MBINU MATATA INAYOTUMIWA NA MATAPELI WA FACEBOOK

Facebook ni Mtandao maarufu sana, watu wengi hukutana kupitia Facebook ingawa kuna mitandao mingi sana ya kijamii, kupitia Facebook unaweza kutana na picha za mtu na historian yake kwa ujumla.
Matapeli wanatumia wa Facebook
sababu ni njia rahisi ya kupata taarifa za mtu, tapeli anaweza akawa nchi yoyote duniani ili kutimiza lengo Lake. Anachofanya ni kutengeza profile nzuri yenye picha za binti anayevutia Baadae anatafuta mlengwa yani mtu ambaye atamtapeli.
Mlengwa anayetafutwa hapa ni yule mwenye marafiki wengi na picha za kutosha kwenye account yake pamoja, pia inakuwa vizur zaid kama mlengwa ataweka wazi information za watu wake wa karibu yani wazazi au marafiki katika profile yake au kupitia post zake uko Facebook
Kinachofuta tapeli uyo atakuomba urafiki na ikumbukwe kwamba mlengwa namba moja ni mwanaume aliyeoa au mtu maarufu au kijana atokae familia ya kitajili. Baada ya mlengwa kukubali urafiki na tapeli uyo basi picha ndo linaanzia apo.
Tapeli hatakuwa na haraka atatumia muda wa kutosha kuhakikisha kwamba anajenga mahusiano mazuri na wewe, kwakuwa tapeli anatumia picha nzuri za mtoto kike basi mlengwa wetu anatekwa kiakili taratibu bila yeye kujua.
Inaweza pita ata miezi 3 au zaidi tapeli akijalibu kumsoma vizur mlengwa wake na siku zote mawasiliano yanakuwa kwa njia ya kuchati na kama mlengwa akimbana sana tapeli uyo ili asikie sauti yake basi tapeli ataomba msaada kwa tapeli wa kike,
yaani utaongea na tapeli wa kike na utaskia sauti ya kike na wasiwasi utakutoka. Baada ya mahusiano ya kirafiki kujengeka basi tapeli ataanza kukutega ili muwe wapenzi, hapo ndipo anapokuingiza Katika mtego wake.
Mkishakuwa wapenzi basi atakuomba umtumie picha zako za uchi na yeye anakutumia picha ambazo si zakwake, baadae atakuomba umtumie video za uchi ukifanya vitu va ajabu ambavyo usingependa mtu yoyote avione.
Tapeli atakikisha kwamba anapicha na video zako nying za uchi.. Yaani za kutosha, sasa Kinachofuata ni kutafuta sababu ya nyinyi kugombana, akifanikiwa katika hilo na hapo ndipo atakuweka kitimoto
Tapeli ataomba atumiwe kiasi cha pesa la sivo ataziposti picha zako na video zako kweny mtandao wa Facebook na kwakuwa anawafahamu watu wako wa karibu kupitia Facebook yako basi atakwambia usipomtumia atatuma video hizo na picha zako kwa watu wako wa karibu.
hasa wale unaowaheshimu kwa mfano mkeo au rafiki wa karibu au mzazi au Katika grupu lolote ulilo jiunga uko Facebook. Watu wengi wamekuwa wakitapeliwa kwa njia hii na wengi wamejiua kutokana na presha na msongo wa mawazo waliopata toka kwa Matapeli hao.
Kuwa makini sana unapotumia mitandao ya kijamii...please Repost this thread u might save someone from the trap
You can follow @Profesa_.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: