Central Party Office #6
.
Kikosi maalumu ndani ya CHAMA na SERIKALI ya Korea Kaskazini chini ya familia ya KIM JONG-UN kwa zaidi ya nusu Karne. Huteuliwa kutoka kwenye Jeshi la watu wa KOREA (KPA), kisha hupikwa upya. Wengi wao ni ndugu wa karibu wa RAIS.
.
thread - uzi🧵
Anapokuwa nyumbani kwao Pyongyang, Korea Kaskazini; Kim Jong-Un analindwa na walinzi wa aina tatu wanaokuwa wamemzunguka, gari yake husindikizwa na gari nyingine pamoja na pikipiki. Lakini mambo yalikuwa tofauti wakati wa mikutano miwili mikubwa aliyofanya na Rais wa Marekani...
...Donald Trump kule Singapore na Hanoi. Ikiwa ndio mkutano wa kwanza kati ya Kiongozi wa Korea Kaskazini na Marekani kwa miongo kadhaa, mwaka 2018 akiwa Singapore, Kim aliwasili kwenye ukumbi wa mikutano akiwa ndani ya Benz nyeusi iliyozungukwa na vijana waliovalia suti...
...wakikimbia kulinda gari iliyombeba kiongozi huyo. Jambo hilo lilikuwa la kushangaza na kuvutia ila kutokana na usiri wa serikali ya Korea Kaskazini hakuna mtu aliyekuwa anajua kwa undani kuwa vijana wale ni kina nani isipokuwa kila mtu aliyeshuhudia tukio lile alitambua...
...fika kuwa wale ni walinzi. Hivyo ilibidi wachunguzi wa mambo ya kisiasa na wasomi kujaribu kufanya uchunguzi ambao baadae ulibaini baadhi ya mambo kuwahusu vijana hao;
.
Ni vijana kutoka kwenye kikosi kinachofahamika kama "Central party Office #6" yaani...
..."Ofisi Kuu ya Chama Namba 6" ni wao pekee wanaruhusiwa kukaa karibu na Kim anapokua hadharani. Vijana hawa wanateuliwa moja kwa moja kutoka kwenye Jeshi la watu wa Korea mara tu baada ya kumaliza mafunzo ya kijeshi. Kuna sifa nyingi zinazoambatana na uteuzi huu ikiwemo...
...Urefu; ni lazima askari anayeteuliwa awe na urefu sawa au unaokaribiana na Kim, sifa nyingine ni Macho; askari ili ateuliwe ni lazima awe na macho yanayofanya kazi sawasawa na ili uteuliwe lazima uwe na uwezo wa kipekee kwenye kitu fulani; kwa mfano kulenga shabaha, ngumi, ...
...Karate n.k. Baada ya uteuzi, askari wateule wanapitia kwenye uchunguzi wa hali ya juu kuwahusu wao na familia zao vizazi vitatu nyuma. Kazi hii ngumu inarahisishwa kwa kuteua askari ambao wana uhusiano wa kindugu na Rais au familia za watu mashuhuri nchini Korea Kaskazini...
...Askari atakaye fanikiwa kupita kwenye mchujo wa uchunguzi haruhusiwi kukataa kujiunga na kikosi. Baada ya uchunguzi askari wanapelekwa kambini kupata mafunzo ya hali ya juu ya kijeshi, mafunzo ambayo yanafanana kwa kiasi kikubwa na yale wanayopewa makomandoo wa KPA...
...Ikiwemo mafunzo ya kutumia silaha za aina mbalimbali, kulenga shabaha, ngumi na karate na mafunzo ya uvamizi. Wakati wote wa mafunzo askari anafuzwa kuwa shupavu na mkakamavu wa mwili na akili, uzalendo ndio msingi mkuu wa mafunzo yao...
...Wakati wote Kim anapokuwa hadharani, askari hawa wanatengeneza pembe tatu kumzunguka, ili kuhakikisha wanapambana na hatari yoyote itakayokuja upande wake. Mbele kabisa ya msafara huo anatangulia mkurugenzi mkuu wa kikosi hicho na wote wanakuwa wamebeba silaha za moto...
...Wanapendelea kuvaa suti za rangi nyeusi, shati jeupe na tai. Pia wanavaa waya maalumu wa mawasiliano ya redio masikioni kwaajili ya kuwasiliana wao kwa wao. Kifuani wanavaa nembo ya kikosi chao ili waweze kutambuana na pia wanafanya mawasiliano kwa...
...lugha ya siri ambayo wanaelewana wao tu. Central Party Office #6 ina askari kati ya 200 - 300, nusu yao ni walinzi na wengine ni madereva pamoja na wataalamu wa mitambo. Tofauti na taaluma nyingine au walinzi wa viongozi wengine wakubwa dunia...
...askari wa kikosi hichi wanafanya kazi kwa miaka 10 tu kisha wanastaafu.

'MWISHO
You can follow @tweetsrifle.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: