Ushawahi kutapeliwa? Mimi nimetapeliwa Tsh milioni kumi (10m) na rafiki yangu wa karibu, (best friend) rafiki ambaye mpaka familia zinajuana. Ila 10m ikafanya urafiki, ushoga na udugu ukafa moja kwa moja. Ilikuwa hivi, Shoga alinunua gari ya kubeba mafuta na kuanza biashara.
Biashara yake ni kununua mafuta depo na kusambaza. Akaniomba niwekeze kwenye biashara yake mana ana upungufu wa pesa ya kuzungusha, tukakubaliana kila mwezi atanipa faida ya mtaji wangu 10% ambayo ni 1m. Na nikitaka pesa zangu nimpe notice ya mwezi 1. Nikaona ni jambo jema.
Badala ya kudunduliza kuweka akiba benki ngojea nimpe shoga, nami nipate tufaida. Nikampa 10m kash. Tulikubaliana tutaandikishana kwa lawyer ila makaratasi hayakuja. Mwezi wa kwanza nikatumiwa 1m fresh, mwezi wa pili mpaka nikakumbusha, nikatumiwa nusu nusu.
Nikaja kujua kuwa amechukua pesa kwa rafiki yetu mwingine kwa dizaini hiyo, ila sikumuuliza. Siku moja kwenye mazungumzo, akajisahau akasema sasa hana stress mana gari kawakodisha watengeneza barabara, yeye wanamlipa tu kwa kutumia gari yake. Nikamwambia, ni vema anirudishie pesa
Hapo ndio shida ilipoanza, miezi kama minne hivi tunadaiana, nikashikwa na hasira nikamwambia ntampeleka polisi. Hamadiiii naletewa barua ya mwanasheria kuwa niache kumsumbua na kumtisha mteja wake. Jema ni kuwa barua ya mwanasheria wake ilikiri kuwa niwekeza hela kwa makubaliano
Kiukweli nilipata ghadabu kubwa mno, nikapata mwanasheria akajibu barua. Swala likafika kwenye familia. Kaka yake akaahidi kuwa nitalipwa. Kutoka october 2018 mpaka leo sijalipwa hata mia. Na si kuwa hawana hela wana mashule ya nursery mpaka college, basi tu, dhulma.
Nikataka kufungua kesi, mama na baba Mishy wakanisomea risala ndefuuuuuuuuu. Nakumbuka mama aliniambia, kama familia yake wamemuacha rafiki yako akufanyie ubaya sisi wazazi wako hatukuruhusu umlipe mwenzio ubaya, ulinde uungwana wetu Samehe. Mungu akatajwa kama mara alfu...hapo
Jana usiku, kuna mtu alikuwa analalamika katapeliwa kikombe (mug) na alikuwa determine kupata haki yake, ikanifanya nikumbuke madhila yangu, nikiri, kahoro bado kanauma - 10m parefu jamaniiii. Nikaona japo niandike kuwakumbusha msirudie kufanya ujinga niliofanya. Nimejifunza mnoo
You can follow @MSalimu.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: