Faham machache kuhusu mwanamuziki huyu maarufu kutoka nchini Marekani. Marvin Gaye: Alizaliwa 02April, 1939 – na kufariki 01April, 1984

Nimekutengenezea video yenye maelezo machache kwa mtindo wa Maandishi.
Full story: SHUKA NA THREAD

Marvin Gaye mtoto wa pili kati ya watoto wanne kwa Mchungaji Marvin Pentz Gay Sr na mwalimu Alberta Williams. Baba yake Marvin alihubiri katika kikundi cha Kanisa la sabato kinachoitwa “HOUSE OF GOD” Nyumba ya Mungu, Wakiwa na kanuni madhubuti zenye maadili na
mafundisho yenye mchanganyiko "Uyahudi wa Orthodox na harakati za watu weusi" hawa hawakuwa na sikukuu wala sherehe ya siku ya kuzaliwa. Baba wa Marvin alikuwa baba anayeogopeka nyumbani kwake, alikua mkali na hakusita kugawa dozi kwa watoto wake wanne pale wanapozingua
Jeanne Gay aliwahi kusema kuwa baba yao hakuwahi kuelewana na Marvin. Lakini kumbuka, Hata uwe mkali vipi, kuna mtoto utamshindwa tu na ataishi anavyotaka. Marvin aliacha shule na kujiunga na Jeshi la Anga la Marekani.
Aliacha kazi baada ya miezi kadhaa tu kwakua alikataa kufuata masharti ya mkuu wa kikosi (ODA).

Ndugu yake ambaye ni Frank akaungana na kaka yake katika shughuli ya muziki na kuanza kurekodi huko Motown (Marvin aliwahi kuwa mpiga ngoma kabla hajawa muimbaji kamili)
Alibadilisha jina lake kutoka Marvin Gay kuwa Marvin Gaye na kuongeza 'e' ili kujitenga na baba yake (Alitengeneza jina jipya la ukoo wake) pia alidhamiria kumaliza mgogoro kuhusu ujinsia wake @Wakazi
kwakua neno Gay linamaanisha mtu mwenye mahusiano ya jinsia moja (kiuhalisia Marvin hakuwa mtu wa hivyo, bali ni jina tu la Baba yake), alimuiga rolemodel wake Sam Cooke, ambaye pia aliwahi kuongeza 'e' kwenye jina lake la mwisho. @BrianSimba_
Marvin alioa mara mbili. Ndoa yake ya kwanza ilikua na Anna Gordy dada wa Berry Gordy, mwanzilishi wa Motown record label. Aliwahi kumuimbia vibao kama “Stubborn Kind of Fellow” na " You Are a Wonderful, walimlea Marvin Pentz Gaye III (Juni 8, 1965).
Mwaka 1973 alipotoa album ya Let's Get It On akaanza kutembea na mtoto wa Slim Gaillard aliyeitwa Jan Hunter na kupelekea kutengana na Anna. Wawili hao walifanikiwa kupata watoto wawili Nona Marvisa Gaye na Frankie Christian Gaye.
Walioana Oktoba 1977 pale ndoa ya Marvin na Anna ilipovunjwa rasmi.
Wao pia, Walitengana kwa sababu ya mvutano na mwishowe walipeana talaka mnamo Februari 1981.
Hapa Marvin akaingia kwenye msongo wa mawazo na kutumia madawa ya kulevya.
Mwisho aliamua kurudi nyumbani kwao mwaka 1983.

Asubuhi ya April 1, 1984, kulikua na malumbano kati ya baba yake Marvin (Marvin Gay, Sr) na mke wake Alberta. Kama unavyotambua baba yake alikua mtata sana na haambiliki @MabalaMakengeza @magolanga @gracemacha
Marvin akaamua kumsaidia mama yake kwa kumgomea baba yake kuwa LEO UKIENDELEA KUMUONEA MAMA LAZIMA NITAKUDHURU. Baba wa Marvin akachukua bastola na kumpiga Marvin kifuani upande wa kushoto (kwenye moyo). @imaniabel37 @TizibazomoB @SalumSl0
Mdogo wake Marvin ambaye pia alikua mwanamziki, alikua jirani na maeneo hayo na ndiye aliyesikia maneno ya mwisho ya Marvin,

alisema “Nimepata nilichokihitaji, nilishinwa kujiua mwenyewe na leo nimemfanya aweze kuniua” @TweveDevotha @IAMartin_ @MarekaMalili
Kumbuka Marvin aliwahi kujaribu kujiua Mara tatu. Mwaka 1969 alitaka kujipiga bastola, wakamzuia na Berry Gordy.

Baada ya miaka 10 alijaribu kuji overdose na madawa ya kulevya lakini hakufa, @derick_tz @mwanichetae @HKigwangalla
Siku kadhaa kabla hajauawa na baba yake, alijirusha kwenye gari lililokua kwenye mwendo mkali na hakufa.

Kwa maelezo ya baba mzazi wa Marvin akiwa mahabusu alisema “hakudhamiria kumpiga risasi mwanaye, siku hiyo Marvin alikua kama mbogo na alimshambulia kwa ngumi nyingi.
Alipojaribu kukimbilia chumbani kwake, Marvin alimfwata. Alimwogopa kwasababu alikua anatumia madawa aina ya cocain na kuhisi angemdhuru. Hata wakati anapiga risasi hakujielewa na alidhani kulikua na baruti tu ambayo ingemtisha Marvin.
@tweetsrifle
You can follow @humphreymoris.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: