MOYO WANGU UNAVUJA DAMU
Walking around pretending I'm okay.
Acting like I'm fine each and everday.
No one knows how I truly feel.
No one knows my heart won't heal.
Who do you turn to when no on cares?
What does it take to stop the pain?
When will my heart cease to bleed?
UZI👇
Bi GRACE STEPHANO MABALE alikuwa ni mzaliwa wa Mkoa wa kagera,wilaya ya Misenyi kijiji cha Kantare.
Bi GRACE STEPHANO MABALE aliolewa na Bwana EDWARD NYAKI MINJA. Bi GRACE STEPHANO alikuwa ni mtumishi wa Halmashauri ya Dodoma vijijini katika idara ya ardhi. Bwana Nyaki Minja alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa akiuza mbao kutoka Iringa pale mkoani Dodoma.
Katika ndoa yao walibahatika kupata watoto wawili ambao ni AGNES STEPHANO(37) na THOMAS STEPHANO(27)watoto hawa walipishana miaka kumi.
Baadae wanandoa hawa walitengana na Bi GRACE STEPHANO akabaki na watoto wote wawili. Ndio maana wana SURNAME ya mama Yao.
Maisha yaliendelea vizuri mpaka siku moja mwaka 1999 mwishoni na 2000 mwanzoni Bi GRACE STEPHANO MABALE aliporudi nyumbani na mwanaume mmoja na mwezi mmoja baadae akawatambulisha wanae kuwa kuanzia siku hiyo na kuendelea yule ndio atakuwa baba yao.
Baba huyo mpya aliitwa ZACHARIA KADUDU aliyekuwa ni mwanajeshi mwenye cheo cha SERGEANT akihudumu kwenye ofisi ya Mshauri wa Mgambo mkoni Dodoma. Kwa kuwa AGNES na THOMAS walikuwa wadogo,hawapata akili ya kuhoji lolote hivyo wakampokea ZACHARIA KADUDU kama baba yao mpya.
ZACHARIA KADUDU tayari alikuwa na watoto wawili wa kiume ambao ni JOHN KADUDU aliyekuwa na umri unaopisha kidogo na AGNES na GOODLUCK KADUDU aliyekuwa na umri sawa na THOMAS.
Kwa kuwa wazazi wao walikubaliana wawalee watoto wote under one roof, watoto wa mzee KADUDU wakahamia kwenye nyumba ya GRACE STEPHANO MABALE iliyokuwepo Area A, Kisabuje Street, Block No.30 Plot No.18 Pia wazazi hawa wakafunga ndoa ya kiserikali mkoani Dodoma.
Mzee KADUDU akataka watoto wabadilishwe ubini wabebe wa kwake, Kwa kuwa AGNES alikuwa mkubwa kidogo alikataa kubadili jina lakini THOMAS alipelekwa mahakamani hakiwa hajui lolote akabadilishwa ubini akapewa ubini wa ZACHARIA KADUDU.
Mwaka 2002 Bi. GRACE alijifungua mtoto wa kiume ROGERS ZACHARIA KADUDU. Hivyo akawa na watoto watatu uzao wa tumbo lake. Wawili aliozaa na EDWARD NYAKI MINJA na mmoja ROGERS aliozaa na ZACHARIA KADUDU. Hapa ndio mambo yalibadilika.
Mzee KADUDU akaanza kuwa violent,Vikaanza vipigo visivyohesabika kwa mkewe mara kwa mara tena mbele ya watoto. Mzee alikuwa ni Mlevi na mhasherati kweli kweli. Akawa anatembea hadi na mabinti wa kazi. Kadudu akawa kadudu kweli mitaa ya CHINANGALI Dodoma mjini.
Matukio yalikuwa mengi san ya manyanyaso kwa watoto na mkewe. Lakini kila watu wakimshauri GRACE STEPHANO MABALE aachane na huyo mzee muhuni waaapi! Alikuwa hasikii. Si unajua tena sikio la kufa... Mzee kadudu alikuwa ka kesi za mimba mara kwa mara kutoka mitaani.
Sasa kuna wakati Bi GRACE STEPHANO MABALE alisafir kikazi, huku nyuma kuna mama jirani alimfata dada yake THOMAS, hapa namaanisha AGNES akaenda kumwambia kuwa aende akaone nyumba ndogo ya baba yao imejifungua. AGNES alipoenda aliona gari la baba yao likiwa limeegeshwa...
...Kwenye ile nyumba ambayo aliambiwa ndipo mchepuko wa baba yake unaishi. Aliposogea karibu kweli aliweza kuisikia sauti ya baba yake akiwa ndani. Baada ya mama yao kurudi kutoka safari AGNES akamwambia kila kitu. Mama yao akaenda kumuhoji mmewe juu ya hilo. Lilikuwa kosa..!
Unaambiwa siku hiyo hakuna kipigo ambacho Bi GRACE halikokosa. Pia binti yake AGNES alipigwa vibaya mpaka akavunjwa taya ikabidi akimbie pale nyumbani. THOMAS alikuwa akishuhudia yote haya lakini kwa kuwa alikuwa mdogo. Pichank ni dada AGNES
Pia yule mtoto ROGERS aliyezaliwa, ingawa alizaliwa akiwa pande la baba,alikuwa na matatizo ya ngozi na maradhi ya mara kwa mara. Alikuwa ni wa kwenda hospitali kila wakati.
Kuna wakati mama yao alipata courage ya kwenda kupima afya yake. Akasindikizwa hospital binti yake. Kwa bahati mbaya sana majibu yake yakatoka H.I.V POSITIVE. Yaani alikuwa ni mhathirika wa Virusi vya UKIMWI just from a careless and selfish husband KADUDU😭😭😭
Mama huyu alipata mshtuko mkubwa sana baada ya majibu yale hali iliyomfanya augue ugonjwa wa shinikizo la damu. Presha ilimsumbua kwa miezi mitatu tu na tarehe 31 October 2005 aliaga dunia. Kina AGNES,THOMAS na ROGERS wakawa wamempoteza shujaa wao😭😭😭😭
GRACE STEPHANO MABALE alizikwa kijijini kwao KANTARE wilaya ya Misenyi mkoani kagera.
Baada ya mazishi ya GRACE, hayakuwa sawa kabisa. Mzee kadudu akaendeleza ufuska wa kuleta wanawake kwenye nyumba ya marehemu mkewe kwenye kitanda cha marehemu mkewe hata kabla harobaini haijaisha😭😭. Pia hakuacha kuwa violent kwa watoto wa marehemu.
Familia ya marehemu GRACE ikaazimia kuwachukua watoto. Ikaamuliwa wakalelewe na mama yao mkubwa huko Bukoba. Hapa ndipo likafanyika tukio la sintofahamu...
Thomasi alimshuhudia baba yake akijikata kidole kkwawembe kisha akamkata ROGERS na kuchanganya vidole vyao vyenye damu.
THOMAS kwa umri wake hakuelewa maana ya lile tukio lakini aliweza kumuuliza baba yake kwa nini amefanya vile. Akajibiwa wamejikata wakati wanamkata kucha. Watoto wote watatu wa marehemu GRACE wakahamia rasmi Bukoba mwaka 2006. Mwaka 2007 ROGERS akaanzishwa chekechea.
Huku nyuma mzee KADUDU aliuza mashamba,Viwanja na nyumba walizomiliki pamoja na marehemu bila kuwapa chochote watoto wa marehemu. Alishindwa kuuza nyumba moja tu ambayo marehemu alikuwa ameiweka kwa jina lake. Ni ile nyumba ya Area A. Tarehe 12 Dec 2006 mzee KADUDU alifariki.
Kule Bukoba ROGERS afya yake ilikuwa sio madhubuti akawa ni mtu wa kupekekwa hospitali mara kwa mara. Kina THOMAS na AGNES mara nyingi walikuwa nje ya Bukoba kimasomo. Mama yao mkubwa aliwalea kwa mapenzi yote kama mama yao mzazi.
Mawasiliano baina yao na wale watoto wengine wa mzee KADUDU yalikata ghafla tu baada ya wake watoto kuonyesha dalili za kutotaka mawasiliano na pia walibadili namba zao za simu. Inasemekana walirudi Morogoro ambako ndiko alitoka marehemu baba yao.
Inaendelea...
Wakati naendeleza hii story msiache kuja telegram manake kumekucha balaa. Mfate admin kwa link https://t.me/Thy_Quizer  Akuunge.Pia nisiache kuwashukuru ndugu zangu🙏🙏🙏 kwa kunibeba kwa mbeleko ya chuma.
Hali ya Kiafya ya ROGERS haikuwa sawa kabisa. Mwaka 2010 mama yao mkubwa alirudi kutoka hospitali akawaambia ROGERS amakutwa na mchafuko wa damu. Wawe wakini kumwangalia asiumie akatoka damu. THOMAS alikuwa anampenda sana mdogo wake,alikuwa anamwogesha na kumpa huduma mbalimbali
THOMAS anasema mwaka 2012 alipoenda Bukoba akamkuta dada yake naye alikuwa karudi nyumbani. Wakampeleka ROGERS ambapo waliambiwa ROGERS ana VVU. Habari hii iliwapa simanzi sana. THOMAS akakumbuka lile tukio aliloona la kuchanganya damu hapo ndio akafunguka maana ya tukio lile.
Akawaeleza ndugu zake ule mkasa wa nyuma. Vilio vikaanza. Wakapiga moyo konde kumlea ROGERS. THOMAS hakuwa kwenye mahusiano yoyote ya kimapenzi lakini akapiga moyo Konde kwenda kupima afya yake.
Alipopima alikutwa NEGATIVE. Aliporudi nyumbani mdogo wake akamuuliza "KAKA NITAPONA"? kaka mtu akamjibu utapona kisha akamkumbatia ili kuficha sura yake isionyeshe machozi yaliyokuwa yameanza kumtoka. THOMAS anasema kuanzia siku hiyo aliongeza upendo mkubwa kwa mdogo wake.
Mwaka 2018 ROGERS alihitimu kidato cha nne. Matokeo yalipotoka 2019 hakuwa amefanya vizuri kwani alikuwa ni mtu wa hospitali kila wakati. Wakati matokeo yanatoka ROGERS alikuwa terminally ill tangu January 2019 akisumbuliwa na ini na figo akiwa hawezi kukaa wala kujigeuza😭😭
Alikuwa amelazwa GOVERNMENT HOSPITALI Bukoba akiwa hawezi hata kula. Ilipofika tarehe 30 September 2019 ROGERS akaomba apelekwe nyumbani kwani amechoka kukaa hospitali. Mama yake mkubwa akamuombea discharge akaruhusiwa.
Siku hiyo hiyo jioni kaka yake THOMAS alimpigia simu kumuulizia hali yake akajibu "Kaka nimechoka,tutaongea kesho".
ROGERS didn't make it because the next day he threw the towel, Yes! he kicked the bucket to end his restless 17 years of sufferings and offensive world😭😭😭
ROGERS alizikwa karibu na kaburi la mama yake. ROGERS alikuwa ni kijana shujaa ambaye maisha magumu aliyopitia tangu utotoni pamoja na magonjwa alipambana nayo. Alilala na kuamka kupambana miaka yote 17 duniani.
Sasa tunasogea kwenye sehemu muhimu zaidi. Niwakumbushe tu Mara baada ya Bi GRACE STEPHANO MABALE kufariki yule mumewe wa kwanza EDWARD NYAKI MINJA alijitokeza na kutaka kuwachukua wanae THOMAS na AGNES lakini KADUDU mdudu alimtolea bastora aondoke na hakuonekana tena.
Watoto hawana kumbukumbu yoyote ya baba yao,hata album ambayo ingeweza kuwa na picha yake hawana. Walikuwa wadogo sana kuweza kuhandle nyaraka ukizingatia na Stress za kifamilia. Pia kuhama inawezekana kulichangia upotevu wa album au labda KADUDU mdudu alizipoteza makusudi.
Familia hii inamtafuta sana baba yao. Wana kiu ya kujua taarifa zake pa kuanzia hawajui. Yeyote mwenye clue ya mtu aitwaye EDWARD NYAKI MINJA please nakuomba DM. kama unajua hata ndugu zake,watoto au mke please waambie watoto wake wanammiss sana.
THOMAS amekuwa TRAUMATIC kutokana na mlolongo wa maisha aliyopitia. Pia akajikuta ana tatizo la ANGINA PECTORIS kutokana na kuwa mtu wa DEPRESSION. Amekuwa ni mtu mwenye ukosefu wa usingizi(IMSOMNIA) na anaishi kwa kutegemea Sleeping Pills.
Dada yake naye amekuwa Alcoholic nahisi yote ni sababu ya msongo. Actually THOMAS alinifata baada ya kusoma kile kisha cha askari aliyejinyonga nilipoandika DEPRESSION KILLS if we don't find someone to talk to. Aliona hii ndio tiba sahii kuzungumza yanayomuumiza
Amekuwa ni mtu wa kujifingia na kulia. Naombeni wote mnaosoma UZI huu mwambieni THOMAS pigana kama alivyopigana shujaa ROGERS. Thomas yuko tayari kupokea ushauri nasaha. Kwa anayemjua Mtaalamu wa counselling DODOMA please nakuomba DM. Nilimuomba mmoja lakini hakujibu hata text.
THOMAS anaamini wakiweza kujua taarifa za baba yao watakuwa wamezitibu sana nafsi zao. Pia yeye na dada yake wote ni wasomi. THOMAS ana Diploma ya Maendeleo ya jamii na AGNES ana Bachelor degree ya Tourism. The just need a little counselling to remake and Stand stall.
You can follow @fbuyobe.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: