Warren Buffett nguli maarufu wa uwekezaji kutoka nchini Marekani alianza kwa kubadili taka kuwa dhahabu na kutengeneza utajiri ambao ni zaidi ya uzalishaji wa nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, hukadiliwa kuwa na utajiri wa zaidi ya trilioni 169, tuiangazie kidgo stori yake 👇
Alizaliwa mnamo tarehe 30 mwezi agusti 1930 uko Omaha Nebraska, Marekani ambako hadi leo hii huishi, akidai kwamba sehemu ile huipenda sana na hakuweza jiona akiishi vizuri sehemu nyingine zaidi ya Omaha, mbali na ivyo nguli huyu hufahamika kutokuwa na makuzi wala matanuzi
Japokuwa anamiliki mpunga mrefu sana, mfano kitu cha thamani yeye anachomiliki mbali na uwekezaji wake ni ndege binafsi tu ila nyumba anayoishi hadi leo hii aliinunua miaka ya 1950 kwa bei isio zidi bilioni 1.3 na kwa upande wa magari, ana gari moja tu ambalo hulitumia kila siku
Kuendea kazini, pia huendesha mwenyewe na si kuendeshwa, nguli huyu pia ni maarufu kwa kuwa na mlo usiopangiliwa tofauti na nguli wengine wengi yeye hula vyakula kutoka McDonald ambavyo vinaweza mgharimu 6,000 tu kwa mlo

Husemekana anatumia zaidi ya masaa 8 kusoma na husoma
Kurasa zaidi ya 400 kwa siku, yote hii pia ni sehemu ya kazi yake kwani kutambua kuwa hisa fulani ni taka na fulani ni dhahabu inahitaji kufanya chambuzi yakinifu kwa kiasi kikubwa

Akiwa na umri wa miaka 6-7 milango ya ujasiriamali ilianza funguka kwake, kutokana na shawishi ya
Baba yake mzazi aliekuwa wakala wa hisa, akajikuta katika umri mdogo kabisa anakuwa mwenye hamasa na uwekezaji pia utajiri, hakuishia kutamani na kuhamasika tu katika umri huo huo alifanya shughuli mbali mbali zilizo kuwa zikimuingizia kipato kidogo, na alipo maliza elimu ya kati
(High school) alikuwa na akiba zaidi ya milioni 30 ambayo aliitumia kununua shamba la ekari 40 na kulikodisha kwa wakulima

Akiwa shule alikuwa akiwaambia wenza wake kwamba atapofika umri wa miaka 30 atakuwa milionea (bilionea kwa fedha za kitanzania) na asipokuwa milionea
Atajirusha kutoka juu kwenye ghorofa refu hadi chini, ahadi hii aliitimiza japokuwa kwa kuchelewa kwani alikuwa milionea akiwa na miaka 32

Pia akiwa bado shule (chuo cha Columbia business school) alikutana na mwalimu wake ambae amebadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa na hata
Kuwapo hapa alipo leo hii, Benjamin Graham( muandishi wa kitabu maarufu kwa wawekezaji, the intelligent investor) pia hufahamika kama baba wa uwekezaji wa thamani akitamba na falsafa yake ya kununua hisa yenye thamani ya 2000 kwa 1000 (hapa wanabiashara mmenielewa bila shaka)
Falsafa hii pia Warren Buffett ameitumia sana na ilimpa mafanikio, lakini kama ilivyo kwa wanafunzi wazuri hujifunza kwa Mwalimu na baadae huwa bora zaidi ya mwalimu na hufanya makubwa, ndivyo ilivyo kuwa kwa Warren Buffett hakuishia kununua na kuangalia hisa ambazo hazifanyi
Vizuri au ambazo hazipewi thamani yake halali tu alienda mbali zaidii....

Itaendelea.......
Imeandikwa na @OscarFMbilinyi

Kama umeipenda usiache kunifuata ukapata zingine nyingi kama hizi,RT iwafikie wengi, like na toa maoni yako

#NyuziZaDropOut
NT. Takwimu za kifedha katika uzi huu ni za kitanzania
You can follow @OscarFMbilinyi.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: