MO DEWJI NI KWELI ANAUZA VITAKASA MIKONO?

Na Thadei Ole Mushi.

Sikutegemea katika hali Kama hii ya janga la Corona wale wenye Unafuu kwenye jamii yetu kufanya Biashara katika taharuki Kama hii. Nasikia hiki kitakasa Mikono Cha Mo Dewji anaviuza, sina shada naye kwa kuwa
ni mfanyabiashara ameona hii ni Fursa. Matajiri wenzake wanafanyaje duniani?

1. Jack Ma mwanzilishi wa Alibaba yeye kachangia mabilioni ya Shilingi kwa nchi yake ya China kupambana na Corona. Kavuka Mipaka kachangia hadi waafrika kwa mfano katoa ventilator 500, Nguo rasmi za
za wauguzi (Suits and face shields) 200,000, thermometer 2,000, Gloves 500,000 nk. Hivi katoa bure kabisa....

2.Bill Gates yeye na Mke wake Melinda wametoa offer ya Kujenga kituo Cha kufanya tafiti ya Chanjo ya Corona pale Marekani. Pia katoa mabilioni kadhaa kwa nchi yake
kupambana na Corona. Hivi katoa Bure kabisa ....

3.Strive Masiyiwa huyu ni tajiri wa Zimbabwe yeye katoa Offer kwa wafanyakazi wa afya kawaongezea Posho US Dollar 200 Hadi 400 kwenye mihsahara yao kwa Miezi sita. Kawanunulia pia Nguo, amewapa Usafiri nk. Hivi katoa bure kabisa.
4. Mark Zuckerberg huyu ni mmiliki wa Facebook yeye katoa 231,440,000,000 kwa wafanyabiashara wadogowadogo. Katoa pia mabilioni kibao kwa WHO na US center for Disease

5.Jim Ratcliffe huyu ni bilionea wa Uingereza anamiliki Kiwanda cha Kemikali, katoa Senitiser kwa hospital zote
bure UK.

6. Aliko Dangote ametoa N 200 Milioni kupambana na Usambaaji wa Corona Nigeria sawa na Shilingi Bilioni Moja Plus. Hizi naye katoa bure kabisa ....

7. Jeff Bezos huyu ni mmiliki wa Amazon (E- Commarce) yeye katoa US dollar 100 Milioni kwa ajili ya wanaopoteza Ajira.
List ni kubwa Sana ya waliojitoa Bure.

Hapo Kenya mfuatilieni Governor wa Mombasa Joho anachofanya pitia hii link kuona Instagram yake
Anagawa hadi Chakula bure kabisa kwa wakenya wa Mombasa. Ameshirikiana na private Sector kutengeneza Centre ya Waathirika wa CORONA

Mfuatilieni Mzee wa Mishe Sonko yeye anagawa Chakula Kenya bure kabisa na ameenda mbali anawagawia watu hadi Pombe.

Hapa Kwetu matajiri wapo wapi
Mo kashaamua kutuuzia vitakasa Mikono, siamini kwa jinsi tulivyomtafuta alivyopotea. Hakupaswa kuona Kama hii Ni fursa....

Wasanii wetu ambao ni Celebrate wapo wapi wanashindwa kujiunga kutoa hata kitu kwa jamii?

Wanasiasa wetu wapo wapi? Hapo Bungeni mnashindwa kujiunga hata
mshahara au Posho ya Kikao kimoja mtoe?

Hawa ni watu wenye unafuu kwenye jamii yetu kwa nn msifanye kitu? Wafanyabiashara wadogowadogo wamepoteana, wafanyakazi sector binafsi baadhi wamepoteana, watoto yatima kwenye Kambi zao wamepoteana, watumishi wetu wa Afya tuwanunulie
hata Mask za viwango jamani, ni wakati wa kurudisha kidogo kwa jamii.

Tusiiachie Serikali tu...

Ole Mushi
0712702602
You can follow @Pdizaina05.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: