#UZI TEKNOLOJIA NA AFYA YA AKILI (kwa hisani ya @simonsinek)

"Tunakua kwenye dunia ya Facebook na Instagram. Kwa maneno mengine, tupo viziri kwenye kuweka FILTERS kwenye vitu. Tupo vizuri kuonyesha watu kuwa maisha yetu ni mazuri, ilhali kiuhalisia tuna sonona"
#DaktariMwandishi
"Mtandaoni kila mtu yupo TOUGH, kila mtu anaonekana ameyapatia maisha. Ila kiukweli, ni wachache sana wapo TOUGH na wengi bado hawajayapatia maisha. Kwahiyo tuna kizazi kinachokosa kujiamini kuliko vizazi vilivyopita.

Tunajua unapotumia simu na mitandao ya kijamii, ubongo wetu"
"hutoa kemikali ya DOPAMINE, ndio maana unapopokea text, unajisikia vizuri.
Au unapojisikia mpweke, unatuma text kwa marafiki kama 10 kuwasalimu, kwasababu unajisikia vizuri unapopata jibu.
Ndio maana tunahesabu LIKES, FOLLOWERS, RTs na unarudi kutazama post yako ina likes ngapi"
"Ndio maana unaumia mtu anapokufollow au kukublock.
Kwasababu tunafahamu hivi vitu vinakupa DOPAMINE ambayo inakufanya ujisikie vizuri.
Dopamine ndio kemikali inayokufanya ujisikie raha unapovuta sigara, bangi, kunywa pombe na unapocheza upatu/unapobet.
Kwa maneno mengine, hii"
"kemikali ina URAIBU(addiction) mkubwa.
Tuna makatazo ya kiumri kwenye kuvuta sigara, kunywa pombe na kubet lakini hatuna makatazo hayo kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii au simu.
Kwahiyo tuna vizazi vilivyo na access na kemikali hii ambayo ina uraibu kupitia mitandao."
"Karibu kila mtumiaji wa pombe, alijifunza akiwa kijana balehe(teenager).
Tukiwa wadogo, tunahitaji kukubalika na wazazi, tunapoingia kwenye ujana balehe, tunahitaji kukubalika na kundi rika zaidi kuliko wazazi.
Katika kipindi hiki tunajifunza kuwategemea marafiki zetu."
"Ili kuhimili stress za kipindi hiki, ndio watu hugundua vilevi ili kukubalika. Hii inakuwa wired kwenye ubongo, hivyo kwa maisha yao yote, wakipata stress, hawatamgeukia mtu, watageukia kilevi.
Vivyo hivyo kwa mitandao. Kinachotokea ni hawa vijana wanapokua, wanashindwa "
"kutengeneza urafiki wa kufa na kufaana. Ukiwauliza vijana sasa, watakiri kuwa marafiki zao wengi ni rafiki-jina, kuwa hawawategemei rafiki zao kwenye shida ingawa wanastarehe nao.
Kwasababu wameshazoea mitandao, wakiwa na shida hawageukii rafiki, wanageukia mtandao."
"Pombe sio mbaya, ila pombe kupita kiasi ndio mbaya.
Kubet sio vibaya, kubet kupita kiasi ni tatizo.
Hakuna tatizo kwenye simu na mitandao ya kijamii, tatizo ni kutokuwa na balance ya matumizi.
Kama umeketi na rafiki zako na upo bize kutext mtu asiye hapo, ni tatizo. Una URAIBU."
"Kama.umeketi kwenye kikao, na umeweka simu yako mezani, haijalishi kama umeigeuza juu au chini, hiyo inatuma ujumbe kwa wale ulionao kuwa wao sio muhimu kama hao unaoongea nao kwenye simu.
Kama unaamka unaangalia simu kabla hujasalimiana na mwenzi wako pembeni yako, una URAIBU."
"Na kama ilivyo kwa URAIBU mwingine, baada ya muda utakuharibia mahusiano na watu, itakugharimu muda na pesa na kuharibu maisha yako.
Ongeza ukosefu wa uvumilivu ktk kizazi hiki. Kizazi kilichokulia ktk dunia ya kuridhika papo kwa hapo. Kipindi ambacho unaweka oda ya bidhaa"
"mtandaoni na inafika siku hiyo hiyo(hakuna kusagula), ukitaka kuangalia movie, huhitaji kwenda kuazima mkanda, unalog in Neflix unanagalia. Kama ni series unaangalia episodes zote mtandaoni, huhitaji kusubiri episode moja kila siku kwenye Tv.
Hata ukitaka kuanzisha mahusiano,"
"huhitaji kukutana na mtu kwanza uanzishe maongezi, ujikanyagekanyage, sasa hivi dating apps zipo kibao, (au unazama tu DM unafunguka, mahusiano yanaanza juu kwa juu)kwahiyo hujifunzi namna ya kustahimili mahusiano ya kijamii na watu
Karibu kila kitu unakitaka, unapata papohapo"
"Isipokuwa hii kuridhika papo hapo huwezi kuipata kwenye KURIDHIKA NA KAZI & UIMARA WA MAHUSIANO, hivi havina App.
Ni process ambazo ni SLOW, zinachosha, zinahitaji uvumilivu, ustahimilivu na si rahisi.
Kwahiyo unakutana na vijana wadogo, walioanza kazi au mahusiano tu na tayari"
"ukiwauliza wanaonaje kazi/mahusiano yao, wanasema wapo tayari kuacha kazi/kuvunja mahusiano kwani wanaona hawapati mafanikio haraka kama walivyotegemea.
Ni kama vile wamesimama chini ya mlima, kilele ni MAFANIKIO, ila hawaoni wala kupanda huo mlima lkn wanataka kufika kileleni."
"Kwahiyo kitu ambacho kizazi hiki kinatakiwa kujifunza ni USTAHIMILIVU. Kuwa baadhi ya vitu MUHIMU sana maishani kama MAPENZI, FURAHA, KURIDHIKA NA KAZI, KUJIAMINI, STADI ZA MAISHA ni vitu vinavyochukua MUDA kupatikana.
Utapata vipande vipande kila siku lkn safari yake ni NGUMU "
"Na bila kuomba msaada na kujifunza ustahimilivu, utaanguka kwenye mlima na hutafika kileleni.
Ndio maana unaona ongezeko la matukio ya kujiua, sonona na matumizi ya vilevi.
Au ndio unakuta mtu anaishi maisha yote lkn hapati furaha ya maisha kabisa, (kama msukule au zombie tu)"
"Unamuuliza mtu vipi kazi yako, anajibu KAWAIDA TU. Au unamuuliza vipi mahusiano yako, anasema AAAH HIVYO HIVYO TUNAKOMAA.
Hajaridhika na chochote hapo, ila basi tu atafanyaje.
Hatuna budi kujenga mahusiano na watu wanaotuzunguka, kusalimiana, kusaidiana na kujenga kuaminiana."
"Simu zisiruhusiwe kwenye meza za mikutano.
Mnapotoka na rafiki zenu, wekeni simu pembeni, pigeni picha halafu ketini ongeeni mjenge urafiki, muenjoy wakati uliopo.
Hivyo ndivyo ubunifu hutokea.
Usichaji simu yako pembeni ya kitanda, ichaji mbali kabisa.
Nunua saa, weka alarm"
"Usitumie simu yako kama alarm.
Ili ujenge uwiano na BALANCE kati ya MAISHA na TEKNOLOJIA.
Ujenge mahusiano ya kweli na unaowazunguka."

Hakuna kitu kinachoumiza na kukwaza kama unaongea na mtu, yeye yupo bize na simu. Upo na mwenzi wako, macho yapo kwenye simu. Inaleta walakini
inaleta wivu na ni dalili ya dharau.
Inamaanisha, unajali hicho kilichopo kwenye simu kuliko huyo aliye pembeni yako.
Ndio maana unajisikia vibaya unaongea na watu wapo bize na simu zao.
Mwisho, huyaishi maisha kwasababu jicho lako limeganda kwenye SCREEN ya SIMU.
Unapoteza watu
nafasi, stadi na mahusiano muhimu kwasababu jicho umegandisha kwenye simu.
Siku unapotoa hilo jicho ili utazame jicho la huyo mwenzi wako, utakuta jicho lake linatazama jicho la mwingine.
URAIBU wa Teknolojia unatupotezea vingi kwenye mahusiano yetu kijamii.
#DaktariMwandishi đź‘Ł
@threadreaderapp unroll please
Halafu hili kundi la vijana, linatoka hapo lina uraibu na simu na mitandao ya kijamii, hawana uwezo wa kujenga mahusiano na watu then wanaingia makazini na shuleni ambapo wanafundishwa USHINDANI. Hii inawaongezea kujitenga na wenzao kwasababu kila saa wanataka kuwa BETTER kuliko
wenzao. Kama unashindana na mtu, ni ngumu sana kuwa na mahusiano ya ukaribu na urafiki wa kweli na yeye.
Kwao hawa vijana kila kitu ni VITA, ni USHINDANI, ni kuonyesha NANI NI ZAIDI.
Hawajui kushirikiana.
Wanafurahia wasiowajua mitandaoni lkn hawana mahusiano na wale wanaoshinda
nao kila siku mtaani, majumbani na shuleni.
Kwahiyo tunajenga jamii ambayo ina U-MIMI, UBINAFSI na ina imani potofu ya kupima mafanikio kwa kile wakionacho kwa wenzao.
Vijana wenye chuki, EGO na kutojiamini au kujiamini kupita kiasi.
TUTAFAKARI!
#DaktariMwandishi
You can follow @Kudu_ze_Kudu.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: