Ted Bundy: Mwanaume aliyevaa tabasamu la kifo cha wasichana.
--------------------------------------------------
Alipotabasamu, wasichana walimwita "handsome". Hawakufahamu kuwa, ni yao hukumu.

Aliishi na mama yake mzazi akijua ni dada yake wa tumbo moja.

Akiwa mdogo, 👇🏿
alizungukia majumbani mwa watu nyakati za usiku, alifunua mapazia ili tu, apate kuwaona wanawake wakiwa uchi.

Alipokua, alifurahia kuua wasichana kama anacheza bao. Aliweza kuua leo, kesho yake akafanya mapenzi na maiti iliyopoa.

Mara nyingine baada ya kuua, alikata baadhi
ya vichwa vya wasichana na kulala navyo kitandani. Alipochoka, alivichoma moto. Alijisikia fahari.

Aliua mji kwa mji; jimbo kwa jimbo; mmoja baada ya mwingine. Kila kona ilikuwa kilio. Ndani ya miaka minne, wasichana wa chuo walipotea kama shilingi majini.

------
"Usiku huo, nilisikia mlango wa chumba chetu unafunguliwa kwa nguvu, nilijaribu kufumbua macho kwa mshangao kutoka katika lepe la usingizi, nilimuona mtu amekwisha ingia. Nilipojaribu kukaza macho na kutilia maanani, alinyanyua mkono wake, na alikuwa ameshika kitu, nafikiri
nafikiri lilikuwa bomba ama fimbo. Sijiui kilikuwa ni kitu gani. Alinisogelea na kunipiga nacho usoni..ilikuwa kama nimechomwa na sindano au nimekatwa na kisu. Mwanachumba mwenzangu[Karen Chandler] aliamka na kutazama kwa mshangao, kabla na yeye kupigwa. Bado nilikuwa nina fahamu
kidogo na naweza kujongea. Alirudi upande wa kitanda changu, alinyanyua tena mkono wake kunipiga kabla mwanga haujaangaza chumbani kwetu. Ulikuwa mwanga wa gari, mmoja[Nita Neary] wasichana alikuwa anarejea akitoka kwa mpenzi wake...[mwanaume] aliogopa..akaondoka haraka", alisema
manusura wa mauaji, Kathy Kleiner, katika kumbukizi ya ya tukio siku hiyo, katika mahojiano yake na CBS NEWS, April 2020.

Ndiyo, ilikuwa ni nyakati za giza la asubuhi, majira ya saa tisa na dakika, siku ya tarehe 15 Januari, 1978. Kwa muda usiozidi dakika 15, mwanaume
ambaye hakufahamika alivamia katika nyumba za "Chi Omega" wanamoishi wanafunzi wa chuo cha Florida, Marekani. Mtu huyo alikwenda haraka katika chumba kimoja kilichokuwa na wasichana wawili, Lisa Levy na Margaret Bowman. Aliwanyanyasa kingono wasichana hao baada ya kuwaua kwa
kuwapiga vichwani. Kwa muda huo mfupi, alikwenda chumba kingine, ambako aliwakuta tena wasichana wawili, Kathy Kleiner na Karen Chandler, wakiwa wamelala. Alifungua mlango kwa shari, kisha akawapiga vibaya wasichana hao kabla ya kugutushwa na mwanga wa gari ambao ulimkimbiza
haraka.

Lakini wakati mwanaume huyu akitoka kwa haraka, alipishana na Nita Neary, msichana aliyekuwa ameshuka kutoka katika gari iliyomulika mwanga muda mfupi tu. Nita alishangaa, haikuwa kawaida mwanaume kufika katika majengo ya wasichana wa chu ya "Chi Omega". Kupishana na
Nita, lilikuwa kosa kubwa kwa mwanaume huyu lililokuja kumuhukumu baadaye. Haikuwa kawaida yake kuacha ushahidi nyuma - kuonwa, alama, ama kuacha mtu akiwa hai. Yawezekana alifanya makosa siku hiyo. Ndiyo, "siku za mwizi ni arobaini".

Muda mfupi tu, Sheriff Ken Katsaris
wa eneo hilo alipokea simu iliyomtaarifu kuwa kuna mauaji wasichana wa chuo cha Florida yametokea katika majengo ya "Chi Omega". Alishtuka. Alikwenda haraka na timu yake akiambatana na ofisi ya uchaguzi. Muda mfupi polisi walikuwa eneo la tukio huku miili minne ikitolewa nje.
Haikupita muda mrefu, Sheriff Katsaris alipokea tena simu, jengo la sita kutoka hapo kuwa wamesikia kelele za msichana akipigwa. Polisi walikimbia haraka, walipoingia ndani ya chumba hicho tu, walimkuta msichana mwingine wa umri wa mika 18, Cheryl Thomas, akiwa amelala katika
dimbwi la damu. Jambo ambalo liliwachanganya. Wakajiuliza inawezekana ni mtu mmoja aliyefanya hayo?

Ndiyo, baadaye taarifa zilitoka kwamba wasichana wawili wamefariki baada ya kuumizwa sana kichwani sanjari na kunyanyaswa kingono. Na wengine watatu wakiwa mahututi kwa
kuvunjwa mafuvu na taya.

Licha ya Nita Neary, kutoa taarifa polisi jinsi alivyopishana na mwanaume mmoja, lakini haikuwa rahisi kumjua. Kwa wakati huo, haikufahamika kwa urahisi ni nani hasa amehusika na unyama huo. Polisi walishangaa, kwamba kwa muda huo mfupi, mtu mmoja
aliwezaje kufanya unyama huo kutoka jengo moja kwenda lingine. Lakini alama ya meno ilibaki katika mkono wa msichana mmoja, Karen Chandler. Hata hivyo, je ni nani wa kumkamata na kumpeleka kwa "Forensic Dentist" ili kuoanisha meno yake na alama hiyo? Hakuna. Na zaidi, katika
katika nyanja ya sayansi ya utambuzi("Forensic") Marekani, utambuzi wa kuoanisha meno haujawahi kufanyika kabla.

Lakini wakati wa uchunguzi wa jambo hilo, Sheriff Katsaris alipokea simu kutoka Colorado. Walimwambia kuwa wameona taarifa juu ya unyama wa wasichana hao. Lakini
wakampa anagalizo kuwa kuna wanaume ametoroka moja kati ya gereza mjini Colorado siku chache tu zilizopita. Anaweza kuwa yeye? Mwanaume huyo anaitwa Ted Bundy. Sheriff Katsaris aliwahi kusikia habari juu ya mtu huyu anayetafutwa na FBI, japo hakuzipa uzito sana kuwa anaweza kuwa
yeye.

Mwezi mmoja baada ya tukio, siku ya tarehe 15 Februari, 1978, katika mji wa Pensacola Florida, lilipita gari la 'kibishoo' wakati huo aina ya "Volkswagen Beetle", ilikuwa ya rangi ya kahawia. Iilipita kwa mwendo wa kasi mno! Polisi walilitilia shaka, walilifukuza hadi
pale liliposimama. Dereva wa gari hiyo alikuwa kijana wa umri wa miaka 31, mtanashati, sura ya bashasha, mwenye kujiamini mno, na zaidi, sura ya kuwatutia wasichana.

Polisi walipomuuliza jina, alikuwa akiketa usumbufu kuwatajia. Lakini aliwaambia yeye ni mwanafunzi wa sheria
You can follow @OscarMwaisoloka.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: