AN OPEN LETTER TO MY FUTURE DAUGHTER 💌

Dear daughter,
Angekuepo bibi yako ambae pia ni mama yangu leo hii siku ya MAMA duniani basi ingemuhusu yeye zaidi, lakini binafsi nimeona niitumie siku hii kukuandikia barua ili siku ukizaliwa uikute
T H R E A D 👇
Nuru ya asubuhi haitofaa kitu bila kuona uso wako. Kifungua kinywa hakitakua na maana bila kupata kumbatio lako pindi unapoamka.

Lile tabasamu lako ukinikaribia ni ishara halisi ya binti shupavu aliyebeba urithi wa asili ya mtu mkarimu wa Afrika.
My daughter wewe ni MAMA AFRICA
Dear daughter, sidhani kama ntachelewa sana au labda ntawahi sana kukuleta duniani, lakini naamini wakati ukifika basi utakuja kuungana nasi.
Sina haraka sana ya kukupata maana nakutafutia mama ambae kwa urembo wake atakutoa binti mzuri ili usije ukamaliza pesa zako kwa make up😄
Kuelezea upendo wangu kwako ni sawa na kupima nguvu ya Tsunami.Nitakupenda pasipo mfano.
Dear daughter, nakuahidi kukupa exposure kubwa ili usije ukaanza kutumia computer ukubwani kama baba yako😄, utasafiri mahali tofauti ujifunze vitu vingi na namna watu wa maeneo tofauti
Wanavyokabiliana na changamoto za maisha.
Nitakuhimiza kuhusu elimu lakini sitokulazimisha uje kuwa nani wala kulazimisha utimize ndoto ambazo zilinishinda mimi. Sitokua nyuma bali nitakupa support yangu yote.

Role model wako atakua Hawa The Buss driver, nkimaanisha
Uwe mpambanaji na mwenye shauku ya kujikwamua kiuchumi wewe kama wewe
Dear daughter, ni vizuri kupata mwanaume ambae tayari ana maisha yake lakini ni vizuri zaidi ukimpata mwanaume wakati wewe tayari una maisha yako pia. Chako utakula bila masimango, cha mtu kina mingi misuguano
Mpendwa binti yangu, joho la hakimu mahakamani ni bora kuliko nguo fupi za makahaba pale barabarani. Vazi la kijani la matabibu pale hospitali ni la maana sana kuliko kuvaa dera nyumbani ukiwa umepewa mimba na mwanaume asiyefahamika na ndoto zako kuharibika.
Dear daughter, sijui utakuwa wa aina gani maana nitafurahi ukitoka mweusi ili nikuoneshe uzuri uliojificha ndani ya hiyo ngozi adimu, ntakuelekeza jinsi ya kuitunza mpaka ukipita juani iwe kama kimiminika cha dhahabu kinatembea❤
Nitafurahi zaidi pia ukija mweupe (light skin)
Ili basi kwa unyororo wa ngozi yako ivutie mno mpaka umeme ukikatika tukufanye taa vile unatumulikia mule ndani kwa ung'aavu wa ngozi yako 🤗

Duniani kuna mambo mengi sana Binti yangu, nitajitahidi kukusaidia kila utakapo hitaji msaada wangu. Ntahakikisha kadri ya uwezo wangu
Pesa isiwe chanzo cha wewe kujiingiza kwenye vishawishi vingi. iPhones, magari na starehe visiwe vya kukustua roho maana ntahakikisha mtu akikufata kukutongoza asiwe na maajabu mbele zako labda umpendee huruma tuu au nguvu ya penzi la dhati basi!!😁
Dear daughter, ntakuandaa uwe kiongozi kwa wadogo zako ili mwisho wa siku waamini jinsi na namna gani kuna nguvu katika mwanamke.
Kaka yako akikosea nitahakikisha wakati mwingine nimchape mbele zako ili akitoa machozi uone kumbe hata wanaume wanahisia na wanaumia. Hii itasaidia
Wewe kulinda hisia za wanaume na kuepuka kuvunja mioyo yao kwa kigezo cha kwamba hawaumii.

Mimi kama mwanaume nitakufundisha jinsi ya kuishi na jinsia ya kiume na mienendo ambayo itampendeza kila mtu maana elimu yako kubwa haitakuletea mume bora usipokua na tabia njema
My princess, furaha yangu ni kukusuka mabutu kabla ya kulala ❤
Nitakua baba yako,nitakua kaka yako,nitakua ndugu yako,nitakua dady nitakua mzee wako,nitakua mshua kulingana na wakati husika.
Mama yako ni mke wangu sio shoga yako wa kubishana au kuchambana nae 👌
Zaidi ni kwambie tuu nikishindwa kukurithisha marafiki zangu walio wema basi ntajitahidi nisikurithishe maadui zangu.😄
Regard your future father @Vet_doctor87
#End
#MyMindSpeak
#NohTalk ☕️
You can follow @Vet_doctor87.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: