THOMAS JOSEPH
ODHIAMBO MBOYA - TOM MBOYA
.
Kijana wa KIJALUO aliyesoma seminari kabla la kwenda kuwa Mkaguzi wa usafi katika jiji la Nairobi. Alikuwa mstari wa mbele kwenye vita vya Mau Mau, akishirikiana na wakenya kupinga sheria kandamizi za umiliki ardhi za wakati huo.....

...Kuanzia mwaka 1953 - 1963 alikua katibu mkuu wa shirikisho la wafanyakazi la Kenya (KFL). Mwaka 1957 alichaguliwa kuwa mwakilishi wa wafanyakazi bungeni akiwa moja kati ya wazawa 8 tu walioingia bungeni wakati huo. Akiwa bungeni alipinga ubaguzi wa rangi na kusaidia....
....harakati za uhuru. Mwaka 1959 akiwa Marekani, aliwezesha kuanzishwa kwa umoja wa wamarekani weusi kuchangisha pesa na kutuma Afrika mashariki jambo lililosaidia Wakenya wengi kusoma nje. Tom Mboya alikuwa moja ya waanzilishi wa KANU na mwaka 1963 baada ya uhuru....
...aliteuliwa na Kenyata kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na baadae alihudumi Wizara ya Maendeleo ya Uchumi kabla ya kuuawa mwaka 1969. Kifo cha TOM MBOYA kiliwastua wakenya wengi na kuzua upya migogoro ya kikabila baina ya wakikuyu na makabila mengine sana sana Kabila la...
....wajaluo alikotoka Tom Mboya.
.
TOM MBOYA anatajwa kama moja ya mashujaa wa kenya japo Historia yake imekua ikifichwa fichwa.
'MWISHO
.
TOM MBOYA anatajwa kama moja ya mashujaa wa kenya japo Historia yake imekua ikifichwa fichwa.
'MWISHO