KLEIST SYKES alianzisha TAA mwaka 1930 na baadae ikawa TANU ya kina Mwl. Nyerere. Alizaliwa mwaka 1894 huko Pangani, Tanga. Baba yake Sykes Mbuwane alikua Mzulu wa Afrika Kusini aliyekua akifanya kazi kwa Wajerumani na Mama yake alikuwa mkulima wa Kinyaturu. Baaada ya baba...
...yake kufariki Kleist, alihamia Dar es salaam ambapo alipigana vita ya kwanza ya dunia akiwa upande wa Mjerumani. Baada ya vita alipata kazi kwenye kampuni ya reli ambapo alikutana na Mghana Aggrey aliyemshawishi kuanzisha TAA. Kleist pamoja na wenzake kina Mzee bin Sudi,....
....Cecil Matola, Suleiman Mjisu na Raikes Kusi walianzisha umoja huo na kujenga makao makuu mtaa wa Lumumba, Dar es salaam ambapo mwaka 1954 palizaa TANU na sasa ni Makao Makuu ya CCM. Kleist alikua Mwafrika wa kwanza kufanya kazi katika Jumba ya biashara la Tanganyika na wa....
....pili kufanya kazi Halmashauri ya manispaa ya Dar es salaam kipindi kile cha mkoloni. Kleist alikua na vijana watatu Abulwahid, Abbas na Ally(Pichani). Marehemu Ally Sykes mtoto wa Kleist Sykes ndiye mmiliki wa Kadi namba 2 ya TANU.🔥

'MWISHO
You can follow @tweetsrifle.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: