◾️Unawezaje kukumbuka sehemu uliyo-pack gari au kifaa chako kwa kutumia Google Assistant

Hakuna kitu kibaya kama kusahau sehemu uliyo-pack gari/kifaa chako lakini kwa bahati nzuri kama una iPhone, iPad au Android smartphone unaweza kukumbuka kwa urahisi

Uzi mfupi 👇
◾️Tuanze kuangalia Google Assistant kwa Android

Kitu cha kwanza unachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha Google Assistant ina-acess location yako kwenye simu yako

Unatakiwa ku-enable location/ weka location ON

Settings >> location >> use location >> switch ON
Baada ya hapo, unatakiwa kufungua Google Assistant kwenye simu yako [ Make sure uko sehemu ya Parking/sehemu unapoacha gari/kifaa chako ]

Kuna namna mbili za kufungua Google Assistant kwa Android smartphone

◾️sema "Okay, Google” au “Hey, Google.”
◾️Kwa wanaotumia
Android 10 na kuendelea unaweza ku-swipe either chini kwenye kona ya kulia au kushoto

◾️Baada ya Google Assistant kufungua na kusikiliza unatakiwa kusema yafuatayo

“I parked here.”

“Remember where I parked"

Hapo Google Assistant itakumbuka sehemu uliyo-pack na kuweka
Kwenye Google Maps

Baadae ukirudi kutaka kujua sehemu uliyo-pack, fungua Google Assistant kisha sema moja kati ya hizi command

“Where’s my car?”

“Where did I park?”

“Find my car’s location"

Google Maps itafunguka na kukuonyesha sehemu uliyo-pack, nenda kachukue gari yako
◾️Google Assistant kwa iPhone au iPad

Kabla ya kuanza kutumia Google Assistant Hakikisha "Location services" iko ON [location services is enabled ]

Settings >> privacy >> Location services [ put it ON ]

Baada ya hapo fungua App ya Google Assistant
Baada ya kufungua app unaweza kusema  “Okay, Google" au bofya kwenye "Microphone" icon

Ikiwa Google Assistant inasikiliza, sema moja kati ya hizi command

“I parked here.”

“Remember where I parked.”

Google Assistant itasave parking location kwenye Google Maps
Baada ya kazi zako kama ukitaka kujua sehemu uliyo-pack gari,

Fungua Google Assistant app kisha sema moja kati ya hizi command

“Where’s my car?”

“Where did I park?”

“Find my car’s location

Map itafunguka na kuonyesha sehemu uliyopack gari

Retweet

Uzi under @chawanyu
You can follow @TOTTechs.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: