Maria na Consolatha.
Unapozungumzia mashujaa waliovunja na kuvuka vikwazo katika mfumo unaowanyima haki sawa kielimu watu wenye ulemavu nchini Tanzania huwezi kuwaacha mapacha hawa, maarufu kwa jina la Mapacha wa Makete.

Pamoja na changamoto za kimfumo na kimiundombinu
Maria na Consolatha walifanikiwa kusoma mpaka kufikia ngazi ya Shahada ya kwanza, ni bahati mbaya tu kifo kilikatisha safari yao kwa ghafla.

Mapacha hawa walisoma Shule ya Sekondari uduzungwa na walifaulu kwa Daraja la Pili na kufanikiwa kuchaguliwa Chuo Kikuu Katoriki cha Ruaha
Maisha ya Maria na Consolatha yanekuwa ni fumbo lililojaa mafunzo mengi kwa mtu ambaye atafungua macho kwa ufanisi na kuona.

Pamoja na ulemavu wao, walikuwa na ndoto na matumaini makubwa ya kesho.

Nilikutana nao May 2018, na maongezi nao yalinifanya nijihoji mambo mengi sana
Ni bahati mbaya Maria na Consolatha hatujawapa heshima wanayostahili.

Mpaka leo, sidhani kama kuna taasisi au hata bodi yoyote iliyowai kutambua mchango wao katika kuonesha umahili katika kuonesha uwezo wa watu wenye ulemavu regardless ya vikwazo.
Yote kwa yote, Maria na Consolatha wametuachia mafunzo yafuatayo:

1. Ulemavu si kushindwa
2. Hatuna kisingizio cha kufikia malengo
3. Vikwazo vya kielimu vikitatuliwa waalemavu watapata elimu bora
4. Kuna uthamani katika maisha ya kila binadamu.
Wito wangu, Maria na Consolatha wanahitaji TUZO YA HESHIMA. Kutoka chuo chochote kile.

Maria na Consolatha wameyafanya kwa vitendo yale ambayo watu wengine wanayaandikia THESIS tu.

#HonoraryDoctorateForMariaAndConso
#HonoraryDoctorateForMariaAndConso
You can follow @TZFanatic.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: