UBINADAMU WA ROMELU LUKAKU KWA MARCUS RASHFORD NA MAANA HALISI YA MAISHA KWETU SISI WOTE.
IT IS THREAD TIME @chawanyu
IT IS THREAD TIME @chawanyu

Usiku mmoja wa Feb 12,2019, ulipigwa mtanange wa kukata na Shoka kati ya Man United vs Psg. Mechi ya kwanza iliyopigwa Old traford Man United alipoteza 2-0 kwa magoli ya Kimpembe na Mbappe. Najua hiyo siku bwana @geoffiejeff aliumia sana


Huku ikionekana Man United wanaweza wasishinde mechi ya Pili kwenye uwanja wa PSG Stade des Princes kutokana na ubora wa PSG, na majeruhi ya baadhi ya key players wa Man United, Hvyo mashetani wekundu walikua na matumaini madogo sana ya kufuzu next round.

Siku ya mechi ya marudiano ikafika, Man United wakiwa kwenye Jiji la kifahari, mjini Paris, wakiwa na matumaini madogo kabisa ya kufuzu hatua inayofuata, from no-where usiku wa hiyo mechi yalifanyika maajabu!

‘Big Man’ Bolingoli Lukaku, alitupia goli 2 za fasta ndani ya dk ya 2 na 30, matokeo hapo yanasoma aggregate 2-2. Mpaka hapo Man United walihitaji goli moja zaidi ili wafuzu. Mungu si athumani, Dk ya 94 Man United wanapata tuta.
Sasa hapa story sio Penati ya Man United, Sio story Man United anaenda kufuzu, story sio PSG na ubora wake wanatupwa nje ya mashindano, Unajua nini?

Wakati kila shabiki na kila mdau wa Soka akiamini Lukaku ataenda kupiga Penati ya Ushindi ili achukue mpira kwa Hat-trick ya Usiku huo, Lukaku anampatia Mpira Rashford akandamize Msumali wa moto kwa PSG. Hakuna alieamini, hata Rashford hakuamini. Lukaku alituachia Funzo

Moja, Kumsaidia mwingine ainuke, nae awe sehemu nzuri ya Maisha,
hakukupunguzii wewe chochote. Ubinafsi usiwe sehemu ya maisha yetu.
hakukupunguzii wewe chochote. Ubinafsi usiwe sehemu ya maisha yetu.
Mbili, Wazungu wana msemo wao bora kabisa, wanasema. “If you're on the rise towards success, don't leave others behind - it can be boring being alone up there” - Raha ya Mafanikio wabebe na walio nyuma yako. Itaboa ukifanikiwa pekee yako. Kwa sababu

Lukaku angeweza kufunga penati, kupata hat trick na kuonekana kila kurasa ya gazeti, ila alimkabidhi dogo, ambae aliona ni wakati wake na yeye kuandika historia Maishani, Lukaku katufundisha Kamwe usiwasahau washikaji zako wakati ukielekea kwenye kilele chako cha mafanikio.

Mwisho Kabisa, Ukiaminika, ukapewa nafasi ya Kung’aa usimuangushe aliekubeba, muonyeshe kuwa hakukosea kukuamini, kama Rashford alivyofanya kwa kupiga penati bora kabisa na kuipa Ushindi Man United.