MICHAEL GERARD TYSON - The Baddest Man on the Planet.
.
Ni Bondia Hatari Zaidi Kuwahi Kuingia Kwenye Ulingo wa Ngumi. Alipewa Jina la IRON yani CHUMA Kutokana na Uzito wa Ngumi Zake. Anashikilia Rekodi ya Kuwa Bingwa wa Dunia wa Uzito wa Juu Akiwa Na Umri Mdogo.
.
threads - uzi🧵
Alizaliwa Brooklyn, New York mwaka 1966. Baba yake mzazi aliyeandikwa kwenye Cheti cha kuzaliwa ni Mjamaika Purcell Tyson ila alilelewa na Baba wa Kambo Jimmy Kirkpatrick ambaye alikuwa ni mlevi na mzururaji. Akiwa na miaka 13 tu Tyson alikuwa ameshakamatwa na polisi mara 38....
....Mama yake alifariki akiwa na miaka 16 na kumuacha chini ya uangalizi wa mwalimu maarufu wa masumbwi Cus D'Amato, ambaye baadaye alimchukua kama mwanaye kisheria. Tyson anaeleza kuwa hakuwahi kuwa na mahusiano mazuri na mama yake, wala mama yake hajawahi kijivunia kumzaa....
....alikuwa akimuona kama mbabe, mwizi na mzururaji. Akiwa mtoto wenzake walimtania na kumcheka sana kutokana na sauti yake ndogo na kithembe. Mara ya kwanza Tyson kupigana ni baada ya kijana mmoja kumnyonga njiwa wake, alimtandika ngumi ndipo akagundua ngumi ni silaha yake....
.....Kabla hajaingia kwenye ngumi za kulipwa, Tyson alishinda medali mbili za dhahabu mwaka 1981 na 1982 kwenye michezo ya Olimpiki ya vijana. Na akiwa na miaka 18 mwaka 1985, rasmi Tyson alianza ngumi za kulipwa ambapo alimtandika Hector Mercedes TKO raundi ya kwanza....
....Kwanzia hapo aliendelea kushinda mapambano 28 mfululizo kati ya hayo 26 yalikua KO na 16 kati ya hizo zilikuwa KO za raundi ya kwanza. Vichapo vyake vikaanza kuvutia vyombo vya habari, lakini ghafla novemba mwaka 1985, Mwalimu na Baba yake mlezi D'Amato alifariki dunia....
....Pambano la kwanza la Tyson kuoneshwa na TV kubwa ilikua mwaka 1986 alipozichapa na Jesse Ferguson. Tyson alimdondosha Ferguson roundi ya tano baada ya kumpiga ambakati(uppercut) ambayo ilimvunja pua. Novemba 1986, Tyson alipigana pambano lake la kwanza la kuwania mkanda....
....wa uzito wa juu wa WBC dhidi ya bingwa wa wakati huo Trevor Berbick, Tyson akiwa na miaka 20 tu alimtandika Berbick roundi ya pili kwa TKO na kuwa bingwa mdogo zaidi wa uzito wa juu katika historia. Nguvu, spidi, uhakika na timing vilimfanya awe tishio kwa wapinzani wake....
....na matumaini kwa Tyson yakawa makubwa. Aliendelea kutembeza vichapo na mwaka 1987 alimtandika James Smith na kuchukua mkanda wa WBA, baadae mwaka huo huo alimchapa Pinklon Thomas na kuchukua mkanda wa IBF. Na alikua bondia wa kwanza kumiliki mikanda mitatu mikubwa kwa....
....wakati mmoja yaani WBC, WBA na IBF. Mwaka 1988, Tyson alipanda ulingoni na nguli wa ngumi Larry Holmes na kutetea mikanda yake kwa kumtandika legend huyo kwa KO roundi ya nne. Mwaka huo huo alimuoa mwigizaji Robin Given lakini waliachana kwa madai Tyson alikua akimpiga....
....Mwaka 1990 katika hali ya kushangaza, kwa mara ya kwanza Tyson alipoteza mchezo, tena kwa bondia wa kiwango cha kati James Doglas na kupoteza mikanda yote. Baada ya mchezo huo kwa hasira Tyson alishinda michezo 4 mfululizo lakini mwaka 1992 alipata kesi ya ubakaji.....
....Alishitakiwa na kufungwa kwa miaka 3, mpaka 1995. Alirejea tena ulingoni mwaka 1996 na kushinda tena mikanda miwili ya WBA na WBC kirahisi. Baadae 1996 alipata pambano na bingwa wa zamani wa ngumi Evander Holyfield na Tyson alipoteza tena kwa mara ya pili kwenye historia....
....yake ya ngumi kwa TKO raundi ya 11. Katika pambano maarufu la marudiano baina ya Tyson na Evander mwaka 1997, Tyson alipoteza vigezo baada ya kumng'ata Evander sikio mara mbili na kupokonywa leseni yake ya ngumi. Tyson alirudishiwa leseni yake mwaka 1999 na kumtandika....
....Franz Botha kwa KO roundi ya 5. Ukorofi wake uliendelea ambapo mwaka 2000 kwenye pambano dhidi ya Lou Savarese, ilishuhudiwa Tyson akiendelea kumpiga Lou Savarese wakati refa alikua ameshasimamisha pambano na kupelekea kumjeruhi refa, baadae mwaka huo huo alipanda ulingoni...
....na Andrew Golota na kumtandika KO raundi ya 3 lakini matokeo yalifutwa baada ya kugundulika kuwa Tyson alikua amevuta bangi. Pambano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kati ya Tyson na Lennox Lewis ambaye alikuwa akionekana kama ndiye mtu aliye kwenye kiwango cha Tyson kwa....
....wakati huo lilifanyika mwaka 2002. Ambapo Tyson alichezea kichapo roundi ya 8 kwa KO. Na hapo ndipo dunia ilikubali kwamba nyakati za Tyson zimefika tamati na sasa ni muda wa kizazi kipya. Mwaka 2003 Tyson alitangaza kufilisika na 2005 alitangaza kustaafu ngumi za kulipwa....
....Amekuwa akishiriki sinema tofauti na jina lake limeendelea kutajwa na kuandikwa kwenye Sinema na Muziki.

Tyson anabaki kwenye Historia kama moja ya mabondia bora wa kipindi chote.

'MWISHO

@McinikaWaLamar
You can follow @tweetsrifle.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: