UZI MAALUM KWA WANAKAGERA KUHUSU MAGUFULI KUHUJUMU UWANJA WA NDEGE OMUKAJUNGUTI
NILIELEZA JAMIIFORUMS KWAMBA..
Kwanini Chato International Airport na si Omukajunguti international Airport? Kagera inaonewa sana
Mpango wa omukajunguti ni wa Siku nyingi

Je, mnatambua kuwa serikali imeshiriki katika kuudumaza mkoa kagera?
Hivi ndivyo mkoa kagera umeachwa yatima na serikali yaCCM,
Tulivyopata Uhuru kagera ilikuwa miongoni mwa mikoa 3 ya uchumi imara,
1.Dar es salaam
2.Kagera
3.Kilimanjaro
Lakin ukweli usiopingika Kagera imetelekezwa na serikali vya kutosha bila kujali majanga yaliyoikuta au michango ambayo Kagera imetoa kwa watanzania.

Kila MTU kutokea Kagera atakuwa ana kumbukumbu zinazomfanya kusononeka sana,
SABABU ZA KAGERA KURUDI NYUMA KIMAENDELEO NA CCM HAIONI HILI
1.VITA YA KAGERA,1978/79
Vita ya nchi nzima ilipiganwa kwenye mkoa mmoja na kuharibu miundombinu vya kutosha , na ule ndo ulikuwa uwanja wa vita hasa, lakini hakuna sehemu yoyote kuna strategy za kuujenga upya mkoa,
tunaishia kusikia maneno ya kashfa tu tena toka kwa viongozi wakubwa kwa wanakagera eti mmeshindwa kujenga hata chuo kikuu kimoja? Aliuliza Kikwete lakini kasahau kuwa yeye kama mkuu wa serikali hajajenga hata chuo cha kutoa cheti.
2. JANGA LA UKIMWI 1983,
Kama inavyojulikana Kagera iko mpakani mwa Uganda, na UKIMWI umeanzia Uganda, na kwa kuwa wana Kagera wana utaratibu wa kufanya Biashara na Uganda , haikukwepeka kupata UKIMWI, nguvu Kazi kubwa ilipotea sana miaka hiyo na kusababisha uchumi kurudi nyuma
3. AJALI YA MV BUKOBA
Janga la pili ambalo linafanya kudhoofisha mkoa wa Kagera ni kuwa , watoto wengi yatima wameongezeka , nguvu kazi imepungua kutokana na ajali ile.
4.1998 EL NINO
Wengi mnaelewa kuwa imekumba sana ukanda wa kanda ya ziwakuliko kanda yoyote ile hapa nchini ,
imeharibu miundombinu na kupoteza wazalishaji Mali,

5. KUSHUKA KWA BEI YA KAHAWA 1998 KWA UZEMBE WA SERIKALI.
Inajulikana Kagera ilitegemea sana Kahawa kama kitega uchumi , kwa uzembe wa serikali hakukuwepo utaratibu wa kuhakikisha Kahawa inabaki na bei ya kuridhisha badala...
yake ikapuuza mpaka wananchi wakakata mibuni maana haikuwa na maana tena,

6. UBAGUZI ULIOJIFICHA TOKA KWA VIONGOZI ( INDIRECT DISCRIMINATION TOWARDS HAYA TRIBE)
Miaka ya nyuma hakuna ambaye hajui kuwa wahaya waliwekewa mizengwe katika baadhi ya sekta, hata kwenye elimu ,
walipandishiwa alama za ufaulu ili wachache waendelee na elimu ya juu maana walionekana kuwa wao ndio wanafaulu na kujaza madarasa mengine, lakin ili kuitamka sentensi hii (INAHITAJI UJIFANYE MWENDA WAZIMU KIDOGO)
Hii CCM mnaelewa na wazee wanajua,alafu anatokea mtu anasema CCM?
7. KUTENGWA NA NCHI KIJIOGRAFIA
Kagera iko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, waliowahi kufika uko ndio wanaelewa namaanisha nini, Kagera imekuwa kama kisiwa maana jinsi ya kufika kule inabidi ukatishe kilometer kadhaa za msitu, ili uingie Kagera,au upite.......
Au upite ziwani kwa meli ndo uende mikoa mingineyo ambayo ni ya Tanzania,hivyo basi wana Kagera walikuwa na urahisi wa kufanya Biashara na Uganda kuliko mikoa mingine ya Tanzania, lakini serikali ilikataza biashara hiyo,wakajikuta wamebaki kama kisiwa ndani ya nchi yao wenyewe,
8.KAGERA KIMBILIO LA WAKIMBIZI MAUAJI YA KIMBALI YA RWANDA 1994 NA MACHAFUKO TANAYOENDELEA UKANDA ULE.
Wanyarwanda wameiteka Kagera hasa wilaya ya Karagwe na Muleba na kujichukulia ardhi , pia wamekuwa watekaji wa magari na kudhalilisha wana kagera
,kitu amabacho kimerudisha
nyuma uchumi wa mkoa, kwa kasi, majambazi wametamalaki na kufanya uharamia ambao umefanya kusiwepo hali ya utulivu na kujenga uchumi, serikali imechelewa kuchukua hatua,
9. KUTOJUMUISHWA KATIKA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO KIKANDA
Kila kanda imetengwa katika kanda mkakati wa maendeleo lakini kanda ya ziwa ambayo ndipo kuna mkoa Kagera hakuna ilipoainishwa katika mpango wa maendeleo.Kagera Umekuwa ni mkoa wa kujitegemea kwa kila kitu utasikia
Ukumbi wa mkutano unajengwa Arusha, sijui chuo cha utalii Dar, chuo cha ufugaji Tabora.

Chuo cha reli tabora, chuo cha science cha nelson Mandela arusha,
Chuo cha serikali cha ugavi, Chuo cha ushirika Moshi Mara..

KWANINI LAKIN CCM MNAWAONA KAGERA NI WAJINGA KIASI HIKI?
Chuo cha mbao Iringa, kwanini Kagera hakuna mipango endelevu, sasa upo wapi uwanja wa Mukajunguti wa ndege na ulishaahidiwa kuwa wa kimataifa na kutengewa bajeti kipindi cha Mkapa?,Rais Magufuli halioni hilo?
Kagera wanekuwa wa kupandia kama daraja, CCM Muwe na aibu kwa Kagera
SOMA HII SASA SERIKALI INA KITU KINAITWA SUBJECTIVE AND OBJECTIVE PLANNINGS,(BIG FOUR REGIONS) IKO HIVI

1.KANDA YA KUSINI AU NYANDA ZA JUU KUSINI
Imetengwa kama kanda ya kilimo hapa kuna mikoa
Njombe,Mbeya,Katavi,Ruvuma,Na Iringa .
Ona sasa.... Upendeleo
2.KANDA NYINGINE KANDA YA KASKAZINI
Hii imeahinishwa na kupewa kipaumbele kama kanda ya utalii,
Mikoa ni
Arusha,
Kilimanjaro na Manyara,
3.NYINGINE NI KANDA YA KATI ,
Taasisi za siasa na Elimu ya juu
Mikoa ni
Morogoro,
Dodoma,
Singida,
Aisee CCM acheni dharau kwa Kagera
4. KANDA YA MASHARIKI INEPEWA Kanda ya viwanda na Biashara, mikoa ni
Dar es salaam,
Mtwara
Lindi
Pwani
Tanga

kanda ambayo kuna Kagera ndo hakuna chochote kilichopangiwa, CCM kagera Hamtatoboa
NAMALIZIA KWA KUSEMA SASA HATA ILE HELA YA TETEMEKO NDO MMEACHA AIBU, HAMJALIPA HATA VIBARUA WALIOJITOLEA KUJENGA IHUNGO, MPAKA SASA WANADAI, NA HELA HAIKUWA YENU ILIKUWA YA WAHISANI
You can follow @Britanicca3.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: