboga
Ujazo: Mpaka Tani 1109
Masoko: EU na UK inategemea na mteja yupo nchi gani.
Hizi ni Baadhi tu.
You can follow @AbdulazizMomba.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: