Leo sijatumwa na mtu wala nini , nimeona mjadala unaendelea kuhusu Rapper Bora wa Muda wote , nikarukia tawi kama Nyani
Swali la msingi , Ili tuseme Dubo au Barry Magiri ni Rapper bora wa wakati wote tunatumia vigezo gani? Karibu 👇
" Nabii" katika muziki wa hip hop , KRS 1 aliwahi kusema " Hip Hop inawakilishwa na Rap lakini sio kila Rap ni Hip Hop "
Akimaanisha kwamba unaweza kuwa Rapper ila haufanyi Hip Hop

Mfano watu kama Kalidjo Kitokololo , Msafiri Diof ni marapa wazuri ila hawafanyi Hip Hop
1. Lyricism

Masuala mazima ya Mashairi
Ili mtu awe ama ajulikane kama Rapper bora kwenye Hip Hop lazima kwanza awe na mashairi "makali"
Pili awe na uwezo mkubwa wa kuandika mashairi yake mwenyewe
Mashairi ni ufunguo kwenye kitasa cha Hip Hop
Mtu anaweza kuuliza mashairi makali yakoje?
Kirahisi , Mashairi yenye ujazo na uzito , yenye mantiki
Hapa vitu kama Metaphors , Wordplays yanahusika

Rapper Canibus anasema " I break the laws of science with Metaphors and Lyrics "
2. Complete Body Of Work

Body of work kwenye muziki ni mkusanyiko wa kazi zote alizofanya msanii kuanzia Singles , EPs , Mixtapes na Albums.
Ili Rapper ahesabike kama Bora lazima awe na muundo wa kazi uliokamilika i.e Singles na EPs , Mixtapes na Albums
FYI : Sugu ana albums 10
Hapo kwenye Complete Body of Work , wachambuzi wa mambo wanaongeza kwamba lazima Rapper huyu tunayemuita BORA awe na angalau Classic album Moja
Classic album ni kitu gani?
Hii ni hadithi ya siku nyingine.
3. Cultural Impact / influence

Hip Hop sio muziki tu , Ni Utamaduni
Tunapozungumzia kigezo tajwa hapo juu , ni lazima Rapper wako awe na impact katika utamaduni huu.
Awe na ushawishi katika jamii kuhusiana na utamaduni huu.
Profesa Jay aliwahi kusema kwenye wimbo wa Nazeeka sasa

"Nilimshawishi baba yako akuruhusu uimbe "

Miaka ya nyuma , muziki ulionekana uhuni hivyo Aliyewezesha wazazi wetu waturuhusu kufuatilia muziki huu ana impact/Influence kubwa
Verse 2 👇
4. Delivery

Uwasilishaji wa Kazi
Marapa watano wanaweza kuongea kitu cha aina moja lakini tukamuelewa vizuri mmoja.
Hapa tuna maana kwamba namna Rapper anavyowasilisha ujumbe wake kwa hadhira ina uhusiano mkubwa na uwezo wake
Hivyo , Delivery ya Rapper wako lazima iwe YENYEWE
5. Flow & Cadence

Rapper anaweza kuwa na Mashairi makali (kigezo namba moja) , ushawishi n.k lakini kama mitambao yake haivutii ama haibambi lazima kuwe na changamoto
Lyricism + Delivery + Flow & Cadence ni vigezo muhimu sana kwa Rapper kuonekana bora
Cadence - kwa lugha nyepesi ni namna unavyotamka maneno yako katika wimbo kutengeneza mpangilio (Rhythm)
Cadence na Flow zinaenda sambamba
Great Rappers lazima wawe na Flow na Cadence maridhawa
6. Time

Tunakubaliana kwamba kuishi kwingi kuona mengi yeah?
Basi , ili Rapper wako awe kwenye kibangala cha Rapper bora wa muda wote lazima awe kwenye tasnia kwa muda kidogo
Sina idadi halisi ya miezi ama miaka lakini lazima awe amekomaa kisanaa.
7. Beat Selection
Rapper bora ni yule mwenye uwezo mkubwa wa kuchagua midundo mahususi kwaajili ya kazi yake
Kuna Rapper aliwahi kusema anachana vizuri mpaka kwenye Ringtone za Nokia (😂)
Midundo ni sehemu muhimu sana ya kazi ya Rapper Bora
Midundo ya Hip Hop
8. Best At Performance

Rapper/Emcee bora katika hip hop lazima awe na uwezo wa kutawala jukwaa na kuliongoza
MC - Tafsiri isiyo rasmi : Moves The Crown , Mic Controller
Muhimu kuwa Mchenguaji mahiri na Sio Mnenguaji mahiri.
9. Uniqueness / Own Style

Rapper bora ni yule mwenye mtindo ama style ya kipekee
Achana na wale wanaoiga mikogo na mbinu za wengine Rapper (mifano na majina Yapo)
muhimu awe "Spesho" kwa namna yake mwenyewe
Katika Sauti ,mitambao ,mashairi n.k
Hivyo ni vigezo kutoka vyanzo mbalimbali
Unaweza ukaongeza vingine ili tuongeze maarifa zaidi
Nakaribisha Maoni , Ushauri , Pingamizi na kila kitu

Je , Kwa vigezo tajwa hapo juu
Nani Rappers wako watano Bora ?
You can follow @MoruoKing.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: