#UZI
#BusaraZaBonge
My future wife ita na mashoga zako na wake watarajiwa wa watu wengine kuna ujumbe wenu hapa. Usilalamike ukaona kuwa sijali confidentiality kati yatu, hapana! nafanya hivi kwa maslahi ya wengi.
#BusaraZaBonge
My future wife ita na mashoga zako na wake watarajiwa wa watu wengine kuna ujumbe wenu hapa. Usilalamike ukaona kuwa sijali confidentiality kati yatu, hapana! nafanya hivi kwa maslahi ya wengi.
Huenda nikakukosa wewe na haitokuwa sababu ya mimi kutotafuta mtu mwengine kusukuma gurudumu langu la kimaisha na si kila mtu anaweza kumuambia mtu wake maneno kama haya. Kwahyo nikaona nisiwe wachoyo kwenye hili. "Kizuri share na mwenzio". Haya na wajuba njoeni mchukue madini .
Mpaka nafikia hatua ya kukuita my future wife ni dhahiri kabisa kuna mengi tumepitia. Nmekuridhia kiasi kwamba hata nikikurupushwa leo nikuchukue kwa lazima, nafsi yangu haitosita wala kuwa na unyonge kuwa nimelazimishwa kufanya hivyo kwasababu ni kitu ambacho nimekua nikikitaman
na ninamuomba Mungu aniafikishe katika kufikia lengo la kuniunganisha na wewe kama mke&mume
My future wife ndoa ni zaidi ya harusi. Ni zaidi ya zile sherehe na tafrija zitakazowafanya watu wale, wanywe na kucheza kwa kufurahia siku yetu tukufu na ya kihisitoria katika maisha yetu
My future wife ndoa ni zaidi ya harusi. Ni zaidi ya zile sherehe na tafrija zitakazowafanya watu wale, wanywe na kucheza kwa kufurahia siku yetu tukufu na ya kihisitoria katika maisha yetu
Ndoa ni zaidi ya ule usiku ambao huenda kwa mara ya kwanza utakuwa huru kunipokea kimwili pasi na kuwa na uoga wa "what if nikishika mimba". Ndoa ni tofauti na zile siku saba za kuubariki upya wetu na kupongezana kwa kitendo chetu cha kuyaingia maisha mapya. Ndoa ni zadi ya hayo
Ndoa ni mimi na wewe kama familia mpya inayojitegemea na iliyohuru ambayo itakua imejengwa kwa misingi miwili ya mapenzi ya huruma baina yetu. Kwa kuanzia ni hayo na mengine yatakayofuata baada ya hapo ni kama zawadi. Wewe mimi kwangu ni baraka ya kwanza na nyingine ni nyongeza.
My future wife najua umenipenda mimi kwa sababu zako binafsi. Sijui wakati unanipenda mwanzo your first impression ilikua ni nini?.. Huenda ilikua ni utanashati, ucheshi, kujali, pesa ama kitu kingine chochote. Lakini kwa sababu yoyote ile iliyokufanya unipende najua wazi kuna
mtu ni bora zaidi katika hilo na umewaona ila bado ukaamua kunipenda. Ndiyo! Wapo kama ni kwasababu ulinipenda kwa sababu nilikupenda mwanzo najua kuna watu walikupenda na bado wanakupenda zaidi ya ninavyokupenda mimi lakini umeamua tu kunitunuku upendo wako na kuniheshimisha.

My future wife life is all about ups and downs. Huenda tutakuwa na wakati mzuri na wakati mwengine mambo yanaweza yakabadilika. Tunaweza kukosana au kupishana katika baadhi ya mambo. Nakuomba sana please! please! please! don't take it personal. Usichukue uamuzi wa kukaa kimya...
utakutafuna wewe na utanimaliza mimi na kilichotuunganisha kati yetu. Mtu pekee unaeweza kukaa nae chini ukazungumza nae kuhusu matatizo yangu na yetu ni mimi. Usitoe mguu kwenda sehemu nyengine kutafuta suluhu kwa sababu haujui watakupokeaje. Ni kweli wazazi wako wanakupenda.
na katika vitu hawataki kuviona ni kukuona ukipata tabu na kuhuzunika. Usikimbilie kwao wakati bado tuna nafasi ya kukaa chini tukayamaliza. Usifanye hivyo mpaka pale kutakapokua na ulazima wa kufanya hivyo. Kwa sababu unaweza kupoteza hata unachokipambania.
My future wife huenda sikupata nafasi ya kukaa na wewe kabla ya kuwa mke na mume. Ni jambo jema pia. Tumelelewa kwenye familia tofauti na hata misingi ya malezi yetu inaweza ikawa inapishana. Kuna mambo huenda yakawa yanakukwaza kutoka kwangu ambayo yanaweza kuwa ni hulka za...
za kawaida za kibinadamu au kutokujua. Kuna wakati ninaweza nikakukwaza nikiwa katika harakati za kukufurahisha pasi na mimi mwenyewe kujua inatokea. Huenda lengo langu jema kutokana na experience yangu ya malezi, makuzi na mazingira yaliyonikuza yakawa kinyume na wewe na lengo..
...langu jema likaonekana baya kwa sababu hiyo. Kwa sababu hizo kipenzi changu mke wangu mtarajiwa naomba unielewe zaidi ya kunivumilia. Ndiyo unielewe zaidi kwa sababu uvumilivu una kikomo na utafika wakati utashindwa na huenda ikawa ndio sababu ya kuuanza mwendo wa dhiki na...
... mifarakano katika maisha yetu ya ndoa. Ninakuomba unielewe sana kwa sababu itasaidia kunielewesha hata pale itakapobidi kufanya hivyo.
My future wife, mimi ndiye nitakaekua mumeo. Mimi ndiye nitakaekuoa. Hata kwenye cheti chetu cha ndoa kutakua na majina mawili langu na lako. Hata kanisani watakaosimama madhabahuni ni mimi na wewe, msikitini watakaoshikana mikono ni mimi na walii wako atakaekuwepo kwa niaba yako
So it is all about me and you. Huenda ukawa unanifahamu mimi vizuri kuliko ndugu au marafiki zangu. Ninakushauri tu uwe mwema kwao na sio kwao tu kwa mtu yeyote yule. Ishi nao tu vizuri na hata ukiona kuna haja ya kufungamana nao kama marafiki au uswahiba ni ruksa kufanya hivyo..
sikukatazi na ni vyema kabisa. Ila ninachotaka kukuambia ni kuwa linapokuja suala la ndoa yetu ni mimi na wewe. Jaribu kutengeneza mazingira kuwa tupo mimi na wewe tu na hakuna mwengine baada yetu duniani. Mambo yote yanayoihusu ndoa usiyafungamanishe na kitu kingine nje ya hapo.
Mimi ndio mshirika wako namba moja kwenye ndoa. Kwenye mengine ruksa unaweza fanya unavyojiskia. Unaweza kuwa na patner wa kibiashara na ukaongea na mtu mwengine kumuomba mawazo kuhusu biashara yenu lakini sio ndoa yetu.
My future lovely wife. Nikishakuoa utabeba identity yangu. Huenda ukachukua jina langu au kujulikana kwako tu kuwa huyu ni mke wa fulani. Kwa upande wangu ninakuahidi kuheshimu na kukujengea heshima hata kwa watu wengine.
Kikubwa zaidi utakua umebeba utu wangu na heshima ya nyumba yangu. Huko mitaani utakua unatembea na kivuli changu. Chunga sana staha yako na yangu pia. Niheshimishe mbele za watu kwa ile namna watakavyokuheshimu wewe.
Heshima yangu haitokua kitu mbele za watu na nitaonekana mtu wa hovyo kabisa kwa kushindwa kuiongoza nyumba yangu akiwemo mke wangu mwenyewe hadi kufikia hatua ya kufanya mambo yatayoivunjia heshima nyumba yetu.
My future lovely wife, aibu yangu ni aibu yako na aibu yako ni aibu yangu pia. Unaweza kukaa kuongea kuhusu habari zangu na wakakusikilza vizuri na wakacheka kwa sababu ni hulka za watu kupenda kusikia habari za watu wengine zisizowahusu na zisizoongeza chochote kwenye maisha yao
zaidi ya kutumika kama kigezo cha kuvulia nguo watu wengine. Vyovyote itakavyokua ninakuomba sana usije ukanivua nguo mbele za watu na mimi pia ninaahidi kuficha aibu zako. Nitakutetea hadharani na kukukanya faraghani pale itakapobidi.
My future lovely wife, najua ni ndoto ya kila mtu kuwa na maisha mazuri na kumiliki vitu vizuri kwa sababu kama binadamu tumeumbiwa kupenda vitu vizuri. Hata tunapokosa tunashukuru tu kwasababu tumevikosa lakini nafsi zetu bado zinavitamani.
Inaweza kutokea nikashindwa kukupa maisha mazuri unayoyatamani, lakini ninakuhakikishia kuwa ninaweza kukupa maisha nitakayoweza kuyapata all of it. At least be greatfull for that na uniombee na usinifanye nikajifeel less a man. Nafahamu kuwa you deserve everything good.
Kwa nafasi yangu nitalipambania hilo nizidi kuwa bora zaidi na wewe uweze kuufurahia ubora wangu.
My future lovely wife, huenda mungu akatubariki kwa zawadi ya watoto. Ni zawadi bora kabisa kwa wanandoa lakini haikufanyi wewe kutokua mke bora endapo utashindwa kuniletea watoto. Mungu amenibariki kwa mambo mengi sana ikiwemo kunikutanisha na wewe.
Ikitokea tukapata watoto naahidi kuwa baba bora. Inaweza ikatokea nikashindwa kuwa na muda wa kutosha na watoto katika harakati ya kuwatafutia maisha bora wewe na watoto wangu. Ikitokea hivyo usiache kuwakumbusha kuwa baba yenu yupo anawahangaikia na anawapenda.
Na hata ikitokea tukakosana nakuomba usiwaingize watoto katika migogoro yetu na wala usiwapandikize chuki. Endelea tu kuwakumbushe tu kuwa baba yao ninawapenda sana na ninawapambania kuwapa maisha bora hata kesho nikiondoka waseme tulikua na baba yetu na....
.... baba yetu na ndiye ametufikisha hapa kwa mapenzi ya mungu na waniombee dua zitakazoniweka sehemu nzuri huko niendako
My future lovely wife. Mwisho kabisa ninamuomba mungu akuongoze uwe mke mwema na mama bora wa wanangu ili hata ikitokea ikanibidi kuondoka basi niondoke kwa amani nikijua kabisa nimewaacha wanangu katika mikono iliyo salama.
Ninakupenda
Ninakupenda
