Mara ya kwanza kabisa kwenye "Today Show" aliweza kumpigia Piano Alicia Keys na baadae aliparticipate kwenye Radio Disney Next Big Thing hapa alikua na miaka 12

I used to know her

Mama yake alikua philippians na baba ni African-American akapatikana Gabriella Wilson
Ila tunamjua kama H.E.R akiwa mdogo sana anaanza kujulikana kama nlivoeleza awali kwenye Radio Disney na Today Show

Huu ni mwaka 2009 na alipofikisha miaka 14 RCA rec waliweza kumsign na kwa mara ya kwanza aliachia single yake "Something to prove" mwaka 2014
Hapo alikua anatumia jina lake halisi ila ulipofika mwaka 2016 alianza kutumia H.E.R rasmi ambapo aliambatanisha na Ep zake mbili H.E.R Vol.1 na H.E.R Vol.2 bila kusahau The B sides

Mwaka uliofuata 2017 aliachia album yake aliyoipa jina "H.E.R" Hii ilikuwa Oct
Humu ndani aliweka baadhi ya ngoma za kwenye Ep zake na akaongeza ngoma 6 mpya,kulikua na ngoma kama Focus,Pigment na 2

Hapa unapata ile Pure R&B yani hakuna makelele kabisa unaenjoy music mzuri huyu mtoto kwanza ni mzuri halafu hana mambo mengi

Mwaka 2018 hapa nadhani
Wengi tulianza kumjua alipokuja na "I used to know Her:The Prelude" na a kaachia tena mwendelezo"I used to know Her part 2"

Nikiongea sana utasema labda ni mapenzi ila huyu mtoto anaimba wewe sikiliza Ep zake kati ya izo hapo juu utakubaliana na mimi
Kama utani mtoto anatokea kwenye Grammy za 61 na anakua kwenye category 5 na anashinda kama Best R&B performance na Best R&B album

Hizi Grammy ni za mwaka jana ndio Grammy za 61 na Grammy za 62 yani mwaka huu aliingiza "Hard Place" kama Song of the year....mtoto ana Grammy
Sasa kazi yote hii hawezi kufanya mwenyewe je ni nani walikua nyuma yake mpaka kufika hapa,kuna mtu anaitwa David Harris huyu ndie producer wake alie produce "H.E.R Vol.1" na "H.E.R Vol.2"

Hapa pia kulikua na watu waliotoa support kama Tyrese,Usher,Alicia Keys,Pusha T
Wyclef Jean pamoja na Bryson Tiller hawa walikua wakipost kazi zake via social media Yani Kure post kutoa S/O bila kumsahau Riri

Riri yeye alifanya kitu kimoja ambacho H.E.R hawezi kusahau alipost clip kule IG huku background ikiwa inasikika ngoma ya "Focus"
Hii clip ilitazamwa zaidi ya mara 5Mil na ilifanya Fan Base ya bi.dada kupanuka ilibidi watu waanze kumfollow chap

Awali kabisa wakati Bryson Tiller ametoka aliweza kumchukua H.E.R na kuzunguka nae kwenye Tour yake

Achilia mbali kina Tiller kuna waigizaji kama
Taraji P.Henson,Issa Rae waliweza kusupport kazi zake kwa ukubwa bila kuwasahau Kylie na Kendall Jenner hawa ni baadhi tu waliofanikisha moja ya hatua yake kwenye kazi kufika hapa alipo now

Baada ya haya yote The Rolling Stones walimueka H.E.R kwenye 10 artists
Ambao unatakiwa uwajue kwa mwaka 2017 pia Forbes walimtaja H.E.R kwenye ile list ya Top 5 alternative R&B artists 2017

Mtoto anazidi kupasua anga tu,unaambiwa H.E.R ana aibu kupitiliza na anasema hio ni sababu kubwa anavaa miwani muda wote
Anasema mwanzo wakati anaanza music alikua akijificha kuogopa kujulikana kwa kuhofia angepokelewa vibaya ila anashukuru haikua ivo

Finally anarudi anarudisha ahsante kwa fundi The Trap Soul Bryson Tiller anafanya nae kazi "Could've been" hii ni mwaka juzi
Hii ngoma ilizidi kuonesha ubora wake pia alitisha na "This way" akiwa na Khalid hii ngoma ilikua moja ya soundtrack ya movie ya "Superfly"

Najaribu kutaja ngoma popular hapa akaja na "Slide" akiwa na bedui YG

Tumeona pia mjukuu wa Bob Marley Skip Marley collabo yao ya
Slow down ikifanya kama utakumbuka Gut Feeling ya Ella Mai aliumiza sana mule ndani yani sauti kama ukiwa masikio popo huwezi kujua wapi Ella Mai wapi H.E.R

Hawa watoto kwanza ni warembo na vile vile wamebarikiwa sauti mpaka muda huu mimi kama Bw.Fisi sijui
Nimchague nani Ella Mai ni crush wangu lakini H.E.R ana nafasi yake kwa kweli

Tukiachana na kina Ariana Grande nazungumzia hiki kizazi chao hapa juzi juzi cha kina Ella Mai,mimi kama mimi kwenye table yangu atakaaa Ella Mai,Summer Walker,SZA,Kiana Lede na H.E.R over
Kwa umri wake miaka 23 na ana utajiri wa $2Mil sio mbaya sana naimani atazidi kukaza kwenye Game

Mkongwe Toni Braxton tumeona amemchukua kwenye ngoma yake mpya "Gotta Move on" nadhani vipaji vinajuana.

#CelebrityLifeStyle
#TillerBrief
You can follow @TillertheWorld.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: