Tukumbushane kidogo kuhusu KIHARUSI (Stroke)
Tatizo la dharura la kiafya ambalo ni moja ya magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo.
Mitindo ya maisha na Lishe ni vitu vinavyochangia idadi ya wagonjwa wanaopata stroke kuongezeka
Kiharusi huacha ulemavu au kifo




KIHARUSI hutokea pale seli za ubongo zinapokufa kutokana kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo hivyo kukosa hewa ya oksijeni na virutubisho.
Kiharusi kikihusisha mshipa wa mkubwa wa damu kwa wastani mgonjwa hupoteza seli za ubongo (neuroni 1.9) kila dakika.

KUNA AINA KUU MBILI ZA KIHARUSI
Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo
Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo
80% ya watu wanaopata kiharusi hutokana na kuziba kwa mishipa ya damu kwenye ubongo.




Vitu ambavyo huchangia watu kupata kiharusi
Ugonjwa wa Shinikizo kubwa la damu
Ugonjwa wa kisukari
Lehemu kuzidi kwenye damu
Uvutaji sigara
Magonjwa ya moyo
Uzito uliopitiliza
Unywaji wa pombe uliokithiri
Kutokufanya mazoezi








Lishe ni muhimu sana katika kupunguza hatari ya kupata kiharusi.
Takribani 25% ya kesi za kiharusi uhusishwa na ulaji usiofaa
Boresha lishe kwa kuzingatia:
-Matunda kwa wingi
-Mboga za majani
-Punguza kiasi cha chumvi
-Punguza matumizi ya nyama nyekundu


-Matunda kwa wingi
-Mboga za majani
-Punguza kiasi cha chumvi
-Punguza matumizi ya nyama nyekundu
Shinikizo kubwa la damu huchangia watu wengi kupata kiharusi. Msukumo mkubwa wa damu kupasua mishipa ndani ya ubongo na kupelekea kiharusi
Pima presha yako mara kwa mara ili kama una presha uanze tiba mapema

Unene uliopitiliza na kitambi huchangia watu kupata kiharusi
Unene husababisha mrundikano wa mafuta kwenye kuta ya mishipa ya damu ambayo ni kihatarishi cha kuziba kwa mishipa kwenye ubongo
Kupunguza uzito ni njia mojawapo ya kudhibiti kiharusi.

Kupunguza uzito ni njia mojawapo ya kudhibiti kiharusi.
DALILI ZA KIHARUSI
Ganzi au udhaifu upande mmoja wa mwili
Kushindwa kuona ghafla
Kushindwa kuongea au mdomo kupinda kuelekea upande mmoja
Kichwa kuuma ghafla kama umepigwa nyundo kichwani
Kupoteza fahamu, kuchanganyikiwa





"FAST" ni namna unayoweza kugundua kiharusi haraka na kutafuta msaada haraka
F-ace : Mdomo kupinda kulekea upande mmoja
A-rm : Kushindwa kunyanyua mkono
S-peech Kushindwa kuongea au kuongea maneno hayaeleweki
T-ime : Muda ni muhimu ili kuokokoa maisha, tafuta tiba ya haraka.
F-ace : Mdomo kupinda kulekea upande mmoja
A-rm : Kushindwa kunyanyua mkono
S-peech Kushindwa kuongea au kuongea maneno hayaeleweki
T-ime : Muda ni muhimu ili kuokokoa maisha, tafuta tiba ya haraka.