SIO KILA ANAEKUOMBA NAMBA YAKO ONLINE NI WA KUMPATIA, JIFUNZE KUPITIA STORY YANGU
Hakuna kitu kinanitisha hapa Twittemorning kama mtu kuomba Namba yangu ya simu, Sijui namba yangu ya WhatsApp. NAOGOPA!
Kuna kitu nyuma ya uoga wangu...
UZI
Hakuna kitu kinanitisha hapa Twittemorning kama mtu kuomba Namba yangu ya simu, Sijui namba yangu ya WhatsApp. NAOGOPA!
Kuna kitu nyuma ya uoga wangu...


Mwanzo kabisa nilikua miongoni mwa watu wengi ambao tunapenda kuwa connected na Watanzania wengine tukiamini kadri tunavyojiweka karibu nao ndio tunavyozidi kuwin nafasi za karibu katika maisha yao...Wengi wenu hata leo mnaamini hapa na mmekua mkitoa namba zenu kwa watu online
Kwanza unatakiwa ufahamu kuwa mtu anapoipata namba yako anakua na uwezo wa kupata taarifa zako binafsi kama vile...Majina yako kamili, wapi ulizaliwa wapi unaishi, Jirani yako ni nani na ndugu zako ni kina nani wapi unafanya kazi au wapi unasoma. Pia kupitia namba yako hiyo hiyo
Mwaka 2016 kipindi iko ndio naanza kufahamu uwepo wa Instagram nilikua miongoni mwa watu ambao tulifanikiwa kuwa na page zilizokua na wafuasi wengi...nakumbuka nilifikia watu 40k...ni wachache lakini kwa kipindi cha mwaka ule hiyo ilikua sio kazi ndogo sasa to kip the story short
Mwaka 2018 kupitia Account yangu hiyo hiyo ya Telegram niliyokua napost video mbali mbali nilifanikiwa kukutana na jamaa mmoja anaitwa Ibra (jina la kutunga tu), Jamaa alinicheki DM kutokana na alivyojielezea alidai kwamba angetamani
Angetamani sana kama angeweza na yeye kuwa na page yenye wingi wa followers kama ilivyo ile yangu...na kutokana na the way jamaa alivyojitambulisha kwangu ilinifanya niamini ni moja ya watu wanaoAppreciate uwepo wangu pale Insta,
Baadae mazoea yakazidi mimi na Ibra, tukafikia kuwa washkaji kabisa nikawa na namba yake nae ana namba yangu. Hapa mawasiliano yetu mengi sana yakawa sasa kupitia Normal text nakumbuka enzi hizo Ukijiunga sms unakazania uchat mpk uhakikishe umemaliza zote....
Basi bwana mzee Ibra akawa mwanangu sana, tukaanza kupeana madili (Hapa mimi ndo niliekua napewa madili sasa maana jamaa ndo alikua mshua halafu mimi ile kawaida tu). Yani chattings zetu zilikua mostly ni ishu za mitandaoni na udaku.
Ikatokea siku moja ilikua ni Sikukuu ya Saba saba sile yani siwezi sahau kabisa iyo siku, Mwana tulikubaliana tukutane Saba saba pale...kipindi iko nakaa mbagala kwa kuwa mchizi yeye alipokua anaishi ni Masaki kule basi tukakubaliana yeye ndo aanze kutoka
Aanza kutoka home, then akifika karibu na maeneo anistue na mimi nipande chap tu...si unajua kutoka mbagala hapo Mbagala hapo Kizuiani sio mbali na viwanja vya sabasaba wala nini... Baada ya jamaa kufika maeneo ya karibu akanistua ndip nikaanza kutoka pale
Ile siku nakumbuka nimefika saba saba pale ila mpaka saa 12 kigiza kinaanza kuingia jamaa simu yake napiga haipokelewi na mimi simu yangu imeisha chaji hapo...Enzi hizo nina NOKIA button si unajua tena betri ikiisha ukitoa ukilamba chaji inarudi yakutosha kuwasha simu

Basi kama waswahili wanvyosemaga “Siku ya kutembea uchi ndo unakutana na mkweo” ile siku nimetoka home sikuzingatia kujaza simu full wala nini so wakati nimeshuka na dala dala pale Sabasaba chaji yote ikaishia kwenye kumtext jamaa kumjulisha nimefika uko pande zp?
Nilituma sms mbili nakumbuka, Sio kwamba sikuwa na dakika ila sikuwa na jeuri ya kujiunga dakika
. Hiyo pesa sikuwa nayo ya kuchezea, Baada ya kutuma text mbili tu nimekaa kaa nawait kimeo changu kikazima na chaji kabisa....

Ishu ikawa kwamba siwezi tena kupata na jamaa...mda ukasogea, kijua kikazidi kuhama mzee mwishoni kikaanza kuzamia. huko kigiza kinaingia....Sikuwa na changu tena nikadandia DSM chap chap mpaka Mbagala....Mbagala nikachukua Dala dala mpaka Kizuiani mzee...
Kitendo cha kufika tu home nikaenda kuweka simu chaji nikaiwashia hapo hapo zikaanza kuingia Simu sasaa...Ikapigwa namba ya kwanza ikaskika sauti ya mzee...sauti nzito...nikapokea ile napokea tu simu nakutana na swali naulizwa uko wapi? Sikuweza kujibu swali la mtu no ngeni
So ikawa sasa kila simu inayokuja naipuuuza ila baadae zikanza kutumwa text ndo nikaja kutumiwa text na Mmama ambae alijitambulisha kama Shangazi yake na Ibra, Ibra kuna tatizo limemkuta na namba ya mtu wa mwisho kuwasiliana nayo inaonesha ni mimi....
Kabla hatujaendelea na story kwanza naona kuna sehemu nimekosea kule juu pale Sio Telegram ni Instagram...Keyboard ime Auto Correct tu ila Telegram haihusiki hapo ni Telegram. Ni Instagram
Enewei tusonge sasa...basi mzee wenu nikafatwa home siku ya pili yake na yule mwanamke shangazi yake Ibra na Maafande Watatu wamekuja na Taxi...
Kufika na kufika tu wakanipiga pingu 
. Kote miguuni na mikononi wakati huo nashangaa story niliyopewa kwamba Ibra amefariki dunia na kutokana na kwamba wa mwisho kuwasiliana nae ni mimi basi lazima wanichukue niende nao...


Ima kutokana na ubishi niliouonesha kuanzia kujitaja mwenyewe kwamba nipo wapi, na pia kuonesha resistance kwa maafande basi ilibidi wanipige pingu...nikafikishwa mpaka Police station iyo ilikua Ijumaa mzee
Na unajua sheria za bongo zilivyo za kikuda ukiingia polisi Ijumaa utalala kutoka Jumatatu. Mwananenu ikabidi nilale rumande siku 2 mfululizo 


Lakini mule ndani pale polisi waliponiweka nilikua karibu sana na Afande mmoja hivi wa kike. Kwa jinsi navyokumbuka pale ndani niliskia maafande wenzie wakimuita Afande “GRACE” so tumuite hivyo hivyo
Unajua tena ile Huruma wanawake hukuaga nayo nikatokea kuzoeana sana na yule dada baada tu ya siku moja ya kuwa pale ndani.
Mazoea yakawa mengi mimi na Afande Grace, yule afande ana kafiga flani hivi...weupe wa kichaga ule
Mazoea yakawa mengi mimi na Afande Grace, yule afande ana kafiga flani hivi...weupe wa kichaga ule
Sasa nakumbua siku ya Jumamosi wakati wa mchana baada ya Lunch sijui tuseme chakula cha mchana afande Grace akaniita kwenye ofisi ya pembeni humo tukawa mimi na ye ya tu wawili nyie yule dada 




Sasa mule kwenye ile ofisi palikua na limeza limoia hivi chakavu chakavu...me nilikuwa nimeketi kwenye kiti Afande Grace amekaa juu la lile limeza chakavu so kinamna flani nikawa nayaona live kabisa bila chenga mapaya yake mazuri yaliyopendezeshwa na rangi ya arabuni
Wanangu halafu mimi kipindi iko sasa si ndio niko ile Adolescence period hapo na haijaisha isha na dryspell kinoma noma...Ghafla sijui nikatolea wapi nguvu za kumtouch mapaja yule Afande....
Afande nimemtouch kama utani tu nimetest zari oyaa si akajibu mapigo unaambiwa akanivuta halafu akanisukumia tena kwenye kiti PAAAAP!! Nikarudi kukaa tena juu ya kile kiti Afande akaanza kunifuata kimiss unaambiwa... Hapo

Kimiss...misssss unaambiwa anatembea kama yule Miss Lindi mnamuitaga Grace Mella sasa yule Afande akawa anatembea namja iyo yani ananijia hivi...Nikajiongeza haraka haraka nikatoa Tshirt niliyovaa juu chap, kwa haraka nikabaki kitumbo wazi
Wakati huo Afande Grace anakuja kwa madaha...ananisogelea nikaona ili asipate tabu akifika nikashusha na nguo ya chini nakumbuka nilivaa surui flani hivi wanaitaga Venta hazinaga Lux so haikua na mkanda nikavuaaa...nikamwaga radhi hapo
Afande akafika akanirukia dizaini kama vile anataka kuua nyoka kwa kumkalia...Akaja kama ananitulia mapajani ili anikalie...PAAAAH
Kanikalia PAAAH nikastuka kutoka usingizini kumbe nilikua naota wakati nimelala Hostel pale Ubungo. S
Kanikalia PAAAH nikastuka kutoka usingizini kumbe nilikua naota wakati nimelala Hostel pale Ubungo. S
Ila main point ni Msitoe toe namba zenu za simu kwa watu huku Mitandaoni. Watu sip watu wengi miyayusho tu. Sawa wapwaaa?? Tumeelewana hapo. Usisahau kunifollow sasa
