SARE NA KITI CHAKO CHA OFISINI VIKUFUNDISHE JAMBO.

#uzimfupi
Ni juzi tu nilisoma hiki kitu mahali, sijui kama ilikuwa humu au ni kwenye group moja la WhatsApp.
Ni kuhusu Mambo ambayo afisa wa jeshi alikuwa anamwambia mwanajeshi mwingine aliyekuwa chini yakr kicheo. Alimwambiahttps://abs.twimg.com/emoji/v2/... draggable="false" alt="👇" title="Rückhand Zeigefinger nach unten" aria-label="Emoji: Rückhand Zeigefinger nach unten">
1. Kila siku unapozivua gwanda zako usiku na kuzitundika jiulize kwamba itakuwaje Kama itatokea siku hautakwenda ofisini na zile gwanda?
Na je itakuwaje kwa mtu ambaye yamkini hata hakusomea uanajeshi kama wewe lakini akazivaa zile gwanda zako na kwenda nazo pale ofisini kwako?
Jibu ni rahisi, Inawezekana kabisa wewe ukazuiliwa kuingia ndani na yule aliyevaa zile gwanda akaruhusiwa kuingia huku akipigiwa salute nyingi sana.
Hapo lazima ujifunze kuwa si wewe wala yeye alikuwa anapigiwa saluti na kupewa zile heshima bali ni cheo kilicho kwenye zile nguo.
Wakati wowote jifunze kwamba cheo/dhamana unayopewa mahali ni koti la kuazima hivyo jitahidi kukitumia kwa faida na maslahi ya wale uliowekwa kuwasaidia katika nafasi ile.
Usisahau Kwamba nafasi ile inaweza kuchukuliwa na mtu mwingine na wewe kutotambulika tena.
Jiandae kwa hilo.
2. Siku moja jioni kabla ya kufunga ofisi yako subiri watu wote watoke ofisini.
Amka kwenye kiti chako na nenda kaa kwenye kiti wanachokalia wateja wako wakati wanakuja uwahudumie.
Hapo jiulize kwamba, je itakuwaje siku nikiwa siko kwenye kiti cha kuwahudumia wengine?
Lakini pia jiulize, je hiki ninachofanya kupitia kiti hiki nilichopewa sasa kwa hawa wanaokalia kiti cha wateja ni sahihi kwa sheria na taratibu za kazi yangu?
Je kesho nikiwa Mimi ndio mteja na mwingine kakalia kiti ninachokalia Mimi Sasa nitafurahia huduma nitakayopewa?
Je, kesho akija ndugu yangu au mwanangu kupata huduma kupitia aliyekaa kwenye kiti hiki ambaye sio mimi, na akapata huduma sawa na ninayotoa sasa, atafurahi au hata Mimi nitafurahi nikisikia kapata huduma sawa na niliyokuwa nikitoa Mimi nilipokuwa kwenye hiki kiti?
Mwisho kumbuka kuwa maamuzi yoyote unayoyatoa ukiwa umekalia kiti chako cha ofisi, usiyatoe kwa utashi wako Bali kwa sheria na taratibu za kazi yako maana kile si kiti chako milele na kesho kinaweza kukaliwa na mwingine na akayabatilisha Yale yote uliyokuwa umepitisha yasiyo sawa
Hivyo kila unalofanya kwa dhamana (gwanda) na nafasi (kiti) unachopewa hakikisha kinanufaisha wale unaowatumikia na si kwa manufaa yako binafsi maana kwa kufanya hivyo utakapotoka pale na ukarudi siku nyingine kama mteja utahudumiwa kwa ukarimu na heshima kama ulivyokuwa ukifanya
You can follow @ZakayoMmbaga.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: