Wote tupo hapa Twitter tunafurahia hii "text broadcasting technology" iliyoanzishwa 2006

Twitter sasa hivi ina thamani ya $30B na CEO wake Jack Dorsey @jack ana utajiri wa $8.3B, lkn nyuma yake kuna;

STORY YA KWELI YA URAFIKI, MAMLAKA, PESA NA USALITI

It's time for Thread
Kuna mtu anaitwa Evan Williams @ev , mwaka 2003 aliwauzia @Google kampuni yake iitwayo @Blogger kwa $50M (TZS 115 bil)

Ktk kipindi cha transition Evan Alifanya kazi Google kwa mwaka mmoja hadi 2004

Baada ya Transition Evan akawa hajui nini afanye, akawa tu idle na hela zake
Kuna dogo m1 kichwa vibaya mno, aliDrop out chuo 2002 bcz aliona anapoteza muda, akawa anagonga codes kuunda tech yake. Anaitwa Noah Glass @noah

Mpk 2004 alikua na podcasting platform inayoweza kutuma ujumbe kwa mfumo wa sauti, akaiita @odeo lkn hakua na pesa ya kupush mzigo
Ikatokea coincidence Evan na Noah wakakutana, Evan ana mawe na Noah ana technology wakaungana kuwa partners wa Odeo

Evan pia alikuja Odeo na mshkaji wake wa dam dam kutoka Google anaitwa Biz Stone @biz huyu ni mchawi na nusu wa web designing pia alikua na mawe mingi
Odeo wakaanza kuajiri employee number 1 alikuwa Jack Dorsey @jack kipindi hiko kulikuwa na watu wachache sana watabe wa coding, Jack alikua mmoja wao

Team ya watu 8 ikakamilika, wakaanza kupush Odeo ije kuwa kitu kikubwa sana duniani, by that time walikua wapo ghetto la Evan
Odeo mambo yakawa matamu, kila kitu kinajipa wanajipanga kuTake Over the world wakakutana na msumari wa utosi;

Sept 2005 @Apple wakatoa iPod nano yenye @iTunes itakayokuwa na broadcasting platform km ilivyo kwa Odeo

Ndoto za Odeo zikafifia bcoz wasingeweza kushindana na Apple
Hii iliwakata sana japo hawakurudi nyuma, waliamini bado wana room ya kutusua

Noah Glass akaomba kustep down as CEO wa Odeo kwasababu alikua na migogoro ya kindoa na mkewe, Evan akachukua hiyo position

Evan akaomba kila mtu afikirie wazo linaloweza kuwanusuru km kampuni
Kazi ikawa 1 tu kuhakikisha Odeo inasurvive, kila mtu akawa anapasua kichwa kuja na idea, huku investors wa Odeo hawaelewi hatma yao

Ili kuja na best idea ilibidi watengeneze makundi ya kuBrainstorm. @jack na @noah wakawa kundi 1, hawa ndo walikua vipanga zaidi, wakawa washkaji
Siku 1 Jack akamgusia Noah idea kali sana ya 'status' ambapo unaweza kutuma text message 1 ikaenda kwa watu wengi ambao wapo ktk group 1

Idea ilikua haielewek vzr bcoz kipind hiko technology ilikua chini sna. Lkn Jack na Noah wakaipiga msasa hiyo idea mpk ikawa ikaanza kueleweka
Jan 2006 Jack na Noah wakaPresent idea kwa mara ya kwanza kwa watu wote ktk kampuni. Noah akafanya presentation kali na akasuggest iitwe twttr

CEO Evan hakuielewa,akamuomba Noah atulie na team yake waisuke vzr. KUMBUKA ni team ya @noah sio ya Jack, akaongezewa watu wa3 kwny team
Prototype & technology yote ya twttr ilikua ktk computer ya Noah @IBM Thinkpad. Mara kadhaa Jack alikua anakata tamaa na Twttr lkn Noah alikua km spiritual father anampush zaidi

Noah akatalakiana na mkewe, ilimkata sana akawa hata analose focus, lkn @jack akawa msaada mkubwa sn
March 2006 @jack kwa mara ya kwanza kbs akaTweet, hii ndio tweet ya kwanza kbs "Just setting up my twttr"

Kila mtu akaanza kuilewa idea, kila mtu yupo excited sn japo kulikua na changamoto 1, ndani ya Odeo kukawa na makundi ma2

-Kundi la Noah (twttr)
-Kundi la Evan (Odeo)
Noah akaomba kuwe na mgawanyo wa majukumu Odeo ijitegemee na Twttr ijitegemee ili kazi zifanyike kwa umakini, thou ownership ingebaki vile vile

Hii kitu ilimkera sn Evan kimoyo moyo, na Noah akawa km vile ni threat na competitor

Pia Jack aliona km vile Noah anamzibia nyota yake
Figisu zikaanza kumpiga chini NoahđŸ˜„. Evan akatuma barua kwa investors wa Odeo kuwa haoni km kampuni ina future tena, lazima wazame, ili kuwanusuru wasiendelee kula loss akaomba azinunue shares zao

Akanunua shares zote Odeo akawa ndio mwenye sauti zaidi ndani ya kampuni
Huku Noah anakomaa na depression, upweke wa kuachika, kampuni yake Odeo kubuma, his LAST HOPE ilikua ni twttr ndio kitu pekee kilichokua kinampa faraja

Akaona iwe makini kubadili twttr kuwa @Twitter na akadesign logo ya kwanza kbs, ikakubalika ndani ya kampuni
Hii ikaendelea kuwa threat kwa Jack ambae aliamini anazidiwa nyota na Noah japo initia idea ya Twitter ni yake

Kisirisiri akawa anapiga majungu Noah afukuzwe akitumia ishu ya depression ya ndoa km fimbo, akija kwa Noah anajifanya mwana
Jack Dorsey akamjaza ujinga Noah kwamba inabidi aombe leave hata ya miezi mi3 ili aende mapumzikoni akae vzr kisaikolojia kutokana na maseke ya ndoa yaliyomkuta

Noah akaona ni wazo zuri sana, akachukua leave ya muda mfupi akae vzr mentally
Maskini Noah Alivyorudi 2007 ndio ikawa mwisho wake, akafukuzwa ndani ya kampuni na Evan @ev akalipwa hela ndogo sn bcoz kampuni haikuwa na thaman

Jamaa akawa na depressions 4
1. Kampuni yake Odeo kubuma
2. Divorce
3. Kufukuzwa kwenye kampuni yake
4. Kusalitiwa na washkaji zake
Baada ya Noah kufukuzwa akamwita Jack ili ampe taarifa, Jack alionekana kusikitika sn hata kumwaga chozi kumbe kimsingi yy ndio alikua mbaya wa Noah

Noah alivyosepa Jack akawa CEO wa twitter akiwa na Evan na Biz km cofounders, Noah akarudi kijijini
Jack Dorsey akawa nguzo imara sana ndani ya Twitter, akaaminika sana na kupewa equity ya kutosha

Akawa na influence kubwa ndani na nje ya kampuni. Mwaka 2011 akam-interview rais wa US Barack Obama, fame yake ikaongeza mara dufu
Twitter wakaendelea kupush, ikaanza kuwa famous japo kulikuwa na competition kutoka kwa @Facebook , @burbn ambayo ss hv ni @instagram nk

Lkn twitter ikajiposition zaidi ktk news zaidi na mtandao wa governments mwaka Nov 2013 Twitter ikaenda public, I mean publicly trader company
Ndani ya masaa machache baada ya kuwa public Jack, Evan na Biz Stone wakawa Billionaires in USD.

Noah Glass hakua na chochote, hakuambulia hata jero.

Miezi miwili kabla Twitter haijaenda kuwa public maskini Noah alitweet hivi 👇
Sasa hivi CEO wa twitter Jack ana utajiri wa zaidi ya $8.3B, anaishi maisha ya anasa sana

Mwaka jana 2019 kajilipa mshahara $1.4 sawa na Sh 3,200

Anaishi nyumba ya thamani ya bil 23 TZS

Anafuga ndevu, ana kipini cha pua

Anamdate model wa Raven mwenye miaka 23
Mwaka jana Jack alisema atakuja Africa kutia kambi kwa zaidi ya miezi mi3

Ni mshkaji sana wa @elonmusk pia ni fan mkubwa wa cryptocurrencies kwenye bio yake kaandika #bitcoin

Ametoa almost 25% ya utajiri wake kwajili ya COVID crisis
Ktk 1 ya interview Jack aliwahi kusema "successful businessmen create enemies along the way" pia hatambui na hajawahi kuAcknowledge mchango wa Noah Glass ktk mafanikio ya Twitter

Noah huku akiwa kachoka vby twitter bio yake inasema "i started this"
Lessons:

1. Muhimu kuamini watu lkn pesa inapohusika TRUST WISELY

2. Hujui usaliti utatoka lini na kutoka kwa nani, lkn ukitokea KUBALI and move on. @noah alishindwa kukubali haraka

3. Baada ya kusalitiwa it's important to HEAL

4. Life is not fair, get used to it ~Bill Gates
You can follow @Sirjeff_D.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: