IT WAS ALL A DrEaM.

Kuifikia ndoto yako kuna ups and downs, cha muhimu simamia kile unachoamini, ushauri unao pewa changanya na zako.Twende na Kijana Raheem Sterling kumalizia Weekend Yetu


Kuifikia ndoto yako kuna ups and downs, cha muhimu simamia kile unachoamini, ushauri unao pewa changanya na zako.Twende na Kijana Raheem Sterling kumalizia Weekend Yetu
Raheem Sterling amezaliwa mwaka 1994, katika familia yake alibahatika kua na dada mmoja, akiwa na umri wa miaka 2 baba yake aliuwawa
. Kitu ambacho kilibadilisha maisha yake yote. Doh! Mama yake akaona njia pekee ni yeye kumaliza masomo yake ili aweze kulea watoto wake.

Baada ya muda mfupi mama yake alifanya maamuzi ya kuhamia uingereza(England) kusoma elimu yake ya shahada(degree)ili awatafutie wanae maisha mazuri. Raheem na dada yake walibaki Jamaica na bibi yao.Waliishi na bibi yao kwa miaka kadhaa hapo Kingston Jamaica.
Raheem alipata shida sana kuzoea kuishi mbali na mama yake, ingawa alikuwa anapata kila kitu kutoka kwa bibi yake
Raheem alikua akiona watoto wenzie wakiwa na mama zao alikua akiumia sana na kupata wivu lakini hakua na jinsi. Alikuwa haelewi kabisa ni nini mama yake anafanya

Kwa umri ule Raheem aliona si sawa kukaa mbali na mama yake mzazi. Kiukweli it was hard
Bibi yake alijitahidi kuonyesha upendo ili watoto wasijisikie upweke. Raheem alikua na mpira wa miguu so aliutumia kucheza akiwa na watoto wenzake hasa kipindi cha mvua


Akiwa na umri wa miaka 5 kabla ya kuhama kutoka Jamaica kwenda Uingereza kwa mama yake, Raheem akili yake ilianza kukomaa akiwa na lengo moja tu la kumsaidia mama yake. Woiii! Ni baada ya kuona jinsi watu wa hapo Jamaica wanavyo pambana kutafuta maisha ili kukidhi mahitaji yao.
Walihama kutoka Jamaica na kwenda London kuishi na mama yao, Raheem alipata wakati mgumu sana sababu ya utofauti wa tamaduni, na walikua hawana pesa ya kutosha. Lakini Mama yake alipambana kutafuta chochote ili akidhi mahitaj ya watoto na ada ya kujilipia masomo yake.
Kama tunavyo jua katika maisha kina mama ni wapambanaji hata akiwa hana kitu hawezi kuonyesha unyonge wake mbele ya watoto. Mama Raheem alikuwa akifanya usafi kwenye hotel hapo jijini London ili apate fedha ajilipie ada na kuhudumia watoto. So Raheem na dada yake waliamua..
asubuhi kabla ya kwenda shule wanaenda kumsaidia mama yao kusafisha vyoo vya hotel, na kutandika vitanda, baadae walijikuta hadi wanapeana zamu leo mmoja akisafisha vyoo kesho anatandika vitanda. Oooops tunasema penye upendo wa kweli kuna kuhurumiana

Kipindi icho Raheem alikua shule ya msingi, alikuwa ni mtoto mtundu sana, alikua akimsikiliza mama yake tu. Ilifika sehemu alihisi kutosikia kwake anaweza mpa ukichaa mama yake. Akiwa darasani hamna mwalimu alikuwa akimsikiliza yeye anawaza muda wa mapumziko ufike atoke nje.
ale chakula na kucheza, alikua anapenda kucheza kwa kumuigiza Ronaldinho
. Kutokana na kuto sikia, ilibidi walimu wamshauri mama yake kua Raheem anahitaji uangalizi wa karibu sana. Ilibidi abadirishwe darasa, akawekwa darasa la wanafunzi 6 na walimu 3
ilikuwa ngumu kujificha.


Siku ambayo Raheem hawezi kusahau ni siku ambayo alikua ndani ya gari la shule, ambalo lilikuwa lina wachukua kila siku na kuwa rudisha, akiwa ndani ya gari alitazama nje akaona watoto wa kike na wakiume wakienda shuleni bila usimamizi huku wakifurahi. Kile kitendo kilimuumiza,
na kutamani kua kama wale watoto. Akajiona alikua anakosea sana kutokana na tabia yake. Huu ulikua mwanzo wake wakubadili tabia yake, Kweli alibadilika na kua na tabia njema. Baada ya mwaka mmoja alihamishiwa shule nzuri zaidi na maisha yalibadilika baada ya kukutana na Clive.
Clive alikua akifanya kazi ya kulea watoto wasio na baba jiran na kwa kina Raheem. Weekend anawapeleka mjini na kuwaonesha vitu mbali mbali na jinsi watu wakiishi hapo London. Siku moja Clive alimuuliza "Raheem ni kitu gani unapenda kufanya"? Raheem hata hakuwaza sababu hakua na
ndoto yoyote kwa muda huo, so alimjibu tu kucheza mpira wa miguu
Awww Clive akasema waooo "I got little sunday league" unaonaje ukijiunga nasi? Lahaulaaa huu ulikuwa mwanzo wa Raheem kuanza kuwaza kucheza mpira wa miguu muda wote. Akiwa na umri kati ya 10 hadi 11....

alipata scouts kutoka vilabu vikubwa mbali mbali Jijini London. Fulham walimuhitaji na Arsenal pia walimuhitaji, kitendo cha Raheem kuhitajika na Arsenal kilimfanya awe excited sana sababu ni team kubwa Jijini London, akaanza kuwaaga rafiki zake kwamba safari ya kwenda Arsenal.
imewadia
banaa weee asijue nini mama yake anawaza juu yake. Mama yake ni wale wa mama anaweza kukushauri kama kuna mtu unampenda ukamuacha
akaanzia mbali mwanangu nakupenda sana, wewe kwenda Arsenal sio chaguo sahihi kwa sasa sababu Arsenal ni team kubwa na ina vijana 50..


Kama wewe na wewe ukienda utaongeza namba tu
. Inabidi uende team ambayo utaanza kikosi cha kwanza
. Akaendelea kumsisitiza na kumshauri aende QPR. Kweli Raheem alimsikia mama yake na kufanya maamuzi ya kwenda QPR. Bhanaa weee shida ikawa mama yake hawezi kumuacha Raheem aende


Training mwenyewe na muda huo alikuwa amebanwa na kazi. Ilibidi dada yake abebe jukumu la kumpeleka mdogo wake training kila siku na kumsubiri arudi nae nyumbani. Kitu kilimpa furaha Raheem hakuwahi sikia dada ake akilalamika kuchoka juu yake
ilimpa sana moyo wakupambana.

Sehemu walikuwa wakiishi Raheem akizunguka tu nyuma ya Nyumba anaona uwanja wa Wembley, akijiona anazidi kuishi kwenye kimvuli cha ndoto zake.Akiwa na umri wa miaka 14 kuna mwalimu alimuuliza "Do you think football is going to be your end goal"? Raheem hakua na jibu zaidi ya
nitakuonyesha. Kweli baada ya miezi 2 akaitwa team ya taifa chini ya miaka 16 na aka assist goal 2 baina ya Northern Ireland. Juma 3 alienda shule kifua mbele sababu alijua kila mtu kaona kupitia vyombo vya habari, na tokea siku hiyo yule mwalimu alikua rafiki yake.Akiwa na umri
Miaka 15 Liverpool walimchukua na baadae akapanda Team ya wakubwa . Nadhani tunakumbuka triple "S" Chini ya Brendan Rodgers. Suarez,Sturige,Sterling. Muda huo alikua akiwaza mkataba tu ili aweze kuwanunulia nyumba wazazi wake waachane na maisha ya kudaiwa kodi.Kwel alifanikiwa
Kweli alifanikiwa kununua nyumba ya mama yake na dada ake.Nothing compares to motherly and Sisterly love
bila hawa tusingemfahamu Sterling.kuna msemo unasema "there is first time for everything ".miaka 17 alifanikiwa kucheza uwanja wa ndoto yake Wembley.

So Raheem anaamini katika maisha anayo yaishi sababu amepitia hustle.
"If you grew up the same way i grew up don't listen to what certain tabloids want to tell you, they just want to steal your joy, they just want to pull you down".
Raheem sterling

#WapwaTuinuane
"If you grew up the same way i grew up don't listen to what certain tabloids want to tell you, they just want to steal your joy, they just want to pull you down".
Raheem sterling


#WapwaTuinuane