UZI: Nadhani umekutana na picha za hii couple zikizunguka mitandaoni, picha hizi zinawaonesha wapenzi wakiwa na tofauti ya kimuonekano.

Hali aliyonayo huyu mwanaume kitaalamu inaitwa "PROGERIA", Ni moja ya hali zinazotokea kwa nadra sana ambapo mtu huonekana mzee. #BongeLaAfya
Hali hii huanza kuonekana kwa mtoto miaka miwili baada ya kuzaliwa, Matatizo ya moyo na kiharusi (stroke) huwa sababu kubwa ya kupoteza maisha kwa watu wenye hali hii. Tafiti zinaonesha hali hii humpata mtoto 1 kati ya milioni 4 dunia nzima.
Ugonjwa huu hutokana na hitilafu katika jini ambayo hupelekea kutengenezwa kwa aina ya protini (progerin), Progerin ni abnormal mwilini, seli zikitumia protini hii hufa kwa urahisi na hivyo mtu kuzeeka haraka. Mtu harithi ugonjwa (not inherited).
Watoto wenye ugonjwa huu huonekana wenye afya njema wakati wa kuzaliwa ila baada ya mwaka mmoja dalili kama;
-Kichwa kikubwa
-Macho makubwa
-Pua nyembamba
-Mishipa kunekana
-Meno kukua taratibu
-Sauti nyembamba
-Nywele kutoka
-Kupungua uzito au kasi ya ukuaji.
Kadiri mtoto anavyokua kutokana na ugonjwa huu mtoto huanza kupata magonjwa na matatizo wanayoyapata wazee. Mpaka sasa haijapatikana dawa ya kutibu japo wataalamu wa tafiti bado wanaendelea kutafuta dawa. Kwa sasa kuna aina ya dawa wanayotumia pia wagonjwa wa saratani.
Dawa hii husaidia kupunguza na kuchelewesha baadhi ya dalili. Ukiona mtoto ana dalili hizi fika hospitali umuone daktari ambaye akigundua ni tatizo hili atakutuma kwa daktari wa watoto.
You can follow @FestoNgadaya.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: