R.I.P DR. SHIKA😭
💔💔
#UZI
MFAHAMU JAPO KWA KIFUPI

👇👇👇
Dr. Shika alikuwa ni miongoni mwa wasomi wazuri lakini bahati mbaya elimu yake haijaweza kusaidia taifa hili achilia mbali kumsaidia yeye binafsi.
Makampuni ya kibiashara yalitumia umaarufu wake kama fursa ya matangazo lakini yakamuacha hohehahe asiye hata na mahali rasmi pa kuishi. Aliwahi kuripotiwa na kituo kimoja cha TV kufukuzwa kwenye nyumba aliyokua akiishi huko Tabata baada ya kushindwa kulipia kodi.
Wengi walimchukulia kimzaha tangu alipoonekana kwenye tukio la mnada wa nyumba za Lugumi (mia tisa itapendeza).
Vyombo vingi vya habari vilikuwa vikimdhihaki na vingine kumuita Kalubandika. Lakini bila shaka vilifanya hivyo pasipo kumjua kiundani Dr.Shika.
Ni mzaliwa wa kijiji cha Kalemela wilaya ya Busega, mkoani Simiyu. Majina yake halisi ni Louis Shika Kidola. Yeye na ndugu yake Jeremiah Shika Kidola (marehemu pia) walikuwa wanafunzi wenye akili sana na waliofaulu vizuri masomo yao ya sekondari kwa alama za juu na kupata
ufadhili wa kusoma udaktari nchini Urusi mwaka 1984 hadi 1991 waliporejea na kuanza kutibu hospitali ya taifa Muhimbili.
Mwaka 1994 Louis Shika alirejea Urusi kujiendeleza kimasomo. Alisomea shahada ya uzamili katika magonjwa ya kuambukiza (MSc in Infectious Diseases)
na udaktari bingwa wa magonjwa ya akili Master of Medicine (Psychiatry).

Akiwa huko alishirikiana na wenzake kuanzisha kampuni ya usambazaji wa kemikali viwandani iitwayo Lancefort Ltd. Kwa sasa ni moja ya makampuni makubwa ya usambazaji wa kemikali nchini Urusi,
na jina la Dr.Shika lipo kwenye website yao kama Muasisi na Rais wa kwanza wa kampuni.

Inadaiwa shirika la ujasusi la Urusi (KGB) liligundua kwamba akina Shika walipata fedha za kuanzisha kampuni kutoka Marekani kama mkakati wa Marekani kudukua taarifa za Urusi.
Kwahiyo baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo walikamatwa. Dr.Shika alitekwa na watu waliodhaniwa kuwa majambazi na kupewa mateso makali sana ikiwemo kukatwa vidole.
Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Urusi, Patrick Chokala mwaka 2017 alnukuliwa na vyombo vya habari kwamba ilbidi kutumia mbinu za "kijasusi" kumnasua Dr.Shika na kumrudisha nchini kwa dharura. Tangu aliporejea alijiingiza kwenye ulevi wa kupindukia kutokana na msongo wa mawazo
Kwahiyo ukifuatilia historia ya *Marehemu Dr.Shika* utagundua hakuwa "kalubandika" kama ilivyodhaniwa. Ni mtu aliyekua na maono makubwa. Kama si mipango yake kuvurugika huenda angekuwa daktari bingwa na mfanyabiashara mkubwa wa kemikali duniani.
Ni kwamba tu alijikwaa, akadondoka na hakuweza kusimama tena. Serikali ilipaswa kumsaidia kusimama lakini nayo ilimtelekeza. Kwahiyo ameishi maisha ya upweke, masononeko na msongo wa mawazo kwa muda mrefu.
Kampuni aliyoanzisha ya Lancefort Ltd ambayo kwa sasa inamilikiwa na serikali ya Urusi (ilitaifishwa) ina thamani ya $27Bil sawa na TZS 60Trilioni (Bajeti ya nchi kwa miaka miwili).
_
Kwa hiyo Dr.Shika alikuwa anajiita "Bilionea" si kwamba alikuwa anaota. He used to have money.
Na hiki ndicho kilichokuwa kinamtesa maana alishindwa kukubaliana na hali yake ya sasa. Hakutaka kuamini kama aliwahi kuwa na pesa.
Kujikwaa na kuanguka ni kawaida katika maisha lakini jambo la msingi ni uwezo wa kusimama tena baada ya kuanguka.
Whinston Churchil aliwahi kusema "Success is not final and failure is not fatal. It is the courage to continue that counts"
Mtu kama huyo hakuwa mtu wa "kumchukulia poa" hata kidogo. Serikali haikutakiwa kumtelekeza. Alipaswa kupewa nafasi nyingine.
Either angerudishwa Muhimbili kutibu au angetafutiwa fursa mahali pengine ambapo taifa lingeweza kufaidi ujuzi wake na pia ingekua njia ya kumsaidia kuondokana na msongo wa mawazo na kusahau "mabilioni" yake kule Urusi.
*Pumzika kwa amani Mr. mia tisa itapendeza*
👇🏾👇🏾👇🏾
⤵️⤵️⤵️
*World Stories Whatsap 0623782805*
You can follow @biturojr.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: