Uasi wa Jeshi la TR na Jaribio la Kumpindua Mwl. Nyerere Mwaka 1964.
.
Peter Bwimbo alikua Mlinzi namba moja wa Mwl. Nyerere. Alianza Kama Askari wa kawaida enzi za mkoloni, akahamishiwa kikosi maalumu na baada ya uhuru akapewa jukumu la kumlinda Raia namba moja.
.
thread - uzi
.
Peter Bwimbo alikua Mlinzi namba moja wa Mwl. Nyerere. Alianza Kama Askari wa kawaida enzi za mkoloni, akahamishiwa kikosi maalumu na baada ya uhuru akapewa jukumu la kumlinda Raia namba moja.
.
thread - uzi

Katika kitabu chake kilichotoka mwaka 2016 kikiwa na jina la "Peter D.M. Bwimbo, Mlinzi Mkuu Wa Mwalimu Nyerere", Peter alieleza namna yeye pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa wakati huo walivyofanikiwa kumtorosha Mwl. Nyerere katikati ya kashi kashi la uasi....
....Peter anasema, alipokea simu saa 8 za usiku kutoka kwa Leon Kazimili ambaye alikua afisa usalama wa zamu wa ikulu siku hiyo. Kazimili alimwambia ameongea kwa simu na mkuu wa majeshi Brigedia. Patrick Douglas(Muingereza) ambaye amemfahamisha kuwa kuna wanajeshi....
....wamevamia Kambi ya Lugalo, hivyo amemuomba amuamshe Mwl. Nyerere kumpa taarifa kwa sababu Brigedia. Douglas hampati Mwalimu kwa simu. Hivyo Peter alitoka fasta nyumbani kwake Upanga na gari yake aina ya Benz Sedan 190 na kukimbia Ikulu ambapo alifika saa 8:20 usiku....
....Alipofika alikuta tayari vijana wake wamesha muamsha Mwalimu Nyerere na Waziri mkuu Rashidi Kawawa na wameshatoka nje wamesimama mlango wa mbele wa ikulu. Baada ya dakika chache waliwasili wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa wakati huo, Mkurugenzi mkuu wa TISS....
....Emilio Charles Mzena na Inspekta Mkuu wa Polisi Elangwa Shaidi. Lakini kati yao hakuna aliyekuwa na taarifa za kutosha kuhusu uasi unaoendele. Hivyo Peter ilibidi achukue uamuzi wa haraka ili kulinda uhai wa viongozi wakuu wa Nchi. Bila kupoteza wakati ilipofika saa....
....8:45 usiku ule, Peter aliwachukua Mwalimu na Kawawa na kuondoka nao kuwatoa ikulu kupitia geti la nyuma, Na ikulu aliwaacha Mkurugenzi wa TISS Mzena na IGP Shaidi. Kwa usalama wao alihakikisha hakuna aliyefahamu anawapeleka wapi, Alipotoka mlangoni aliondoka na asikari 2....
....Hivyo wakawa watano Mwalimu, Kawawa, Peter na wale askari 2. Walienda mpaka kivukoni feri ambapo walikuta pantoni wakapanda kuondoka kuelekea Kigamboni. Alipopanda alimwambia mwendesha pantoni kwamba kuna kikao cha dharura kinachofanyika Chuo cha Kivukoni....
....Na viongozi hao wawili wanatakiwa kuhudhuria haraka. Peter anadai wakati wanaanza safari na pantoni walisikia kelele kwa mbali ambazo zilikua kama ishara kwamba wanajeshi waasi tayari wameshatia timu Ikulu. Walipofika kigamboni, Peter alimwambia Mwendesha Pantoni....
....asirudi upande wa magogoni awasubiri wanaenda fasta kwenye kikao na wanageuza muda si mrefu, lakini nia yake ilikuwa kumzuga ili kupunguza uwezekano wa waasi kuweza kuwafuata nyuma. Waposhuka walianza kutembea kuelekea Mji mwema, wakapita Mji mwema wakaingia kijiji cha....
...Salanga. Walipofika Salanga, Peter aligundua kwamba kuna karibia kukucha hivyo ingekuwa hatari kutembea na viongozi hao, Hivyo waliingia kwenye nyumba ya mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la Sultan Kizwezwe ambaye aliwakaribisha vizuri na kuwahifadhi. Wakati huo uasi ulikua...
....umeshika hatamu, jiji lipo kwenye taharuki na baadhi ya raia wenye asili ya asia walikua wakiuawa. Kwa zaidi ya masaa 24 hakuna kiongozi wala mwananchi yoyote aliyekuwa akijua Rais na Waziri mkuu wako wapi, pia Mwalimu na Kawawa walikua hawajui kinachoendelea nje....
....kwasababu pale kijijini kulikuwa hakuna simu wala namna yoyote ya mawasiliano. Baada ya siku mbili Bhoke Munanka aliyekuwa waziri wa nchi alikuwa mtu wa kwanza kujua walipo Mwalimu na Kawawa akaenda kuwaeleza kinachoendelea na akapewa maelekezo ambayo alirudi kuwaeleza.....
....Viongozi waliokuwa Ikulu. Baada ya uasi kutulizwa na waziri wa ulinzi Oscar Kambona. Mwalimu na Kawawa walirudi ikulu na kukutana na viongozi wa uasi Elisha Kavana na Francis Hingo Ilogi. Baada ya makubaliano ya mabadiliko ya mfumo na maslahi kwa wanajeshi kufikiwa....
....Waasi walikamatwa na kupekwa mahakamani ambapo walisomewa mashtaka, kukutwa na hatia na kufungwa.
'MWISHO
'MWISHO