"NIHURUMIE.."🙍‍♂️

Nipo zangu gheto siku hiyo ni weekend imeanza,sina hela wala mchongo wowote wa maana niliofanya wiki nzma..kimtndo najiona fara ila sa ntafanyaje..nilipambana nilivyoweza atleast sifi njaa..ingekua ni leo ningejiona msanii kama chris anavyotuitaga..
Ila shkopa..nikavuta kiepe kikavu,vuta Pc,weka headphone..nianze kula movie ya fast n furious.
Nikakata almost dk 40 hvi..naskia kwa mbali kama sauti nyingi nje..nika pause..toa headphone nasikia kelele nje kidgo ya nnapokaa..siwezi pitwa kinyozi Richy anihadithie huwa ana chumvi
nyingi😅 kama umekaa survey karibu na survey motel au kwa Shengena baba ntilie utamjua tu..
So natoka kwenda kucheck..naona watu wamejazana kama duara..najaribu kupenya ila siwez kuona vizuri..naamua kuforce kingi..dah nakuta dogo wa makamu ya kwenda chuo kashikiliwa
Damu zimefunika nyuso,sauti mbalimbali zinasema aveshwe tairi,kuna mtu ananyoosha gongo anamtandika begani..tofari linatokea kati ya watu wa nyuma bahati nzuri linampitia na kumpata kidogo kwenye paji la uso..namwangalia vizuri sura kama naijua ila amevimba kichizi na damu imejaa
Anaangalia upande wangu niliosimama kwa jicho moja ambalo lipo sawa kidogo maana yamevimba..hawezi kuongea vizuri nnachosikia ni "NIHURUMIE.."
Nashindwa kuendelea kuangalia natoka nauliza kwani kaiba nini..hamna anaejua..nyuma namwona mama naomi namfata
Anasema anasikia kakutwa nje kwenye nyumba ya wanachuo wanaopanga anaanua nguo zao..nauliza ni nani?naambiwa ni mtoto wa mama flani (sitamtaja jina..)
Dah..dogo namjua na mara nyingi anakujaga hadi gheto kuniomba nimwekee movie..
Najaribu kurudi nichek kweli kama ni yeye maana moyo kma unagoma kuamini ila nashndwa watu ni wengi..mara yowe zinapgwa nyuma mama ake anatokea anakimbia machozi kibao anasema "msiniulie mwanangu" anapita kwa nguvu hadi kati japo watu wanajitahidi kumzuia ila wap
Anakatiza anaenda kumfunika kwa mwili wake pale chini..anavua kitenge anamfunika mwanae anabaki na chupi tu...wamama kama wawili wanaamua kuingia na khanga zao ili kumsitiri mwenzao..hvyo umati kidgo unasitisha dozi na baada ya dk kumi wanatokea wanajeshi wawili wanatuliza
Watu na kumchukua dogo..sikumwona tena hadi nahama kule..

Jana nipo zangu maeneo kisehem flani Tegeta ki date cha kishkaji..namwona dogo..katinga uniform freshi..Ile kuniona tu kwenye meza akashtuka..
Akasema " bro nakujua ila sidhani kama unanikumbuka"
"Nikamwambia kunenepa kwako kusikudanganye"
Tulipiga stori kidgo akanieleza kilichomkuta tukagusia kidgo siku ile japo nilijalibu kukwepa hyo mada ila alinambia, ukiona kifo kwa karibu tena ukizingatia ni kwa kitu kidgo kama nguo lazima ubadilike
Alinambia "bro,wengi pale mtaani walikua wanaogopa vitu vyao nisije iba..ila wewe ulikua unaniruhusu hadi ndani..movie unanipa..stori japo sio nyingi ila tunapiga na hukuwa na tatzo ndo maana niliapa sitakupiga tukio..
Na siku ile nipo chini pale nikakuona umesimama tu unanishangaa..nikawaza ni wewe pekee unaweza nisaidia maana hujawah nichukulia kama mwizi nikaomba kwa mungu unisaidie..ila ukatoweka..ila nashukuru hukunyanyua mkono wala mguu kunipiga"
Kiukweli karoho kakaniuma kidgo.
Akaniambia sasa yupo pale anafanya kazi analipwa fresh..kapanga gheto nyuki na anaishi na mchumba wake na anakaribia kujifungua..akaomba nimtembelee na mawasiliano tukapeana

Maongezi hayakuchukua hata dk 10 ila yalikua deep sana
Wakati nasepa nilimwangalia kichzi wakat tunaagana
Moyoni nikasema "KUNA MAFUNZO MENGINE HUWA MAZITO"
Unaweza usiwe mwizi ila kama unachofanya sicho,
FUNZO LAJA.

#fanani✍️ hapa

Wote Turetweet for awareness🙏
@gracemella95 @Mshambaflan @abdulazackabdul @MarekaMalili @mpambazi_
You can follow @crazyTanzanian.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: