PABLO ESCOBAR MUUZA MADAWA YA KULEVYA ALIYEITESA DUNIA KUTOKA COLOMBIA
——————————————
•Alikuwa msambazaji wa dawa za kulevya duniani kote
•Alichoma zadi ya US dola milion 2 sababu ni ——
• Hakuwahi kukamtwa mpka alipojisalimisha! Kwann!?
•Alikuwa na ndoto ya kuwa Rais
Uzi👇👇
Pablo Escobar maarufu km Don Pablo, El Patron, Sir Pablo alizaliwa huko Rionegro Colombia mnamo tarehe 1 Dec 1949! Akiwa mdogo kabisa Pablo Escobar alianza kuonesha ukorofi na kujihusisha na uhalifu
Baba yake alikuwa mwalimu na mkulima na alipenda mwanae awe na maadili mema
Pablo Escobar alioa binti mrembo aliyeitwa Maria Victoria Henae mnamo mwaka 1976 na kubahatika kupata watoto wawili Manuel Escobar na Sebastian Marroquin.

Aliishi vema na mke wake na watoto huku akiwapenda vibaya mno na kuwatunza! Alikuwa na utajiri sana katika maisha yake.
Pablo Escobar alijenga kasiri la kifahari alilojipa jina la Hacienda Napoles likiwa ni heshima ya Jiji la Naples lililopo Italy
Kasiri la Don Pablo lilikuwa la thamani ya dola milion 63 likiwa kwenye eneo la ukubwa wa ekari Elfu 7000! Ndani jumba hili ama kasiri la Don Pablo
Kulikuwa na uwanja wa mpira, tenis na Golf! Pia kulikuwa na swiming pool, uwanja wa ndege binafsi, magari ya kifahari, uwanja wa ng’ombe kupigana na zoo ya wanyama tofauti kama tembo, mbuni, pundamilia, ngamia, twiga na viboko! Pia kulikuwa na ziwa la kutengenezwa kubwa kabisa
Alimiliki magari mazuri ya kifahari na ndege za binafsi ambazo alitumia kusafirishia dawa za kulevya.
Party ama sherehe kwa Don Pablo ilikuw ni kitu cha kawaid kwani kila mara alionekana akila bata na warembo na watoto wake kwenye visiwa huku akiambatana na ulinzi mkali
Don Pablo alipendawa na wananchi wa Colombia vibaya mno!

Licha ya unyama aliofanya na kuuza dawa za kulevya Don Pablo alipendawa kiasi cha kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kiti cha Senators kwenye baraza la Congress mwaka 1982!
Pia alijenga shule, viwanja na nyumba za masikini kiasi
cha kuitwa “Robin Hood” na alifadhili vilabu mbalimbali vya timu ktk nchi ya Columbia

Aliwahi kumuita Maradona kwenye kasiri lake na kumlipa mamilion ya dola ili tu acheze nae mpira huku Maradona akikiri kuwa alikutana na walimbwende wengi waliokuwa kwenye kasiri la Don Pablo
Don Pablo aliwahi kuomba serikali imruhusu aisaidie kulipa deni la US dola bilion 10 ambalo nchi ilikuwa inadawa! Jambo hili lilizua mjadala sana kitaifa na kimataifa!

Mataifa km USA na Brazil yaliilaumu Colombia kuwa inamfuga DonPablo mpka anaingilia mambo ya ndani ya serikal
Don Pablo aliua zaidi ya watu 4000
Inashangaza kidogo lakin ndio ukweli inasadikika kuwa Don Pablo aliwaua wote waliojaribu kukwamisha biashara, akiwemo waziri wa kupambana na madawa ya kulevya, maafisa wa polisi na wanajeshi kadhaa! Muda wote alitembea na bastola ya kisasa
huku akitumia msemo wake wa “Plata o Plomo” akimaanisha “Rushwa au Shaba” yaani ukija kwenye anga zake ukubali kupokea rushwa ama basi utakula shaba!

Japo jamaa alipiga biashara ya kuuza dawa kwa muda mrefu lakin hakuwahi kukamatwa kizembe! Alitafutwa na polisi, inteligensia
na interpol wa USA kwa zaidi ya miaka kumi bila kukamatwa! Alikuwa anajificha sana na kufanya mambo yake kwa siri na ikiwa moja ya mshirika wake angeonekana kuvujisha taarifa basi risasi ingemhusu!
Mwaka 1989 Don alihusishwa na kudungua ndege kwa bomu iliyokuwa imebeba maafisa
wajuu wa serikali waliokuwa na taarifa muhimu za kufanikisha kukamatwa kwake ambapo katika udunguaji huo zaidi ya watu 100 walipoteza maisha! Kitendo hiki kiliiudhi sana polisi ya Columbia na jumuiya ya Interpol kimataifa huku wakitaka nguvu zaidi iongezwe ili Don Pablo akamatwe
Mwanzoni kabisa Pablo Escobar alifanya kazi ya wizi wa magari ambapo haikuchukua muda mwaka 1974 alitiwa korokoroni na maafisa wa polisi na kufanikiwa kutoka!
Baada ya kuona biashara ya kuiba magari haimlipi Pablo aliamua sasa kuanza kuuza dawa za kulevya duniani kote na kuunda
kundi lake lililoitwa Medellín Cartel ambalo yeye na binam yake ndo walikuwa wakuu huku wakipata wasambazaji duniani kote!

Dawa za kulevya zilizouzwa na Medellín Cartel ni kama Cocaine, Heroini, bangi na Mchanganyiko wa dawa zingine! Medellín Cartel ilisambaza zaidi ya 80% ya
dawa zote za kulevya duniani! Nchi kma USA, Mexico, Brazil, Paraguay, Argentina, Chile, Uruguay na Canada ndio kuliko kuwa na wateja wengi ambao kundi la Medellín cartel waliuza dawa zao!

Medellín Cartel walipata wateja wengi duniani kote, huku mapato yao yakiongezeka kila siku
Ajents au washirika wa kila nchi walifanya kazi kwa uaminifu mkubwa huku Medellín Cartel ikiwa na connection kila sehemu kama viwanja vya ndege, bandarini vituo vya barabara ambako kote huko waliweza kupitisha mizigo yao bila kukamatwa!
Pia walitumia mahandaki ya chini
ya ardhi kusafirisha dawa za kulevya kutoka samehe moja mpka nyingine!
Medellín Cartel kwa siku walikuwa wanauza dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya US dola milion 420.
Pesa hizo aliziweka store,vyumbani na nyingine akizichimbia chini ya ardhi! Kila aliyefanya kaz alifaid
Alitafutwa mno mnamo mwaka 1986 alikamatwa na kufungwa jela! Watu walifurahi lakin mwaka 1991 alifanikiwa kutoroka gerezani na kuanza kutafutwa tena! Inasadikika Pablo aliendelea kuuza dawa huku akiwa jela, yaani baadhi ya maafisa polisi walishiriki biashara sababu aliwapa pesa
Aliwah kimbilia mlimani akiwa na mwanae Manuela Escobar na kutokana na baridi kali mwanae alibanwa mno kwa homa ya kukosa joto!
Ili kumnusuru mwanae kipenzi, Pablo Escobar ilibidi ateketeze zaidi ya US dola milion 2 kwa kuchoma moto km tukokavyo moto! Pesa ilitumika km kuni!
aliwindwa mno na ushirikiano wa polisi wa USA kitengo cha DEA dau likitangazwa kwa atakaye fanikishwa kukamatwa kwake. Hata hivyo juhudi zao zilikuwa kaz bure kwani Pablo mwenyewe alijitokeza mwaka 1991 na kudai anaomba ajenge jela mwenyewe Colombia na kufungwa bila kupelekwa
jela za USAakidai ni bora afe akiwa Colombia na sio kwenda kufungwa USA!
Serikali ilikubali na jamaa alifungwa jela iliyoitwa La Catedral! Taarifa zikatoka kuwa jela ya La Catedral ilikuwa na umeme, maji moto, Tv, computers na simu kumaanisha jamaa aliendeleza biashara yake.
Maofis walimuhamishia jela nyingine chini ya ulinzi mkali! Hata hivyo July 1992, jamaa alitoroka tena na taarifa za alipo hazikupatika!
Mwezi Dec 1992 Pablo alifanya part kwenye maficho yake akisherekea miaka 44 ya kuzaliwa ambapo moja ya waliohudhiria alikuwa afisa usalama!
Kesho yake asubuhi vikosi vya usalama, polisi wakisaidiwa na kikosi maalum kutona USA walifika eneo hilo karibu na Medellín na kuvamia ambapo Pablo na bodyguard wake walitoroka kupitia paa la nyumba lakin alipigwa risasi zilizompata kichwani na hapo hapo mwamba akapoteza uhai!
Mpaka anauliwa alicha zaidi ya us dola bilion 60 na inasadikika zaidi ya us dola bilion 2.1 ziliharibiwa ama kwa ukungu, kuliwa na panya na mchwa kutoka na uhifadhi mbovu
Huyo ndiye Pabla Escobar mfalme wa Cocaine duniani!

Imeandikwa na @IamFranco92
Retweet
Like
Coment Asante
You can follow @IamFranco92.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: