JINSI YA KUANZISHA BIASHARA UKIWA UMEAJIRIWA: Biashara yoyote iwe mpya au ya zamani ina changamoto zake especially kwenye mazingira yetu. 50% Ya biashara zote ndogo zinakufa katika mwaka wake wa kwanza kuanzishwa. UZI #ElimikaWikiendi
Mtandao wa Investopedia ulitoa sababu ya biashara ndogo kufa, 1. Mtaji Mdogo, 2. Uendeshaji Mbovu, 3. Mpangilio Mbovu wa Biashara na Bidhaa yako au huduma yako haihitajiki sokoni (Hakuna wateja wanahitaji bidhaa zako). Pamoja na sababu zingine nyingi.
Sasa kama tulivyoona hapo juu changamoto ni nyingi. Kabla ya kufikiria kuanzisha biashara ukiwa umeajiriwa inabidi ujipange. Kitu kimoja kikubwa ambacho Ajira itakusaidia kipindi unataka kuanzisha biashara ni MTAJI pamoja na muda wa kujipanga kabla ya kuanza biashara full time.
Kuna watu hua wanafikiria kuacha kazi ndio waanzishe biashara. Ndio unatakiwa kufuata ndoto zako lakini sikushauri hicho kitu. Asilimia kubwa ya biashara mpaka zianze kuingiza pesa inachukua hata mwaka mzima. So its either uwe ume save hela za kutosha kukusaidia muda wote huo
Hizi ni hatua chache za kufuata ili uanzishe biashara ukiwa umeajiriwa. Kwanza hakikisha mkataba wako na mwajiri wako unakuruhusu kufanya biashara ukiwa mwajiriwa wake. Kuna baadhi ya makampuni huwezi kuanzisha biashara ukiwa bado mwajiriwa wao. Soma Mkataba wako wa kazi
MUDA: Tambua kwamba biashara mpya inahitaji muda wako wa kutosha. Kuna muda wa kazi yako na muda wa biashara yako. Panga muda wako vizuri. Punguza au ondoa vitu ambavyo vinakumalizia muda wako na sio vya maana mfano Kuangalia Netflix, Social Media, Video Games, etc
WAZO LA BIASHARA: Usichague wazo la biashara na aina ya biashara ambayo hutaweza kuifanya part time. Mfano umefungua mgahawa au bar kama hautokuepo hapo full time kipindi cha mwanzo au huna msaidizi. UTALIA. Kama tulivyoona hapo juu moja ya sababu biashara kufa ni usimamizi mbovu
Kabla hujachagua wazo la biashara uchague au ufanye jipime skills, abilities, and weaknesses zako. Kisha focus biashara ambayo itakufanya utumie strength zako. Kama huna hio skill ambayo biashara unayotaka kuifanya tumia muda wako kujifunza au mpe hio kazi mtu mwingine akusaidie.
Tuseme ushachagua wazo lako la biashra. Kibinadamu ni rahisi kuona wazo lako ni zuri na litakufanya upige hela. That’s the TRAP. UTAFELI. Kabla ya kutumia muda wako mwingi VALIDATE your idea first. Fanya utafiti, Market research. Soma Uzi Huu hapa https://twitter.com/GillsaInt/status/1286330051655606273?s=20
Malengo yako ni kuanzisha biashara ambayo inaongeza thamani kwa watu. Haitakua namaana kama utakua na bidhaa ambayo hakuna mtu anahitaji. Kusanya maoni kutoka kwa watu/wateja wako walengwa tokea unaanza biashara na usiache kuwaskiliza.
Tengeneza detailed, measurable, and realistic goals. Ni ngumu kwenda popote kama hufahamu unakwenda wapi. Panga mipango yako ya siku, wiki, mwezi. Kisha panga mkakati jinsi gani jinsi utayafikia malengo yako.
Biashara ina mahitaji mengi ili ifanikiwe na wewe kwa sababu umeajiriwa huna muda wa kutosha kuyafikia mahitaji yote. Mfano unahitaji Social Media Makerting kwa biashara yako na wewe huna muda. Hio kazi mpe mtu mwingine. Focus kwenye vitu muhimu vinavyokuza biashara yako
Faida inayopatikana kwenye Side Business yako Re Invest kwenye biashara yako na kiasi kingine kinachopatikana SAVE itakusaidia pale ambapo utaamua kuacha kazi na kufanya biashara full time. Hakikisha umeweka mipango na bajeti ya jinsi utatumia hela zako.
ANGALIZO: Usitumie mali za kampuni/mwajiri wako kwa kazi zako binafsI. Usitume email, printer, laptop, etc. Hii ni pamoja na muda wa mwajiri wako usitumie kwa biashra zako.
Kuanzisha biashra ukiwa umeajiriwa sio kazi ndogo lakini INAWEZEKANA. Kuna njia nyingi za kua mjasiriamali hii ni moja wapo. #ElimikaWikiendi
You can follow @GillsaInt.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: