KID BWAY Producer pekee aliyetengeneza Hits Nyingi akiwa mikoani, Tena kwa wasanii ambao walikuwa hawajulikani mpaka kufika level ya kujulikana Tanzania Nzima kutokana na Ngoma zao kuwa kubwa lakini Mara zote kuna sehemu ameonekana kuwa anakwama. #Uzi
Unapolitaja jina la Kidbway akili yako inaweza kuwaza vitu kadhaa kama Producer(Mtayarishaji wa muziki) , Kama Mtangazaji (Presenter) lakini pia kama meneja kwa wasanii ambao aliokuwa anafanya nao kazi kama Label (kama ilivyokuwa kwa majani )
Ukitaja muziki wa Mwanza na kanda ya ziwa Basi moja kwa moja huwezi kuacha kulitaja jina la Kid Bway ambaye alileta Hits Nyingi sana mjini bila hata yeye mwenyewe kuwa mjini. Kwa kumbukumbu zangu nakumbuka msanii Hussein Machozi hakuwa anajulikana kimuziki..
Lakini baada ya kusainiwa Tetemesha Records(label ya Kidbway) aliweza kutengeneza hits kadhaa kama Promise, Kafia Ghetto, Kwaajili yako , Utaipenda na akaenda mbali zaidi kwa level za kimataifa.....
Kwa kutoa Full Shangwe ambayo original yake alikuwepo Ay lakini ikapigwa Remix ambayo humo ndani hitmaker wa Banjuka Mkenya DNA alishirikishwa na ngoma kuzidi kubwa, yote hayo yakifanyika kwa Producer kutoka mkoani Mwanza.
Baada ya kutengeneza Hits kadhaa na Hussein Machozi baadae Machozi aliamua kujitoa label na kuamua kufanya kazi mwenyewe. Na toka hapo Hussein amekuwa si mtoaji wa ngoma za kusumbua kama alivyokuwa Tetemesha.
Baada ya Hussein nyota ikahamia kwa kijana mdogo (enzi hizo) akiwa bado anasoma secondary SAJNA ambaye walitengeneza Hits kama kawaida yake Iveta ikawa Iveta na watu wakaiimba sana Iveta na mikono kama Sitaki Kuumizwa na Linnah nayo ikasumbua.
Naye yalitokea ya Kutokea SAJNA akawa hayuko chini ya Tetemesha Records ndipo kijana C Sir Madini naye akatengeneza naye ngoma kadhaa na ngoma kama Pain Killer ikawa hit kubwa Tanzania. Ila naye hakudumu sana Tetemesha.
Baraka the Prince huyu naye aliwahi kupita Tetemesha Records na Jichunge ikawa ngoma yake ya Kwanza iliyomtambulisha kwenye game na kumfanya kupewa show za Fiesta by that time akifanya bure kwenye show kama mbili tatu lakini uwezo
Na mapokeo ya watu stejini uliwafanya uongozi wa clouds kuona bora wawe wanampa chochote kwani walikuta Kanda ya ziwa watu wanamjua na wanajua sana ngoma za Baraka kiasi cha kuona anastahili kulipwa licha ya yeye awali kuomba afanye show bure.
Baraka chini ya Producer Kid Bway walitengeneza ngoma pia kama Siachani nawe, Na Nivumilie Baada ya Baraka kumalizana na Baraka Kid Bway aliamua kustop masuala ya Label na kwa muda hakukuwa na kazi kutoka kwake.
Lakini miaka kadhaa Kidbway alikuja na kijana COYO nafikiri ndiye rapper pekee ambaye Kid Bway amewahi kufanya naye kazi kama msanii wa Label yake au kum'manage. Naye ngoma kama Njoo baadae , Ziwafikie na Itakukost zilimsogeza mjini.
Ukiangalia vizuri huo mlolongo Kid Bway amefanya hits kadhaa Kali sana akiwa mkoani pengine kuliko producer yoyote kutoka mkoani lakini hakuwahi kudumu na msanii kwenye label yake kwa muda mrefu unahisi shida ni nini???
You can follow @SharoGangstar.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: