Najma ni rafiki yangu sana nilikutana naye TikTok.
Kama ilivyo kawaida ya mitandao, aliweka picha na video zilizonivutia sana na nikatamani tujamiiane nje ya mtandao huo. Nilijituma sana ku-komenti, ku-like picha na video zake hata kuzama katika dimbwi la ‘DM’ yake kwa meseji

zilizochuruzika upendo na kusindikizwa na emoji za makopa.
Kwa kipindi zaidi ya mwezi mmoja, Najma alitazama meseji zangu kama hazioni wakati kwenye comenti akijibu kwa kifupi tena kwa kizungu ‘thank you’. Kwa wasioijua ‘thank you’ maana yake ni asante.
Kwa kipindi zaidi ya mwezi mmoja, Najma alitazama meseji zangu kama hazioni wakati kwenye comenti akijibu kwa kifupi tena kwa kizungu ‘thank you’. Kwa wasioijua ‘thank you’ maana yake ni asante.
Nadhani umeelewa hisia za mvurugo unazoweza kupata pale unapoeleza hisia zako za upendo na kujibiwa kwa neno moja tuu ‘asante’.
Kuna siku sina hili wala lile niko zangu nafanya mazoezi kutengeneza mwili wa picha, huku nikiwa nimevalia headphones
Kuna siku sina hili wala lile niko zangu nafanya mazoezi kutengeneza mwili wa picha, huku nikiwa nimevalia headphones
nikisikiliza muziki wa kuniongezea mzuka, mara paap… nikasikia notification yenye mlio wa pekee kwenye simu yangu. Jambo ambalo sikuona ni la muhimu kukwambia ni kwamba tayari Najma alishaanza kutawala moyo kiasi cha kwamba kuna maamuzi niliyafanya bila kujua.
Tayari nilishaseti kamlio maalumu kwa ajili ya kuarifiwa endapo Najma ataweka chochote kwenye ukurasa wake.
Moyo ulipasuka paa, nikiwa siyaamini macho yangu, kiarifu (notification) kilionesha ujumbe kutoka kwa Najma.
Moyo ulipasuka paa, nikiwa siyaamini macho yangu, kiarifu (notification) kilionesha ujumbe kutoka kwa Najma.
Tena kilionesha ni meseji na sio komenti, moyo ulitokwa na jasho la furaha. Asikwambie mtu hisia za mapenzi zinajua kuipumzisha akili aisee. Ndani ya sekunde kadhaa nilishafuta jasho la mikono na kutoa nywila kwa kuweka alama ya dole gumba katika simu yangu na tayari uso
uligubikwa na tabasamu kama mtu aliyeshinda michezo ya kubahatisha.
‘Hi Malili, sorry I haven’t been looking at my DMs for so long. You seem to be a good person, how are you?’. Kwa wale tuliokimbia umande hapa Najma alimaanisha kwamba hakuwa anasoma meseji kwa muda mrefu

na amefurahishwa na mwenendo wangu na anashuku kuwa naweza kuwa mtu wa maana. Najma amekamilisha ujumbe wake kwa salamu yenye ishara ya kuendeleza mazungumzo.
Yeah….!, kichwani kawimbo ka Zali la Mentali kalianza kutumbuiza kwa mbali na kunifanya niporomoshe mistari kwa ustadi
Yeah….!, kichwani kawimbo ka Zali la Mentali kalianza kutumbuiza kwa mbali na kunifanya niporomoshe mistari kwa ustadi
mkubwa sana. Bahati nzuri kizungu cha kuombea maji na kurudisha glasi kilikuwepo na bado kipo. Basi ukawa mwanzo wa mahusiano moto moto ndani na nje ya mtandao.
Kwa bahati nzuri, Najma ni msichana aliyekuwa akifanya kazi nzuri na pia ametoka katika familia ya uchumi wa kati,
Kwa bahati nzuri, Najma ni msichana aliyekuwa akifanya kazi nzuri na pia ametoka katika familia ya uchumi wa kati,
hivyo sikuambulia maumivu kama ya x zangu wengi. Mapenzi yetu yalianza kwa nguvu, mambo ya dina, vacation na mbwembe zote za kuunga mkono juhudi za mioyo. Wajumbe wote walitupitisha mpaka kamati kuu ya mashemeji na familia zilielewa.
Safari yetu ilikuwa nzuri sana isipokuwa kwa jambo moja tuu ambalo sikuwahi kulisemea kwa kulinda kitumbua kisiingie mchanga. Najma alikuwa akimaliza bando lake mapema sana. Nilikuwa nikimuunganisha kifurushi cha Jimwage cha Vodacom kila mwezi ambacho kina GB 60 (TZS 50,000).
Penzi lilivyo la ajabu, maumivu ya 50,000 sikuyasikia kabisa. Kifurushi hiki mimi nilikitumia kuangalia mpira, kuangalia na kupakua movie na muziki YouTube, lakini hakikuisha. Wakati mwingine niliwaunganisha mpaka washkaji Wi-Fi lakini bado kilidumu mpaka muda wa bando ulipoisha.
Kwa malkia wa moyo Najma ilikuwa tofauti sikujua ni nini kilisababisha kila baada ya wiki mbili ando lake linaisha. Mwenyewe alisema hajui, hafanyi chochote zaidi ya kuingia kwenye mitandao na kuanganisha Wi-Fi kufanya kazi za ofisini kwenye laptop yake.
Akawa analalamika anaibiwa bando na mimi nikawa nahisi story za wizi wa bando huenda zikawa za kweli. Daah, nafanyaje sasa.
Baada ya kumzoea na kujenga hekaya ya makopa, siku nikaamua kumuomba simu yake niangalie tatizo. Mwanzo alinishangaa kwa nini namuomba simu,
Baada ya kumzoea na kujenga hekaya ya makopa, siku nikaamua kumuomba simu yake niangalie tatizo. Mwanzo alinishangaa kwa nini namuomba simu,
nataka nipekue chats zake lakini nikamwelewesha akanielewa. Kupekua nikakuta kumbe Najma alikuwa akimfaidisha moja ya jirani yake aliyekuwa akiishi naye katika apartment moja.
Najma alijiunga na Wi-Fi kwa lengo la kutumia internet kwenye laptop yake kupitia simu. Lakini hilo halikuwa tatizo. Tatizo ilikuwa ni Najma kutokuweka password katika simu yake.
Na mshkaji wa jirani (jina tunalihifadhi) alipogundua akatumia kama ganda la ndizi kuteleza.
Akawa anasubiri kila Najma akirudi kazini anajiunga na kudownload na kufanya kila alichotaka kufanya.
Akawa anasubiri kila Najma akirudi kazini anajiunga na kudownload na kufanya kila alichotaka kufanya.
Daah, wanaopenda vitonga wapo wengi. Najma hakuamini, alikasirika sana na kufoka “‘mxie…huyu kaka hana adabu kabisa…mwizi mkubwa…kwanza alinitaka nikamkatalia halafu ananifanyia ushenzi.
Aaah! Basi na mimi nikachukua point zangu tatu. Nikamtuliza bibiye na kumwekea password ngumu kama password ya BOT.
Nikashuhudia muujiza mwingine kama muujiza wa jua kuwaka huku mvua ikinyesha, Najma akanikumbatia kwa nguvu na kusema kwa sauti ya mapenzi, nakupenda sana Malili.
Nikashuhudia muujiza mwingine kama muujiza wa jua kuwaka huku mvua ikinyesha, Najma akanikumbatia kwa nguvu na kusema kwa sauti ya mapenzi, nakupenda sana Malili.
Sijui kwa nini sikujibu DM zako mapema.
Mlume nikajibu kwa mbwembe na sauti ya kukoroma kama mtangazaji wa kipindi cha mapenzi. Baby
Mlume nikajibu kwa mbwembe na sauti ya kukoroma kama mtangazaji wa kipindi cha mapenzi. Baby