Kikundi cha watalii kilitembelea mto wa kufugia mamba na walikuwa wakielea kwenye meli ndogo katikati ya mamba wenye njaa. Ikasikika sauti ya mmiliki wa eneo hilo ikisema: "Atakaye ruka kwenye maji na kuogelea kutoka nje atazawadiwa dola milioni 10".
Kila mtu kimya, ghafla mwanaume mmoja akajirusha majini. Alikimbizwa na mamba kwa bahati nzuri alitoka salama. Akatangazwa mshindi. Wakati anarudi hotelini na mkewe akamwambia mkewe "Aisee sijajirusha mwenyewe majini, kuna mtu alinisukuma nikapambana niokoe maisha yangu".
Mke wake akatabasamu na kusema "Ni mie ndio nilikusukuma". Wewe ungemfanyaje kama ni mkeo? Simulizi linatufundisha: "Nyuma ya kila mwanaume mwenye mafanikio kuna mwanamke anayemsukuma kufikia mafanikio". #ElimikaWikiendi