Sitaisahau hiyo siku, yapata miaka 10 sasa imepita. Nilikuwa natoka Dar naelekea Mbeya, asubuhi saa kumi na moja nipo Ubungo. Kufika, foleni ndefu watu utitiri kama sisimizi. Ikabidi kushuka, kutembea kwa mguu. Nilienda na usafiri binafsi @SwahiliBible @tonytogolani https://twitter.com/SwahiliBible/status/1265167073178726400
Akatokea kijana mmoja na mkokoteni, "Dada nipe mzigo wako twende haraka". Nikampa. Nkawa nyuma yake tunaenda chap chap... Tumeenda mpk pale getini, kwasababu ya wingi wa watu, kuingia hivi, kanipotea. Nikapanic. Kila kitu kipo sandukuni. Watu wengi. Nageuka kila mahali simuoni.
Kucheki muda, almost time. Nikasali, Mungu, naomba malaika zako wamlete huyu mtu kwangu. Sina jinsi ya kumpata. Yaani, sijui nisemeje. Ilikua kufumba na kufumbua, huyu hapa. "Oyaa sista, ndo nini kunipotea hivyo"... Hapo ninatetemeka maana ilikua kama mtu kanijibu mawazo yangu...
Nikawaza, angeweza kuniibia akatoroka. Lakini Mungu mkubwa, ananilinda kila niendapo japo simuoni. Nikabaki na shukurani na kujua sipo peke yangu duniani. Malaika zake wapo nami wakati wote.