#OURprivacyMATTER
#BEsafeONLINE
#SpreadAwareness

🐾HACKING/UDUKUZI

🐾➡️Utajuaje kama unadukuliwa??
🐾➡️Je,bundle lako linawahi kuisha??
🐾➡️Dalili zitakazojulisha kuwa unadukuliwa!
🐾➡️Cha kufanya ukikutana na hali kama hizi!
🐾➡️Pita hapa👇, kisha retweet waipate wengi hii!
#NoSystemIsSafe #SecurityIsMyth

🐾➡️Kumekuwa na mambo mengi sana mtandaoni yanatokea mengine yanatupa faida mengine yanatugharimu, ikiwemo swala la kuingiliwa faragha zetu(hacked). Hii kiukweli si wote wenye ufahamu na hili na wana uwezo wa kujilinda nalo, ila tunaweza kuchukua
.. tahadhari na kujua ni hatua gani tunaweza kuchukua pale tunapogundua kufanyiwa hivi...

.........hujapoteza muda wako kupitia hii thread!....Karibu👇

🐾➡️Hizi ni baadhi ya dalili zitakazokujulisha kuwa unadukuliwa!...

1.BATTERY LIFE
🐾➡️Ukiona battery yako linakata ...
... moto kwa haraka na kifaa chako kinapata moto sana na hio sio kawaida basi tambua watu wanakuchimba!..

... Kiaje?

... Hacker(mdukuzi) hawezi kukuingilia faragha yako bila kiunganishi(Malware or malicious software) chochote kati ya kifaa chako na chake! Hii malware ndio...
.. itakayofanya battery yako iishe kwa haraka, kwa maana itakuwa ikirun bila wewe kuiona na ikifanya kazi kubwa ya kuiba taarifa kwako na kupeleka kwa hacker!.

2.MNYONGEO(SLUG) WA KIFAA CHAKO
🐾➡️Ukiona kifaa chako kinasinzia mara kwa mara(freez)au kinaganda, na muda mwingine...
... utaona unafungua app fulani kisha inaload na kujifunga(crashing) au kuna app kila ukiifunga unakuta ina run!... Au simu yako ina restart yenyewe kila baada ya muda fulani!..
🐾➡️Hii hutokan na malware iliyopandikizwa na hacker inaoverload kifaa chako na kupelekea hayo.
3. DATA(BUNDLE LA MB) KUISHA KWA HARAKA.
🐾➡️Kuna watu wanalalamika sana kuishiwa bundle kwa haraka na kuhisi kampuni za huduma zinawaibia!... Si kweli, zipo sababu kadhaa zinazopelekea bundle kuisha kwa haraka pasipo matarajio yako!..hii nayo ni moja ya sababu.
🐾➡️Hapa kinachotokea ni kwamba malwares hutumia data kutuma taarifa lengwa kutoka kwako kwenda kwa hacker, (Pasipo mtandao huwezi dukuliwa)
🐾➡️Zaidi, kwenye kifaa chako tafuta sehemu ya data management, hapo utaweza ku-monitor data zako vizuri na kujua kila app inakulaje bundle
... pia unaweza hata ukaikuta huko hiyo malwares(utaona tu app ambayo haieleweki inarun)

4.MILIO ISIYOELEWEKA(MYSTERY POP-UPS)
🐾➡️Kuna muda utaona kifaa chako kikitoa mlio ambao huutambui(pop-up alerts) japo sio mara zote! Ila hii huonyesha kuwa kifaa chako kina malwares! Kwa..
... maana hii malware wakati mwingine hulazimisha kufungua mafaili.

5.MAMBO AMBAYO HUJAYATEGEMEA KUTOKEA KWENYE ACCOUNT ZAKO AMBAZO UNAINGIAGA KUTUMIA HICHO KIFAA.
🐾➡️Mfano; kupungua kwa followers, retweets, taarifa kwenye email inbox yako za kulog in au kufanya mabadiliko am..
.. bayo wewe binafsi hukuhusika.
🐾➡️Hapo ni pale kuwa malware ishafanya kazi yake na hacker ana taarifa zako zote na kuweza kufanya anachotaka!..

⚠️CHA KUFANYA UKIYAONA HAYO;
NB;sio moja tuu kuanzia mawili au matatu na kuendelea!
🐾➡️Njia ya haraka na nyepesi ni...
.kufanya analyzation kwenye kifaa chako au kurestart, pia usisahau kutumia Ant-malwares mbalimbali na FIREWALLS!

🐾➡️Kwa leo!.... Nitazileta dalili zingine.. stay tune🚨
🐾➡️Thanks kwa time yako
🙏Kindly RT @razaqdm01 @TOTTechs @GillsaInt @pompeowabuza @DosaRahma @MijuLee_Tz
You can follow @knwlerKIKoti.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: