"Unataka kuuza maji yenye sukari maisha yako yote au ongozana nami tukaibadilishe dunia" ni maneno kutoka kwa Steve Jobs muanzilishi wa shirika la Apple akimwambia aliekuwa mkurugenzi wa Pepsi kumtaka awe mkurugenzi wa Apple na aachane na kazi ya kuuza maji yenye sukari(soda)
....hatua iliyomgharimu Steve mbeleni. Ndani ya miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980 Steve alikuwa ni kama nyota mpya inayong& #39;aa katika ulimwengu wa teknolojia na ujasiriamali, ni kutokana na chachu, upya au mabadiliko yaliyo kuwa yakiletwa na shirika lake changa Apple
Hatua na maamuzi ya kumuajiri aliekuwa mkurugenzi wa Pepsi na kuwa mkurugenzi wa Apple yalitokana na baraza kutoamini uwezo wa Steve kwasababu hakuwa mtu mwenye historia ya kufanya kazi ya usimamizi au kuwapo kwenye nafasi ya ukurugenzi sehemu yeyote ile hivyo
....hakuwa na sifa ya kuwa mkurugenzi hata katika shirika lake alilolianzisha yeye mwenyewe, Steve alilielewa hilo na hata kazi ya kumtafuta mtu ataefaa kuwepo katika nafasi hio aliisimamia mwenyewe na mwishowe kumchagua John Sculley aliekuwa mkurugenzi wa Pepsi 1977-1983
Miaka hiyo ya 1980 shirika liitwalo IBM ndilo lililokuwa likiongoza katika utengenezaji na uendelezaji wa teknolojia ya computer hivyo moja kwa moja Apple ilikuwa ikishindana na IBM, Steve alikuwa na jukumu la kuishinda IBM au bidhaa za IBM kwenye mauzo, pamoja na team yake
....walipewa mradi ulioitwa Macintosh wenye matarajio ya kuishinda IBM na kuwa kama bendera ya Apple, Steve pamoja na team yake walifanikiwa kuumaliza mradi huo na kuukabidhi kwa ndani ya miaka miwili lakini haukufikia matarajio viongozi wa baraza waliyokuwa nayo
....kitendo kilichomfanya Sculley kufanya maamuzi ambayo Steve hakuyapenda kabisa

Sculley aliamua kumuamisha Steve kitengo cha kuiongoza team ya Macintosh na kumuweka mbali kabisa na mradi huu, maamuzi haya kwake Steve yalikuwa kama kufukuzwa kazi kabisa katika shirika
....alilolianzisha yeye mwenyewe na kwa hasira alienda moja kwa moja kwa viongozi wa baraza na kuwa eleza lakini viongozi nao wakawa upande wa Sculley na kutomsikiliza Steve, Steve baada ya hapo akaacha kazi kabisa katika shirika hilo japokuwa uvumi nje ya shirika
....wengi walizani kafukuzwa katika shirika alilolianzisha yeye mwenyewe, alirudi katika shirika hilo baada ya miaka 12 toka alivyo ondoka na kuubadilisha ulimwengu wa teknolojia kwa kishindo, 2001 aliizindua bidhaa iliotoka mikononi mwa team aliyo kuwa akiiongoza
....bidhaa iliyo itwa iPod na milele bidhaa hiyo ikabadilisha ulimwengu wa muziki, 2007 alizindu smartphone iliyokamilika ya kwanza duniani maarufu kama iPhone na milele imebadilisha ulimwengu wa mawasiliano vivyo hivyo kwa bidhaa kama iTunes, Macbook na iPad, leo hii
....Apple ni shirika kubwa duniani likiwa na thamani zaidi ya trilioni 2,300 na ndilo shirika la kwanza duniani kufikisha thamani ya zaidi ya trilioni 2,300

Imeandikwa na @OscarFMbilinyi

#NyuziZaDropOut

RT kule juu iwafikie wengi, like na toa maoni yako. Shukurani
NT. Takwimu za kifedha katika uzi huu ni za kitanzania
You can follow @OscarFMbilinyi.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: