Utunzaji wa midomo ( lips). Kama unavojali na kutunza ngozi ya uso wako, vivyo hivyo lips pia ni kiungo kinachohitaji matunzo ili kuendelea kuongeza mvuto na kukufanya kuendelea kua mrembo zaid.Mara nyingi kipind cha hali ya hewa ya barid hufanya midomo (lips) kuwa mikavu hali
hii hupelekea maumivu midomon na mara nyingne lips kupasuka.
Kuna njia mbal mbali za kutunza na kulainisha lips zako.Ambazo ni

1.Kunywa maji ya kutosha.
Kwa kawaida Binadam huitajika kunywa maji angalau glass 6-8 kwa siku. Unywaji wa maji utakusaidia kupunguza kukauka kw ngozi
ya mdomo ivo bas huondoa tatzo la kupasuka,hulainisha midomo (lips) yako na kuifanya kubaki na unyevu wakati wote.

2.Tango.
Kata tango kipande na uweke juu ya lips zako kwa mda wa dk 20.Maji yanayopatkana katk tango husaidia kulainisha, kung'aza na kuponesha sehem zilizoathirika
kutokana na ukavu.

3.Scrub ya sukari na mafuta ya nazi au maj.
Changanya sukari na mafuta ya nazi au maji.kisha weka juu ya lips zako subr kw md wa dk 20 hadi 30.Scrub hii husaidia kuondoka ngozi mfu na ngozi kavu.

4. Mafuta ya nazi.
Paka mara kw mara inasaidia kufanya midomo
iwe na unyevu na pia ing'ae wakati wote.

5.Asali na oliva oil.
Mchanganyiko huu hutumika kama tiba. Ni dawa kw lips zilizopasuka na kuathirika na ukavu.Paka mchanganyiko huu kabla ya kulala.

6 Paka mafuta ya petroleum jelly kabla ya kwenda kulala.
Hii husaidia kufanya lips ziwe laini na zenye kuvutia. Ukijenga Tabia ya kufanya hivi mara kwa mara itafanya midomo yako ivutie wakati wote.

7.Tumia lip balms.
Lipbalms zinazoshauriwa hapa ni zile zinazo saidia kukulinda na athari zinazotokana na mionzi ya jua.
8.Kula vyakula vinavojenga mwili.
Vyakula vyenye Vitamin B na C ni muhimu sana katika Afya ya ngozi. Ni vyakula kama mayai,nyama,samaki,matunda na mboga za majani.Ulaji wa vyakula hivi kwa wingi husaidia kujenga afya ya ngozi na midomo (lips) yako kwa ujumla.
Mwisho,Epuka tabia za kulamba midomo kila wakati na kung'ata kucha hii itakusaidia sana katika utunzaji wa midomo (lips) yako.
You can follow @Maggystylish.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: