Hakika Mtaji / Mitaji ni Changamoto sana ila isiwakatishe vijana wabunifu ama wenye mawazo ya Biashara kuona hawawezi kuyafanikisha..

Moja Ya Uwekezaji Wangu Ni Ndani Ya watu wanaofanya / Wanaotaka kuanzisha Jambo ila wanasuasua Kwenye pesa , ushauri ama soko la Bidhaa.
Naomba Leo nimfundishe kidogo mwalimu wangu wa uchumi na uwekezaji @16Limbe Hii mbinu hakuwahi kunifundisha pia nataka nimfumbue Brother @official_silayo Juu ya maoni Yangu ya kwa Nini pesa haiwezi kutunzwa kwenye kibubu ndani na ikafikia kusudi.
Kwanza Niseme Watanzania wengi tuna roho ya Ubinafsi sana na hatuamini Kwenye ushirikiano Brother @JohnieZeBest usiwe mbali pia na wewe tumalizie hapa lile jambo letu.

Vijana wengi sana Wako na Mawazo mazuri ya Biashara ama Ubunifu kulingana na soko la Teknolojia linavyokuwa
Changamoto kubwa sio pesa ili waweze kufika makusidio yao ila Tatizo kubwa ni Uaminifu na Kutokujua mbinu Ya Kuungana Baina Ya mwenye Wazo na Mwenye Mtaji ila siku watu wakikaa Kwenye hii Mbinu Basi Hata ikija kutajwa tuko Kwenye uchumi wa Juu basi hatutalialia.
Wakati naelekeza Juu ya Co Partner Kwenye Jambo nagusia zaidi kama sehemu Ya saving ( Akiba ) kwa mtu mwenye pesa na iwapo ataiwekeza kwa mujibu wa sheria ama makubaliano Basi faida Yake ni kubwa sana kuliko kuwekeza Kwenye Kibubu.
2017 Na 2018 Nilijifunza hii mbinu toka Kwa Brother Mmoja ambaye alianza kuamini Kwenye Hili zaidi Ya Miaka 20 Nyuma Leo yuko hatua kubwa sana kila pesa Yake ambayo anahisi inatosha kuiweka Kwenye jambo basi atatafuta Wenye hilo jambo anawaongezea mbinu na anaweka pesa.
Hii unaweza kuanza kidogo kidogo hata kwa wafanyabiashara wa chini sana Chips, mama lishe, wauza Nguo na Viatu ama vifaa vya umeme.

Natumia Nafasi Hii pia Kuwashukuru Madada Wote waliowahi Kununua ama wanaoendela kununua Viatu na Nguo karibu na Geti Dogo la DIT
Mungu awabariki sana pamoja na macrush wenu wanafanya Myahudi naendelea kupata mahitaji Yangu kupitia Gawio linalopatikana hapo..

Natamani Vijana waamini katika kishirikiana pamoja na watu Wenye mitaji pasipo kuhofia kuibiwa idea zao .
Kitu Cha muhimu kama ni idea zenye kuleta mabadiriko kutoka upande wa Tecknolojia kuna namna na sehemu za kuzisajili kisha tafuta mtu umuelezee aichambue idea kisha akuandikie plan ambayo itakuwa inaonesha namna na wakati wa kupata faida kisha nenda kwa mtu mwenye pesa.
Tafuta Mwanasheria Wamejaa sehemu zote akuandalie mikataba ambayo itaonesha unufaikaji wenu Wote wewe na huyo mtu Mwenye Mtaji pamoja na washiriki wengine kisha wekezeni nguvu kuifanya itokee.
Huo ni Upande wa wenye idea ila ni Wakati sasa wa watu wenye pesa ila hawana sehemu za kuwekeza kutafuta vijana Wabunifu kisha waingie mikataba na wawasimamie mpaka matunda yaonekane.

Usishangae kusikia watu wana pesa afu hawana vitu vya kuzifanyia ni mambo Ya kawaida sana.
Binafsi Naamini Kwenye hizi Njia aidha Kuuza Mawazo Yenye matokeo Chanya ama kuingia mikataba na watu ili kuweza kufanya Jambo .

#Infopreneur #Fixer #Nipedili
You can follow @Wakusnooz.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: